MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji.
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimu
Elimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Wanataaluma wamejitahidi kutoa maana ya elimu kuwa ni mabadiliko ya tabia yanayotokana na ujuzi. Kwa maana hii Elimu haiishii kwenye kuijua tu bali elimu hukamilika inapomwezesha mwenye kujua kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko yule asiyejua.
Nani aliye elimika?
Kutokana na maana ya elimu tuliyojifunza hapo juu, mtu aliyeelimika ni yule ambaye ujuzi alioupata humuwezesha kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko pale alipokuwa hajapata ujuzi huo. Mtu aliyesoma hatachukuliwa tu kwa kirahisi kuwa kaelimika, bali kuelimika au kutoelimika kwake kutathibitika katika matendo na mwenendo wake wa kila siku. Matarajio ni kwamba mtu aliyesoma anapaswa aelimike kwa kutenda kwa ufanisi zaidi kuliko asiyesoma. Ni katika kuzingatia hili Allah (s.w) anatukumbusha katika Qur-an:
“... Sema, Je! wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” (39:9)
Jibu la swali hili ni wazi. Mjuzi na asiyejua hawawezi kuwa sawa kiutendaji na kitabia. Endapo mtu atajiita msomi kwa kusoma vitabu vingi au kupewa shahada nyingi lakini kitabia na kiutendaji akawa hatofautiani na wale wasiosoma atakuwa bado hajaelimika na mfano wake ni ule unaopigwa katika Qur-an:
“Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua (kwa kuitia katika matendo) ni kama punda aliyebeba (mzigo) wa vitabu vikubwa (bila ya kufaidika kwavyo) ni mbaya kabisa mfano wa watu waliokadhibisha aya za Mwenyezi Mungu. Na Mw enyezi Mungu haw aongoi w atu m adhalim u.” (62:5).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Swala ya jamaa na taratibu zake
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya jamaa na taratibu zake.
Soma Zaidi...benki za kiislamu na njia zake za kuingiza kipato
Benki za KiislamuBenki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba.
Soma Zaidi...Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.
Soma Zaidi...