MAFUNZO YA ANDROID JAVA SOMO LA 2:


picha


katika somo hili utajifunza kuhusu sehemu kuu za android studio.


SEHEMU KUU ZA ANDROID STUDIO:

Kama wewe ni kwanza unaanza kujifunza kutengeneza App basi utahitajika kujifunza kuhusu android studio inavyofanya kazi. Katika somo hili utajifunza sehemu kuu za android studio ambazo ni lazima uzijuwe.

 

Sasa kabla hatujaanza kuziona hizo sehemu kuu zza androis studio, kwanza nitakupa maelekezo uweze kutengeneza app yako ya kwanza. Ambapo hiyo app ndio tunakwenda kuitumia kwenye somo hili.

 

  1. Bofya android studio kuifunguwa
  2. Hatuwa ya pili baada ya kufunguwa bofya palipoandika new project 

 

  1. . Bofya hapo palipoandikwa newa project kisha menu nyingine itafuata. Menu hiyo itakutaka kuchaguwa template ya app yako unayotaka kutengeneza. Sasa wewe chaguwa iliyoandika empty view activity.

 

  1. Baada ya kubofya hapo ukurasa mwingine utafuta. Sasa kuanzia hapo utatakiwa kuwa makini. Ukurasa huo una mambo makuu matano ambayo ni:-
  1. name : hapo utaweka jina la App yako. Ni vizuri jina lianze kwa herufi kubwa
  2. Package name: hapo utaweka jina la package. Hapo utaona kuna com.example.jinalaapp jna lako la app utaliona hapo baada ya kuandika. Sasa unaweza kubadili hiyo package name kuwa unavyotaka. Kwa mfano nikaweka com.bongoclass.mafunzo
  3. Save location hapo ni locatio ya app yako. Kwamba app yako itakaa wapi
  4. Language hapo utachaguwa lugha ya kikompyuta kwa ajili ya app yako. Sasa kwa mafunzo haya tutatumia java. Hivyo hapo wekka java.
  5. Minimum sdk hapo utachaguwa android api na android version. Yaani mfano kwa sasa tupo android toleo la 13 ambalo ni sawa na API level ya 33. Ina maana app yako ukisema minimum ni API 24 versio 7 hiyo app unayotengeneza haitaweeza kutumika kwenye simu za versio ya sita na kuja chini. Angalia video yetu imefafanua zaidi https://www.youtube.com/@tehama-tz

Baada ya hapouta bofya next na ukurasa mwingine utafunguka. Ila hapo kuwa na subira kama ndio mara yako ya kwanza, kwani inaweza kuchukuwa muda, pia bando litahitajika angalau usipungukiwe na MB 500. Kama mabo yote yatakuwa sawa ukurasa huu utafuata

 

Na hapo ndipo hasa somo letu linakwenda kuanzia. Sasa fanya hivi bofya hapo alipoandika app ili ukurasa huo uonekane hivi . Angalia video yetu kuna maelekezo zaidi nimeyatoa hapo. Pia unaweza ku download video hizi kwenye maktaba yetu.

 

SEHEMU KUU ZA ANDROID STUDIO:

Kama inavyoonekana hapo kuna sehemu kuu mbili ambazo kama ndio unaanza kutumia android studio unatakiwa uzijuwe, nazo ni hizo hapo juu app  na Gradle Scripts kisha sehemu hizo zimegawanyika zaidi.

 

APP:

Hii ndio sehemu ambayo utakwenda kuitumia sana kwa asilimia 80 ya kazi zako za kutengeneza app. Kama utabofya neno app ukurasa huo utaonekana hivi 

Hapo utaona sasa kuna sehemu tatu ambazo unatakiwa kuzujuwa ambazo  ni:-

  1. Manifest
  2. Java
  3. Res

 

1. Manifest:

Hilo ni faili ambalo litabeba structure ya app yako. Yaani ni faili ambalo linabeba mpangiliomzima wa hiyo app yako. Kwa wajenzi wa nyumba ni swa na kusema ramani nzima ya jengo ipo hapo. Shughuli zote zinazofanyika kwenye hiyo app lazima ziorodheshwe hapo na kama app itahitaji kutumia hard ware za simu kama spika, microphone, camera sensor na vinginevyo itahitaji kuomba ruhusa kwenye simu. Sasa hizo ruhusa huombwa hapo.

 

2.java

Hapo ndipo ambapo mafaili yote ya java yatakaa hapo. Mafaili ya java ndio yanayohusika kayika utendaji kazi wa app yako. Kama utabofya hapo utakuta tena kuna mafolda matatu. Sasa bofya hilo la kwanza  ukurasa utaonekana hivi.

Kuna faili moja la java linaloitwa MainActivity lipo hapo. Hilo ndio tutakwenda kuanza nalo.

3.res

Res ni kifupsho cha maneno resources. Hapo patawekwa mafaili ambayo yana resources. Mafaili hayo yanahusika na muonekano wa app. Na yenyewe yapo katika langaage ya xml hii ji moja ya markup mangauge kama ilivyo html na css. Ndani ya folder la res kuna mafolda kadhaa ambayo utayaona:

  1. Drawable hapo ndipo ambapo itaweza picha
  2. Layout hapo ndipo panapokaa mafaili ya layout
  3. Mipmap hapo ndipo ambapo icon zitakaa
  4. Value hapo kunakaa mafaili yanayohusu style za app yako. Hapo utakuna kuna 

  1. Colors hapo ndipo hukaa rangi zitakazotumika kwenye app
  2. String hapo ndipo hukaa text muhimu kwa ajili ya app kama jina la app
  3. Theme hapo hukaa style za app

 

Pia kwenye res utaweza kuweka mafolder mengineyo kama

  1. Row kwa ajili ya kuweka media files
  2. Asset kwa ajili ya kuweka asset file kama html code
  3. Menu kwa ajili ya kuweka menu

 

GRADLE SCRIPTS

Ukibofya folder hilo itaonekana hivi

Hayo ni mafaili ambayo yanahusika katika folder hilo. Katika mafaili hayo tutakwenda kufanyia kazi mafaili mawili ambayo ni

 

Hilo la buil,gradle (module app), hapo hookah configuration za app kama:

  1. Compile sdk: yaani version ya SDK ilyotumika kutengeneza app
  2. applicationId: hii ni ille package name
  3. minSdk: 
  4. targetSdk:
  5. versionCode: kila toleo la app lina code yake. Toleola kwanza litaanza na 1 na la pili ni 2 na kuendelea.
  6. versionName: hili ni jina la hilo toleo la app yako.

Utaona taarifa hizo ni katika zile ulizojaza mwanzoni kabisa. Angalia kwenye video una ufafanuzi zaidi.

 

Sehemu nyingine muhimu kwenye faili hilo ni dependance{} hii ni sehemu ambayo uta imort library na sdk mbalimbali. Kwa mfano unataka kutumia sdk ya facebook kuweka matangazo yo, basi hiyo dk utaiweka hapa.

 

Kwa ufupi hizo ndo sehemu kuu mabzo unapaswa kuzijuwa na matumizi yake. Sasa tukutane somo la tatu ambalo tutajifunza jinsi ya kubadili jina, package na icon.

 




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...