MAFUNZO YA ANDROID JAVA SOMO LA 3


picha


Katika somo hili utajifunza jisi ya kutest app yako kwa usb, wifi ama kwa android emulator. Pia utajifunza jisni ya kutengeneza APK.


Jinsi ya ku test app yako.

Katika somo hili nitakwenda kukufundisha jinsi ya u test app yako. Hili ni somo muhimu sana kwani linahitaji mazingatia hasa kwa wale ambao komputa zao ni ndogo kiuwezo. Utahitajika kui run app yako kwenye device mablimbali ili uweze kujuwa kama ina shida yeyote au laa.

 

Kuna njia 4 nitakufundisha ambazo utajitumia ku test app yako. Angalia video za course hii ya android java kwenye cjannel yetu ya youtube inayofahamika kwa jina la tehama. www.youtube.com/@tehama-tz utaweza kuangalia kwa vitendo njia hizi:

1. Kwa kutumia USB

Hapa utaweza ku unganisa simu yako kwenye android studio na ku test app yako. Chomeka waya wa usb kwenye simu yako na kwenye kompyuta. Kisha kwenye simu yako nenda kwenye setting kisha bofy my phone  kisha nenda kwenye Build number hapo bofya mara 3 iki ku activate menu ya developer.

 

Baada ya hapo rudi kwenye setting  kisha bofya kwenye  system hapo utakutana na meu ya developer options mwishoni kabisa kwa huo ukurasa. Bofya hapo kwenye developer options . mwanzoni kabisa hakikisha pako on kwenye hiyo batani ya kwanza bofya hapo iwe na rangi ya kijani kumaanisha ipo ON.

 

Shuka hini hadi palipoandikwa USB debuging hapo napo weka on hiyo batani iwe na rangi ya kijani.kisha shuka tena chini hadi palipoandikwa Verify apps over USB hapo weka on pawe na alama ya kijani.

 

Baada ya hapo chomeka USB kweye kompyuta yako. Hapo simu yako itaonekana kwa juu baada ya ile batani ya ku play 

 

2. Kwa kutumia wireless

Hii ji kwa wale ambao simu zao ni kuanzia android version ya 11 na kuendelea. Hakikisha simu yako na kompyuta zimeunganishwa kwenye connection moja ya wireless. Kwa mfano kama una rooter ama siu nyingine utawasha wireless kisha utaunganisha . 

 

Baada ya hapo kwenye simu yako ndenda kwenye developer options kama ulivyofanya hapo juu. Shuka chini hadi palipoandikwa wireless debuging happ washa pawe na rangi ya kijani. Baada ya kuwasha utarudi kwenye kompyuta yako hapo kwenye jina lasimu yako bofya kuna menu itakuja. Sasa shuka nayo mpaka kwenye palipoandikwa pair device using Wi-fi.

 Kama camera ya simu yako nzima basi bofya palipoandikwa pair with QR code. Hapo ukurasa wa ku scan utakuja. 

Rudi kwenye simu yako kisha scan hiyo picha. Kama kila kitu kipo sawa basi ita connect  na hapo jina la simu yako litaonekana kama inavyoonekana picha hapo chini

 

Sasa kwenye android studio pale juu karib na batani ya ku play jina la simu yako litaonekana.

 

Kama camera ya simu yako sio nzuri ama mbovu basi kwenye ku connect utachaguwa pair using pairing code


 

3. Kwa kutumia Android emaulator:

Kwenye android studio kwa juu bofya menu iliyoandikwa tools kisha shuka nayo hadi palipoandikwa device manager menu huyo pia utaipata kwa upande wa kulia kwa juu kuna ico imefanana na kijisimu. Ukibofya hapo ukurasa utafunguka. Bofya palipoandikwa create device

 

Hakikisha una bando lisilopunguwa gb 1 kwani itakubidi ku download components. Utachaguwa simu na kubofya next. Utachaguwa aina ya device unayotaka na itaanza ku download. Baada ya kumaliza utakwenda next. Kisha utabofya finish. Hapo device yako itatengenezwa. Utakuja kuiona kwenye list ya device manager. 

 

JINSI YA KUTENGENEZA APK:

 

1. Kwenye menu kwa juu bofya palipo andikwa build

Shuka nayo hiyo menu mpaka palipoandikwa  build bundle/APK  utaona itafunguka tena kulia kuna menu kama  build apk bofya hapo kisha kuwa na subira. Angalia kwa chini upande wa kulia utaona kumeandikwa gradle build run apk yako ikiwa tayari utaiona hapo. Utabofya palipoandikwa  locate kisha utakopy hiyo APK na utaifanya unachotaka wewe maana APK yako itakuwa umekamilika.

 

Apk yako utakuta imeandikwa app-debug, unaweza ku share na marafiki ama ku upload kwenye online emulator.


 

2. Kwa kutumia external emulator. Hapa sasa itakubidi u download emulator kama blue stack, koplayer, ldplayer ama nox player. Yeyote katika hizo. Baada ya ku insdtall utatenegeneza apk ya app yako kisha utaitaifunguwa na emulator yako. Angalia video jisi nilivyotumia ldplayer. Hizi emulator pia zinaweza kuu ganishwa moja kwa moja kwenye android studio.


 

3. Kwa kutumia online emulator. Hii ni njia nyingine nzuri kwa wale ambao kompyuta zao hazina uwezo mkubwa. Hii utatumia online emulator kwa mfano utatumia mtandao wa https://appetize.io/apps hapa utatengeneza account kisha uta upload apk ya app yako. Utaifunguwa kama vile unatumia simu. Kwa maelekezo zaidi angalia kwenye video.




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...