MAFUNZO YA ANDROID JAVA SOMO LA 4


picha


Katika somo hili utajifunza jinsi ya kubadili jina la app, icon ya app, package name ya app na root folder.


Katika somo hili uatjifunza jisni ya kubadilisha jina la app, icon ya app na app pachage name.

 

1. Kubadili jina la App:

Ili uweze kubadilisha jina la app ingia kwenye folder la res kisha values kisha sting hapo ndipo utaweza kubadilisha jina. Kwenye faili la string angalia kuna code zinasomeka

Sasa hapo kwenye Tehama badili weka ICT kisha run app . tunaposema run app yako tunamaanisha bofya batani inayofanana na plya ama bofya neno run kwenye menu kwa juu, kisha bofya run app. 

 

Ukisha run app yako jina la app yako litauwa limebadiika, na hata uki install utaona ina jina lingine .

 

2. Kubadili package name

Kwenye folder la java bofya folder la kwanza lenye jina la package name.

Hapo right click kuna menu itafunguka, hapo shuka nayo mpaka kwenye refactory kwa upande wa kulia kuna menu itafunguka hapo bofa rename.

 

Hapo ukurasa mwingine utafunguka. Utabofya all directory

Kisha menu nyingine itafunguka. Na hapo ndipo dipo utaweka jina lako jipya unalolitaka wewe la hiyo package name yako.

 Mapak ahapp package name itakuw aimebadilika. Sasa utakwenda kwenue folder la gradle scripts kisha utabofya palipoandika build.gradle (module app)

Kisha utabofya balipoandikwa  sync now  kwa juu

 

Mpaka kufikia hapo utakuwa umeshabadili package name.

 

3. Kubadili folder name

Hapo kwenye folder la gradle scripts shuka chini kuna faili limeandikwa settings.gradle (project setting) lifunguwe hilo.kuna ukurasa wa code utafunguka

Kwenye huo ukurasa nenda hadi chini ku apalipoandikwa rootProject.name utaona jina la project yako hapo. Libadilishe ukitaka.ukimaliza bofya kule juu palipoandikwa sync now. Na hapo utakuwa umemaliza kazi

 

4. Kubadili icon ya app

Ili uweze kubadili icon ya app juu kabisa kwenye app android studio upande wa kushoto angalia palipoandika app right click kuna menu itakuja. Hapo bofya palipoandikwa new ukurasa mwingine pembeni utafunguka hapo shuka chini mpka kwenye image asset bofya hapo

 

Hapo ndipo autaanza ku set icon zako. Sasa kuna aina tatu za aicon

  1. Image
  2. Clip art
  3. Text

Kama utahitaji kuweka ya picha utatiki hapo kwenye image kisha pembeni kidogo utabofya kwenye kijipicha cha folder. Hapo utarudishwa kwenye kompyuta yako ili uweze kuchaguwa picha unayotaka kuiweka uwa icon

Na kama utahitaji icon ya maandishi utaa=tik kwnye text kisha utaweza kuandika. Utaset na rangi za background na rangi za maandishi.

 

Kwenye option hapo unaweza kubadili umbo la icon yako kwa mfano kuwa ya duara, ama pembe 4.

 

Ukimaliza hapo bofya next  kisha bofya finish . mpaka kufika hapo utakuw aumebadili icon ya app yako. Sasa  run app yako ili kuona kama mabadiliko yako sawa. Kama kuna error rudia tena kubadili icon itakubali. Kwa maelezo zaidi angalia video yetu youtube.

 

Mwisho:

Tukutane somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu ukurasa wa layout




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...


MAFUNZO YA ANDROID JAV...