MAFUNZO YA HTML LEVEL 1 SOMO LA 1


picha


Hili ni somo la kwanza katika mlolongo wa mafunzo ya HTML level 1 kwa wanaoanza kujifunza.


HTML SOMO LA KWANZA

HTML ni ufupisho wa maneno yanayosomeka kama:-

Hypertext

Markup

Language

 

 

Ni lugha ya komputa inayotumika katika kutengenezea kurasa za tovuti (website) ama blog.Inaungana na lugha nyingine katika kuboresha kurrasa za tovuti ama blog na kuzifanya ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa vyema. Unaweza kutumia HTML tu ukatengeneza website yako bila ya lugha nyingine. Hata hivyo muonekano wake hautakuwa vyema sana kama hutatumia nyinggine.

 

Je na wewe una ndoto za kuwa na blog ama website uliyoitengeneza wewe mwenyewe. Mafunzo haya ni kwa ajili yako. Katika mafunzo haya utajifunza namna ya kutengeneza website yako kupitia kiganja chako yaani simu yako ya mkononi. Kama utakuwa na kompyuta hatutakuacha pia.

 

Somo hili la kwanza utajifunza namna ya kuandaa simu yako kwa ajili ya kutengeneza website, ama kwa ajili ya kutumia HTML. Kama tutaenda vyema na mafunzo haya hadi mwisho nakuhakikishia kama Mwenyezi Mungu akitujaalia nguvu, uwezo na uhai, utaweza kutengeneza website yako na kuiweka live.

 

Muda wa masomo haya kwa hatuwa za Awali (Basics) itakuwa na wiki moja. Kisha baada ya hapo hatuwa ya pili ya mafunzo itaendelea. Tafadhali kuwa tayari kujifunza, kuwa muulizaji na mchangiaji:

 

 

VIGEZO VYA KUJIFUNZA:

1.Kuwa na simu ya smartphone

2.Uwe unajuwa kusoma na kuandika

3.Kuwa tayari kujifunza

4.Kuwa mjanja

5.Uwe mwenye kufanyi akazi (fanya mazoezi)

 

 

NAMNA YA KUANDAA SIMU YAKO:

1.Download App inayoitwa TrebEdit. Tumia link hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.teejay.trebedit

2.Funguwa App yako kisha bofya Menu

3.Bofya palipoandikwa Workplace

4.Bofya kitufe chenye alama ya kujumlisha chini

5.Kisha bofya palipandikwa New Project

6.Andika jina la Project (mimi natumia HTML) kisha bofya save.

7.Ingia kwenye project uliotengeneza kwa kubofya jina lake, ukurasa mpya utafunguka

8.Bofya tena kitufe cha alama ya kujumlisha
9.Bofya palipoandikwa new folder (hapa tunatengeneza folda la kuweka picha tutakazokuja kuzitumia kwenye tovutu tutakayotengeneza)

10.Andika jina la folda tumia image kisha bofya save.

11.Baada ya hapo rudi nyuma hatuwa moja kwenye project yako.

12.Bofya tena jina la project yako

13.Bofya kitufe cha alama ya kujumlisha

14.Bofya palipandika New file (hapa ndipo tutakapoanzia kuweka code za kutengeneza tovuti yetu)

15.Utatkiwa kuandika jina la file hapo andika index.html (hili ndio faili letu la kwanza la tovuti yetu.

16.Bofya faili hilo ulilolitengeneza, utaona limeandika index.html

17.Baada ya kufunguka kuna maneno chini yameandika html snippet, bofya hayo maneno

18.Ukursa wako sasa utaona una code HONGERA SANA KWA KUFIKA HATUWA HII

19.Juu ya ukurasa kuna kibatani cha kusave, kimefanana na kile cha kwenye microsoft office. Bofya hicho kibatani, hapo utakuwa umesave code zilizopo hapo.

20.Kuna kibatani kingni cha kuplay kimefana na kile tunachotumia kwenye media player. Bofya hicho kupreview code zako.

21.Utaona ukurasa mtupu. Vyema sasa fanya hivi rudi nyuma kisha:-

22.Tafuta haya maneno <title>Page title</title> kisha yabadilishe yasomeka <title>Home Page</title>

23.Chini ya maneno haya <body> weka maneno haya

<h1>Mafunzo ya HTML</h1>

<h2><u>Jifunze bure</u></h2>

<p>Haya ni mafunzo ya HTML kwa kutumia simu</p>

<br><br><br>

<i>From <br>Bongoclass</i>

24.Save

25.Bofya kitufe cha kupyay ili kuangalia kilichotokea baada ya kuweka hizo code

26. Hongera sana ukurasa wako wa HTML umekamilika. Unaweza kubadili maneno kwenye hizo code hapo juu kweka yako.



Somo la pili tutaanza kujifunza hizo code ulizoziweka kazi yake na vipi zinafanya kazi. Kama umefanikiwa hatuwa zote hizo tupe maoni yako, ama tutumie screenshot yako.

 




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...