Mafunzo ya HTML level 1 somo la 4 (HTML basic level FOR BEGINNERS)


picha


Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.


HTML SOMO LA NNE
Karibu tena lwenye mafunzo haya ya HTML lugha ya kompyuta inayotumika katika kutengenezea website, blog na web application. Html hutumika na mchanganyiko wa lugha nyingine za kompyuta kutengeneza software na system. Hata hivyo unaweza kutumia html peke yake kutengeneza website (tovuti) na ikawa live watu wakaweza kuitembelea.

 

Je na kama na wewe ni mmoja kati ya wenye ndoto za kuweza kufanya haya, karibu tena kwenye somo hili. Katika somo la kwanza hadi la tatu tuliona namna ambavyo HTML inavyofanya kazi, pia tuliona mpangilio wa faili lake na tukaona tag na element. Katika somo la tatu tulijifunza code 25 muhimu zinazotumuka katika uandidhi. Unaweza kupata somo la kwanza la pili na tatu kwenye linki hizo hapo chini:-

 

 

 

Katika somo hili la nne tutaona jinsi ambavyo tag 25 tulizozitaja kwenye somo la tatu zinavyoweza ktumika na kuandikia makala katika ukurasa wa mtandao. Kama utakuwa unatumia kompyuta funguwa note pad kisha fatilia somo hili, tumia notepad kuandikia code kama somo litakavyoonyesha. Kwa wale wanaotumia simu kama mimi, utaratibu umetangulia katika somo la kwanza, unatakiwa utumie App inayojulikana kama TrebEdit ipo playstore, linki utaipata kwenye somo la kwanza.

 

FILE EXTENTION KATIKA FAILI LA HTML
Tunapozungumzia file extension huwenda likaonekana kama neno gumu, ila kwa ufupi nitolee mifano. Unapotaka kusevu faili katika microsoft office unaweza kusave as document (.doc), extensive document (.docx) portable document file (.pdf). pia katika media kuna (.mp3, .mp4) kwenye web site kuna (.com, .net, .io, .co, .ac). hivyo extension ndio ambayo huiambia kompyuta aina ya faili. Sasa unapoandika faili lako la code za HTML, wakati wa ku save lazima uweke (.html) mfano katika somo la kwanza tulitumia faili tuliloliita “index.html” usisahau kuweka doti.

 

Sasa funguwa App yako ya Treb editi kisha menu, kisha workplace, kisha click project yako kama tulivyofanya kwenye somo la kwanza na pili. Kisha new file, weka jina mfano “tag.html” kisha save. Click hilo faili, kisha bofya HTML snippet chini, hapo ukurasa mpya wa code utatokea. Kwa watumiaji wa kompyuta kweka code hizi kwenye notepad yako:

 


<!DOCTYPE html>
<html lang="en">
<head>
<meta charset="utf-8">
<title>Tag Muhimu</title>
</head>
<body>

</body>
</html>
 

Kisa saveas all files kija weka tag.html

 

Sasa hadi kufikia hapa tupo tayari kuanza somo. Somo
Katika tag zote 25 tulizoziona katika somo la tatu, baadhi yake tutakuja kuziona tena kwenye masomo yajayo kutokana yanahitaji ufafanuzi zaidi. Kwa mgano tag hii <img na <a> hizi tutakuja kuziona zaidi katika somo lijalo. Sasa kama ulishafunguwa TrebEdit yako ama notepad, sasa kopi code hizo hapo chini kisha paste kwenye faili lako ulilolisave kwa jina la tag.html. Kisha previes, kwa kubofya kitufe cha kuplay au click file kwenye komputer litafunguka kama website.

 

Code zenyewe ni hizi:-

 

 

 

<!DOCTYPE html>
<html lang="en">
<head>
<meta charset="utf-8">
<title>Tag Muhimu</title>
</head>
<body>
<h1>Heading 1</h1>
<h2>heading 2</h2>
<h3>heading 3</h3>
<h4>heading 4</h4>
<h5>heading 5</h5>
<h6>heading6</h6>
<p>hii ni paragraph</p>
<b>bold</b>
<u>underlined</u>
<hr> msitari<hr>
<i>italic</i> <br>
6<sup>2</sup><br>
H<sub>2</sub>O <br>
<code>code type</code> <br>
<tt>type writer</tt> <br>
<small>small text</small><br>
<em>emphasizing</em> <br>
<strong>strong text</strong> <br>
<mark>marked text</mark> <br>
<s>striked text</s> <br>
<q>quoted text</q> <br>
line<br>break<br>break<br>
wacha&nbsp;nafasi&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp;nafasi <br>
<a href="https://bongoclass.com">link</a><br>
<button>Tabani</button><br>
<pre>
maandishi yatakuwa kama unavyoyaonahapa kwenye cde
mfano:
kama unapoandika mashairi
unataka iwe
kama ilivyo
bila kuharibu mpangilio
wa
vina
</pre> <br>
<form>
<label>Jina kamili</label>
<input type="text" placeholder="enter your name">
</form> <br>
<img src="" alt="picture"> <br>
<div>this is block text</div>
<span>this is inline block text</span>
</body>
</html>
 



 

 

Katika posti ijayo tutakuja kuona namna ya kuweka staili kwenye faili la html, kama kuweka rangi, kupangilia text, kuweka link na kupangilia muonekano wa text. Endelea kufanyia mazoezi tag hizo hapo juu, ili iwe rahisi kuendelea na somo lijalo. Usisite kuuliza swali ambapo hapaposawa.

 


Mafunzo haya yamekujia kwa hisani ya:
Bongoclass.com
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...