Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 5 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 5)


picha


Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi


ATTRIBUTES NA NAMNA AMBAVYO ZINAFANYA KAZI:
Kama tulivyoona katika somo lililopita tulijifunzakuwa Attributes zina kazi ya kuongeza taarifa nyinginezo kwenye tag. Katika somo hili tutakwenda kujifunza zaidi kluhusu attributes, sifa zake, kanuni zake na zinavyofanya kazi. Kwa ufupi attributes zinawza:-

 

1.Kuwa katika element yoyote ya HTML
2.ATTRIBUE HUPATIKANA KWENYE TAG YA KUANZIA NA SI YA KUFUNGIA
3.HUONGEZA TAARIFA ZA ZIADA KWENYE ELEMENT
4.Attributes zinakuwa katika kanuni hii jina=”” naani unaanza kutaja jina la attribute kisha unaweka alama ya sawasawa kisha thamani ya attribute inawekwa ndani ya alama za funga semi.

 

MIFANO YA ATTRIBUTES
1.Attribute wakati wa kuweka link. Hii hukaa kwenye tag ya <a> pale unapotaka kuweka link ya ukurasa mwingine wa wavuti.

 

Kwanza utaweka tag ya <a kisha itafatiwa na jina la attribute href (hhypertext referrence) kisha itafatiwa na alama ya = na thamani ya attribute itawekwa kwenye alama za “”. 
Mfano
<a href=”www.bongoclass.com”>weka jina la link hapa</a> katika mfano huu <a ndio tag na href ni jina la attribute na “www.bongoclass.com” ndio thamani ya attribute.

 

2.ATTRIBUTE ZINAZOTUMIKA KUWEKA PICHA
Attribute hizi hukaa kwenye tag ya <img lengo la attribute hii ni kuweka chanzo cha picha na jina la picha. Chanzo cha picha huwekwa kwa src=” ” na jina la picha huwekwa kwa alt=” ”

 

Mfano:
<img src=”bongo.png” alt=”picha”> katika mfano huu <img ndio tag na src ndio jina la attribute na “bongo.png” ndio thamani ya attribute. Pia katika mfano huu una attribute mbili. Attribute nyingine jina lake ni alt na thamani yake ni “picha”. attribute hii hutumika kuonyesha jina la picha hiyo. Endapo picha haita onekana kwa mfano mtandao ukawa low basi jina ndio huonekana.

 

3.Attribute zinazotumika kuonyesha ukubwa kama urefu na upana. Attribute hii ni height kuonyesha urefuwa kimo na width kuonyesha upana wa kitu. 

 

Mfano
<img  src=”picha.png” width=”100%” alt=”picha”> katika mfano huu attribute nyingine hapo ni width kuonyesha upana wa picha na thamani yake ni 100%.

 

4.Attribute ya kuweka style
Atribute hii hutumika katika shughuli nyingi. Kwa mfano ukitaka kuweka rangi kwenye maandishi, ama kubadili muelekeo, na mpangilio wa herufi atribute hii hutumika. Kwa mfano:-

 

<p  style=”color:yellow”>maandishi haya yatakuwa na rangi ya njano</p> katika mfano huu attribute ni style na thamani yake ni color:red yaani rangi nyekundu.

 

5.Attribute ya title yaani ya kuwekea kicha cha habari cha faili. Mfano   <h1 title=”HTML”> SOMO LA HTML</title> katika mfano huu tumeweka jina kwenye tag ya <h1> hivyo attribute ni title na thamani yake ni “HTML”. 

Attribute nyingine kama ile ya lang tuliotumia kuweka lugha inayotumika katika faili la html.pia atribute za metadata  na nyinginezo tutaziona katika masomo yajayo.  Katika kutumia attribute unashauriwa kutumia herufi ndogo na funga na funguwa semi mbilimbili yaani “ kama ilivyo kwenye mifano hapo juu.

Hivyo katika mifano hiyo tumetumia attributes zifuatazo:-
1.href
2.src
3.width
4.alt
5.style
6.Title

Tukutane somo lijalo tutakapokuja kujuwa zaidi jinsi ya kuweka stayle mbalimbali katika uandishi katika html. Somo hili litaanza kutumia tag na attributes kwa pamoja katika ufanisi wa kufanikisha uandishi.




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...