MAFUNZO YA HTML LEVEL 2 SOMO LA 9 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 9)


picha


Katika somo hili utajifunza taratibu za kufuata unapotaka kutengeneza website ama blog.


HATUWA ZA KUTENGENEZA WEBSITE AMA BLOG
Unapotaka kutengeneza website ama blog kuna mambo mengi unatakiwa uyawaze hata kabla ya kuanza. Blog ama website ni kitambulisho cha biashara ama kampuni ama taasisi husika. Ni kitambulisho ambacho kitawafikia watu dunia nzima, watu wa jinsia zote kwa malengo tofauti tofauti. Hivyo basi unatakiwa ufikiri kwa makini.


Haya ni mawazo unatakiwa ujiulize kabla ya kudizaidi tovuti yako:
1.Itahusu nini
2.Kina nani watakuwa wateja wako
3.Ni aina gani tovuti yako
4.Kwa nini watu watembelee tovuti yako na si nyinginezo
5.Nini wanufaika kwako ambacho kwa wengine hawatakipata.
6.Kwa nini unahitaji tovuti
7.Je ni gharama kiasi gani itahitajika


baada ya kuyapata majibu ya maswali hayo unatakiwa uwaze kabisa jinsi watu watakavyokupata kwenye hito tovuti yako. Tambuwa kuwa kuna zaidi ya tovuti bilioni tatau. Na karibia tovuti milioni 400 zipo active. Hivyo unatakiwa ufikiri vyema vipi watu watakupata. 

1.Tafuta jina la tofuti yako liendane na malengo yako
2.Jina liwe fupi na lennye maana
3.Jinaliwe lenye kukaririka vyema
4.Lisiwe lipo wazi
5.Jina liwe la kipekee
6.Lugha yako iendane na watu uliowatageti

Baada ya kuwaza namna ambavyo watu watakavyokupata sasa ni wakati wa wewe kuanza kunihusisha moja kwa moja katika utengenezaji. Haijalishi uwe unatengenezewa ama unatengeneza wewe mwenyewe, kuna mambo unatakiwa uyafanye:-
1.Gharama kiasi gani nitatumia
2.Muda gani utahitajika
3.Chanzo cha maudhui ya tovuti yako.
4.Je web yako itakuwa static ama dynamic
5.Nani anatengeneza ni wewe ama unatengenezewa.


Kuna aina kuu mbili za tovutii ambzo ni static ana dynamic. Static ni ile ambayo inatumia html, css na javascript. Yaani static inakuwa haibadiliki. Dynamic ni zile ambazo taarifa zake hubadilika badilika. Yaani admin anaweza kuedit makala hata kamakuna mtu anaisoma. Dynamic ni kama ambazo zimetengenezwa na php na database. Blog zote zinaingia kwenye kundi hili.

Kwa ufupi ststic ni tovuti ambazo zenyewe taarifa zake hazina mabadilikobadiliko. Na inachukuwa muda mrefu kubadili taarifa moja, mpaka uingie kwenye system nzima.ststic website zenyewe zinahitaji html na css . Lakini dynamic zenyewe muda wowote unaweza kuongeza taarifa na kutoa ama kuediti ama kukoment. 


Hatua inayofata ni kuingia kazini sasa kuitengeneza tovuti yako. Hapa ndipo panahitaji umakini, kwani ukiharibu kwenye muonekano unaweza kukosa watu. Kumbuka uzuri we muonekano wa tovuti kwenye kompyuta sio sawa na kwenye simu. Katika hatuwa hii fanya haya:-
1.Chora mchoro wa kuonyesha tovuti yako itakavyofanya kazi
2.Chaguwa text editor kulingana na level ya ujuzi wako unaweza piakutumia WYSIWYG
3.CODE tovvuti yako kwakufuata mchoro wako
4.Zingatia mabadiliko ya screen, kuna wengine watatembelea tovuti yako kwa kompyuta na wengine simu, hivyo uzingatie na ubora
5.Fanya iwe simple, usitumie sana rangi


Baada ya kuikamilisha website yako utahitaji kuihost. Kuihost ni kuifanya ipatikane kwenye internet. Cheki somo la nane katika course iliyopita tumetoa maelekezo ya video jinsi a kuhost kwa free. Kuna mitandao mingi inatoa huduma ya kuhost code zako free. Hapa ntakuorodheshea tovuti chake
1.Google cloud
2.Google firebase
3.00webhosting
4.Infinityfree
5.Digitalocean


Zipo kampuni nyingine nyingi tuu zitakupa huduma hii ure. Nimetaja hizo chache kwa sababu nina uzoefu nazo. Kama utakuwa na code za php nakusauri tumia 00webhosting ama infinityfree. Ila kama ni html css na javascript google firebase ni nzuri japo ni ngumu kuielewa mwanzo, hivyo vyema kutumia hizo mbili nilizozitaja hapo juu.




Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS


Post Nyingine


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...


MAFUNZO YA HTML LEVEL ...