MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3



Katika somo hili utajifunza jinsi yakutengeneza database kwa kutumia PHP.


Katika somo la pili tiliona namna ya kuunganisha databe na PHP.  Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutengeneza database kwa kutumia php. Somo hili linategemea sana somo lililotangulia. hapa tutakwenda kutengeneza database ambayo tutaiita mafunzo. unaweza pia kutengeneza kulingana na unavyotaka wewe.



Ili uweze kutengeneza database kwa kutumia PHP kwana unatakiwa ujuwe jinsi ya ku open connection kwenye server na kisha kuunganisha connection hiyo na PHP kama tulivyojifunza somo lililotangaulia. baada ya kukonnect server sasa tutakwenda kutengeneza database.



kama ulishiriki vyema somo lililopita utakuwa umeelewa nama ya kuuganisha php na server.

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

 

// kufanya connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password);

 

// kuangalia connection

if (!$conn) {

   die("You are not connected: " . mysqli_connect_error());

}

echo "You are connected";

?>

 

Kama umeshafika hapo kuna kazi ya ziada unatakiwa uifanya. Kwanza ni kuandaa variable kwa ajili ya kutengeneza database. Pia unatakiwa ujuwe SQL command ya kutengeneza database. rejea mafunzo ya database. Kama mambo yapo kama hivyo wacha nikujuze tena kuwa tunatengeneza database kwenye MySQL kwa kutumia SQL kwa “CREATE DATABASE

” kisha utahiyajika kutaja jina la database unalotaka kutengeneza. Mfano tunataka kutengeneza database inayoitwa mafunzo. hivyo tutasema CREATE DATABASE mafunzo

 

Baada ya hapo unatakiwa utengeneze sasa PHP variable kwa ajili ya kuwakilisha CREATE DATABASE mafunzo Kwa mara nyingi variable inayotumika ni $sql ila unaweza tumia yeyote ile unayotaka mfan ukasema $chai. Kama tayari unaelewa jinsi ya kuandaa variable hapa hutapata shida. hivyo variable yetu itasomeka:-

$sql = "CREATE DATABASE mafunzo"; 



Baada ya hapo kinachofuata ni kuweka meseji kwa ajili ya kutujuza kama database imeshatengenezwa ama laa. kufanya hivi tutatumia if else statement kufanya hivyo.  Hivyo tutaangalia variable zetu ambazo ni $conn kwa ajili ya ku connect databse na $sql kwa ajili ya kutengeneza database. hapa tunachoangalia ni je hizi variable zimefanya kazi. hivyo ytahitaji function ya kuangalia variable hizo. function yeyewe ni hii mysqli_query($conn, $sql) hiyo mysqli_query ndio function yenyewe ya kuangalia variable hizo.



Hivyo kama tumekwenda vizuri php code za kutengeneza database zitakuwa hivi:-

<?php

 

//kuandaa variable

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

 

// kufanya connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password);

 

// kuangalia connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " . mysqli_connect_error());

}

 

// kutengeneza database

$sql = "CREATE DATABASE mafunzo";

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Database created successfully";

} else {

   echo "Error creating database: " . mysqli_error($conn);

}

 

//kufunga connection

mysqli_close($conn);

?>

 

Ukimaliza hapo pesti hizo code kwenye ukurasa wako wa php, kisha ufunguwe na browaer yako, hakikisha faili lipo kwenye localhost. kama utafanya hivyo utakuwa umeshatengeneza database yako. rudi kwenye phpmyadmin uone database yako.

 

Mwisho

Tukutane somo linalofuata utajifunza jinsi kutengeneza table na kufuta database na table kwa kutumia php.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT