MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1



Haya ni mafunzo ya PHP na huu ni utangulizi wa somo. Hapa nitakujuza mabo kadhaa yanayopasa uyajuwe kabla ya kuanza somo linalofata.


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 (PHP, SQL(DATABASE) & HTML)

  1. 1 UTANGULIZI

Karibu tena katika mafunzo ya PHP na hii ni level 2. Katika level 1 tulijifunza mambo mengi kuhusu basic za PHP na pia tulweza kufanya baadhi ya project kama 4 kwa kutumia HTML na php. Naamini katika level hii utajifunza mambo mengi zaidi.

 

Katika level hii tutakwenda kujikita kwenye php na database tu. hatutaangalia mabo mengine meengi. Katika php level 3 tutajifunza zaidi kuhusu PHP na tutaona baadhi ya concept nyingi ambazo mpaka sasa hatujazigusa. Hivyo katika level hii utajifunza kuchanganya PHP, HTML na database.

 

  1. 2 YALIYOMO:

KATIKA LEVEL HII UTAJIFUNZA:

  1. Namna ya kuunganisha DATABASE SERVER NA PHP 

  2. NAMNA YA KUTENGENEZA DATABASE KWA KUTUMIA PHP

  3. NAMNA YA KUTENGENEZA TABLE KWA KUTUMIA PHP

  4. NAMNA YA KUFUTA DATABASE NA TABLE KWA KUTUMIA PHP

  5. NAMNA YA KUWEKA TAAFIFA KWENYE DATABASE KWA KUTUMIA PHP

  6. NAMNA YA KUEDIT NA KU UPDATE TAARIFA KWENYE DATABASE

  7. NAMNA YA KUFUTA TAARIFA KWENYE DATABASE

  8. KUPANGILIA MUONEKANO WA TAARIFA KWENYE DATABASE KWA KUTUMIA PHP

  9. KUSEARCH DATA KWENYE DATABASE KWA KUTUMIA PHP

  10. KUZIFANYIA MAHESABU TAARIFA ZA KWENYE DATABASE  KWA KUTUMIA PHP

  11. KUTUMIA CONDITION STATEMENT (if, else, ifelse) KWENYE DATABASE KWA KUTUMIA PHP

  12. JINSI YA KUTUMIA HTML FORM NA DATABASE

  13. KU UPLOAD FAILI KWENYE DATABSE KWA KUTUMIA PHP

  14. PROJECT YA CHAT APP (APP YA KUCHATI) KWA KUTUMIA PHP NA HTML

  15. KUHOST PHP PROJECT

 

Baada ya hapo tutakuwa tumefunga somo la PHP level 2. matarajio yetu ni kuwa kumaliza level zote tatu ili kuanza kutengeneza full website na blog yetu wenyewe bila ya kuhitaji msaada. Baada ya kumaliza level 3 za PHP mafunzo ya kutengeneza Android App yataanza rasmi.

 

  1. 3. SIFA ZA MSHIRIKI WA MAFUNZO HAYA YA LEVEL 3

  2. Awe na ufahamu kuhusu misingi ya php na database, ama awe ameshajifunza kupitia mafunzo yetu php leve1 na database

  3. awe na kompyuta ama simu ya smart phone. utaratibu mzima wa kuandaa simu ama kompyuta yako umeshatoka katika mafunzo yaliyotangulia.

  4. awe anajuwa kusoma na kuandika, angalau aujuwe kusoma maneno marahisi ya kiingereza akama select, update, order, where, by na mengineyo tutakayoyaona.

  5. awe mjanja na pupa ya kutaka kujifunza.

 

  1. 4 MUDA WA MAFUNZO.

kama orodha inavyojionuesha hapo kuna masomo 15, na kila somo ni siku moja. maratajio mafunzo yatakuwa ni wiki 2 ila endapo kutatokea uhitaji zaidi yanaweza yasimalize wiki hizo 2.

 

  1. 5 GHARAMA ZA KUJIFUNZA

Masomo haya yanatolewa bure, gharama yako ni bando la kifaa chako. hakika tunatowa mafunzo haya bure, hutahitaji kulipia gharama yeyote ile. tutafanya hivi kwa masomo mengine yanayofuata baada ya haya. kama utaona haja ya kutuunga mkono kwa kiasi kidogo cha kununua kikombe cha kahawa itakuwa vyema pia.

 

  1. 6 SEHEMU YA KUJIFUNZIA:

Masomo yetu ni ya ONLINE. na sehemu ambayo tutajifunza ni hapa tu, hatuna grupu la wasap, wala telegram, na itakuwa hivyo hatutakuwa na marupu mengine zaidi ya hili. hivyo usiwe na shaka kama unatumia free fb kuwa huru na hapa.

 

hata hivyo mafunzo haya pia unaweza kuyapata kwenye tovuti yetu bongoclass.com. hivyo wakati mwingine ninaweza kuweka link ya mafunzo, kabla ya kuweka post yenyewe. ni kwa sababu mafunzo haya kabla ya kuletwa fb yanawekwa kwenye tovuti yetu kisha ndipo yahamie fb. kuna sababu za msingi za SEO kufanya hivi.

 

 

MWISHO.

Nikutakie ujifunzaji mwema, na endelea kuwa nasi katika mafunzo mengineyo. tembelea kama utakuwa na maoni na mapendekezo yeyote usisite kuungaa nami kwenye comment na mawasiliano ya wasap.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]

WhatsApp: 0774069753

 

 



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT