MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10



Somo hili la 10 litakwenda kukufundisha jinsi ya kutafuta taarifa kwenye database. hapa tutatumia table yetu ya menu. Kwa mfano kwwenye menu kuna zaidi ya item 200 unataka kutafuta ugali. Baada ya kukodoa macho mpaka 200 unaweza kutafuta tu. kufanya hivi tunatumia LIKE pia alama ya % itakuwa ikitumika.


Kuandaa sql kwa ajili ya ku serarch

kwanza utatakiwa kuselect SELECT ikifuatiwa na column ya hiyo iten unayotaka kuisearch kulingana na mfano wetu ni name ikifuatiwa na FROM kisha jina la table kisha WHERE ksiah jina la column ambapo item uayoserarch ipo kisha LIKE kisha hicho unacho kitafuta kama ni ugali ila hakikisha unakiweka ndani ya ‘’ kama string.  mfano SELECT Name FROM menu where name LIKE ‘wali%’

 

Sasa hapa kuna japo alama ya % ikiwa mbele ya hiyo inayosearch (wali%) maana yake unatafuta neno linalomaliziwa na hicho unachoserarch. na ikiwa alama ya % utakaa mwano (%ugali) maana yake unatafuta neno litakaloanziwa na hicho unacho search. na ikiwa alama ya % itakaa mbele na nyuma  (%wali%)  ya hilo neno unalo search maana yake unatafuta neolo alililoanziwa ama kuishiwa na hicho unachosearch. 

Kwa maelezo hayo basi variable ya kusearch ugali inaweza kuwa hivi

 $sql = mysqli_query($conn, "SELECT name FROM `menu` where name LIKE '%wali'");

 

Kiachofuat ni kuandaa table ya HTML kwa ajili ya kupangilia muonekano. Pia andaa variable zako kwa ajili ya ku connect. kama kila kitu kipo sawa code zake zinaweza kuwa kama hivi

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

?>

<style>

   table, th, td {

       border: 1px solid black;

   }

</style>

<table style="width:100%">

   <tr>

 

       <th>Name</th>

 

   </tr>

 

<?php

$sql = mysqli_query($conn, "SELECT name FROM `menu` where name LIKE '%wali'");

       while($fetch = mysqli_fetch_array($sql)){

       ?>

   <tr>

 

       <td><?php echo $fetch['name']; ?></td>

 

   </tr>

<?php }?>

</table>

 

Hii itakupa matokeo haya

 

Pia kufatuta kwa mtindo wa alphabeti kwa mfano ukasema nataka kuona majina yote yalioanziwa na heruzi u,  hapa itakuwa hivi (%u) ama majina yte yalioishiwa na herufi u (u%) ama majina yalioanziwa na u na kuishiwa na i (u%i)

 

Tutajifunza zaidi kuhusu mada hii kwenye muendelezo wa course ya database. Kwa sasa hapo unachotakiwa ni kufanya mazoezi kwa wingi ili iwe rahisi kuelewa masomo yanayofata..

 

Tukutane somo la 11 tutajifunza jinsi ya kuzifanyia mahesabu taarifa zilizomo kwenye database.

 

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT