MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13



Katika somo hili utajifunza jinsi ya ku upload faili lolote kwenye database. Katika mafunzo ya database tulijifunza kuwa media fail zote zinakuwa katika BLOB.


Katika somo hili utajifunza jinsi ya ku upload faili lolote kwenye database. Katika mafunzo ya database tulijifunza kuwa media fail zote zinakuwa katika BLOB. Hivyo itabidi tuongeze column nyingine kwenye table yetu. column hiyo tutaiita file. Ingia kwenye databse yako hotel kisha ingia kwenye uwanja wa SQL kisha pest code hizi ALTER TABLE `menu` ADD `file` BLOB NOT NULL AFTER `price`;     Kufanya hivyo utakuwa umeongeza column mpya inayoitwa file.

 

Kuna namna mbili tunawea kuzitumia ili ku upload file kupitia ukurasa wa wavuti. Njiaya kwanza ni kutumia blob ambapo fili lenyewe linakwenda kukaa kwenye database. Njia hii sio nzuri kama database yako ni ndogo, kwani itaweza kujaa kwa haraka. Kwa kupitia niia hii file litakaa kmoja kwa moja kwenye database. 

 

Njia ya piili ni ku upload taarifa za faili tu ila faili lenyewe linabakia kwenye mafolder ya website tyako. Kwa kutumia njia hii storage pekee ndio hutumika ila database itabakia kuwa na taarifa kuhusu hilo faili kama jina, path, aina, ukubwa wake, limewekwa limni n.k. Hivyo ukitaka kuliona file hilo lazima uangalie taarifa kwenye database. lakini pia utaweza kulikuda kwenye ma folder ya website yake.

 

katika somo hili tutatumia nia ya kwanza. Nia ya pili tutaijuwa katika muendelezo wa course hizi. Ili ku upload file kwa kutumia njia ya kwanza yaani kwenye blob, ingia kwenye table ya menu. Kisha chaguwa menu unayotaka kuiwekea picha, kisha bofya edit kisha sehemu ya file utaona pana Choose File

Ukibofya hapo utapelekwa kwenye storage ya kifaa chako ili kuchaguwa file. Baada ya kucaguwa file bofya Go. hakikisha faile lako hallizidi KB 64. Baada ya hapo utakuwa umesha upload file lako. File hilo litakuwa katika mfumo wa herufi na nmanamba, hivyo ili tuweze kulisoma tutatitajika ku encode kutoka maherufi na namba kuwa image.

 

Katika table yetu tulioitengeneza katika somo lililopita sasa tutaongeza <td> ya kuonyesha picha. Hivyo katika <th>ongeza moja ya picha kisha katika <td> utaongeza moja ya picha. Katika mafunzo ya html tumejifunza namna ya kuweka picha kwenye ukurasa wa wavuti ni kwa kutumia tag aya <img> Hivyo tutahitajika kutumia tag hii ili ku load picha. 

 

Kitu cha kukumbuka ni kuwa lazima ujuwe path ya hiyo pic utaipata wapi path inaingia kwenye src=””> Kwa kuwa path ya file la kwenye blob ipo katika mfumo wa string utahitajika kutumia character set, standard tutatumia UTF-8 pia tutatumia base 64. (Tutajifunza mbeleni kuhusu hizi base) src="data:charset=utf8;base64 pia  Tutahitajika kufanya encoding ili kubadili hizi string zilizopo kwenye base 64. Kufanya hivi tutatumia function ya ku encode base64_encode ndani yake  ndipo tutakwena kufetch file path. Kwa pamoja tag ya image itakuwa hivi  <img src="data:charset=utf8;base64,<?php echo base64_encode($fetch['file']); ?>">

 

Sasa tutakwenda kuweka image kwenye <td> Ili kuweza kuiload pamoja na data nyingine. Hakikisha kila menu umeshaiwekea image yake. Mi nimetumia image moja ambayo nimeiandika no image ili kupunguza muda wa ku upload ma image meengi.

 

Mpaka kufikia hapo utakuwa umejifunza jinsiya ku upload file kwenye database. Tutajifunza zaidi kwa kutumia php katika muendelezo wa course hii. Tukutane somo linalofuata ambapo utajifunza namna ya kutumia HTML form kwenye php kwa ajili ya kukusanya madodoso.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT