MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14



Katika somo hili ninakwenda kukufundisha jinsi ya kukusanya madodoso kwa kutumia html form na PHP.


Katika somo hili ninakwenda kukufundisha jinsi ya kukusanya madodoso kwa kutumia html form na PHP. Katika somo hili utakwenda kuongeza data kwenye menu yetu kwa kutumia html form. Kufanya hivi tutatengeneza file la php lenye sehemu kuu 2. Moja ni kwa ajili ya kukusanya taarifa, na nyingine ni kwa ajili ya ku process taarifa na kuziweka kwenye database.

 

Sehemu ya kwanza (HTML FORM)\

Kumbuka kuwa tumejifunza kwenye mafunzo ya php level 1 kuwa html form ina sehemu mbalimbali ambazo ni method, action, submit na sehemu ya kuweka data. Method nazo zipo mbili kuna POST na GET. Hizi ni njia ambazo taarifa zako hubebwa kutoka kwenye html form kwenda kwenye code za ku process hizo taarifa na kuziweka kwenye database.

 

Tafadhali rejea mafunzo ya PHP level 1 somo la 10 hadi 12 utajifunza jinsi html firm ilivyo na jinsi inavyokusanya taarifa. Faili tutakalolitengeneza kwenye somo hili litakuwa na sehemu kuu 2 kama nilivyokwisha kukueleza hapo awali.

 

  1. Sehemu ya kwanza: html code

Sehemu hii ni kwa ajili ya kukusanya taarifa kwa kutumia html form. Form yetu itakuwa hivi

<form method="post" action="">

   <input type="hidden" name="add" value="1">

   <label>Name</label><br>

   <input placeholder="Name la menu"  name="name"><br>

   <label>Description</label><br>

   <input placeholder="Inahusu Nini"  name="description"><br>

   <label>Price</label><br>

   <inputtype="number" placeholder="Weka Price "  name="price"><br>

  <input type="submit" value="save">

</form>

 

Kama html form inavyojionesha hapao, Method (njia) itakafotumika kubeba taarifa ni method="post"  na kwakuwa faili letu litajiprocess lenyewe hivyo kwenye action hatuhitaji kuweka chochote kama unavyoona hpo patupu action="" tungeweka link ya faili ambalo lina code za ku process data tutakazo kusanya, ila sisi hatuhitaji  faili lengine.

 

form yetu ina user input 5, yaani taarifa zinazotakiwa kubebwa. 

 <input type="hidden" name="add" value="1">

Hii ni kwa ajili ya kuwezesha utumwaji wa taarifa. Taarifa zote hapa zitachakatwa kwa kuanzia hapa. Nimeipa jina la add name="add" na haiwezi kuonekana wakati wa kujaza.

 

<input placeholder="Name la menu"  name="name">

Hii ni kwa ajili ya kukusanya taarifa zinazohusu jina la menu unayotaka kuweka. Place holder ni sehemu ambay inabeba jina ambalo mtumiaji ataliona nalitamjulisha kuwa kijumba hicho kinahitaji kujaza nini. Usern input hapa imepewa jina la name name="name   

   

Pia  <input type="number" placeholder="Weka Price "  name="price"> hapa utaona kuna kitu kimeongezeka a,bacho ni type="number" type maana yake ni aina unaweza kusema kuwa ni aina gani ya data unahitaji ziweze kuwekwa kwenye hiyo sehemu. hapo kwa kuwa ni price himeamuwa iwe namba. Hivyo hutaruhusiwa kuweka herufi hapo.

 

Mwisho kuna <input type="submit" value="save"> Hii kazi yake ni ku submit, yaani kutuma taarifa, Yaani hiyo ni kama batani, ukiibofya taarifa zinatumwa na kupelekwa kwenye sehemu ambayo kuna code za ku process. Sehemu hii ndio inayotajwa kwenye action.                           

 

  1. sehemu ya pili: php codes

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

 

if(isset($_POST["add"])){

   $conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

   $name = ($_POST['name']);

   $description = ($_POST['description']);

   $price = ($_POST['price']);

 $sql = "INSERT INTO menu (name, description, price) VALUES ('$name', '$description', '$price')";

   if (mysqli_query($conn, $sql)) {

       echo "Data added";

   } else {

       echo "Error: " . $sql . "<br>" . mysqli_error($conn);

   }

   mysqli_close($conn);

}

 

?>

 

Hapa kuna vitu unatakiwa uvielewe mapema kabla ya kuenda mbele. NItakuchambulia kila part na kazi zake ili kwamba tuwe pamoja.

if(isset($_POST["add"])){}

Sehemu hii kazi yake kuu ni kuangalia taarifa kama zimejazwa, ni taarifa zipi zimebebwa. kwakuwa method tuliotumia ni POST ndio maana unaona hapo $_POST["add"] Kwa ufupi wa maneno ni kuwa sehemu hii kazi yake ni kuangalia taarifa zilizojazwa kutoka kwenye html form.

Baada ya kuwa taarifa zimeshakaguliwa sasa zinaweza kuwekwa kwenye mchakato. Hivyo utatakiwa kuzitengenezea variable kwa kila moja (rejea mafunzo ya php level 1 jinsi ya kutengeneza variable). 

$name = ($_POST['name']);

$description = ($_POST['description']);

$price = ($_POST['price']);

 

Kila input iliyokuwepo kwenye html form tunatakiwa tuitengenezee variable. kwakuwa data hizo zimebebwa kwenye method ya POT hivyo variable nayo kazima ichukuwe data hiyo kutoka kwenye post. Angalia mfano huu $name = ($_POST['name']); Kapa variable ni $name na value yake ni       ($_POST['name']) Kama unakumbuka kwenye html form input ambayo ilikuwa inachukluwa majina ya menu iliita name na hivyo kwa jina lilelile tunakwenda kuiita hapa ili tuweze kuzinyakwa taarifa zilezile.

 

Baada ya hapo tutaweka variable ya ku connect database kama tulivyojifunza $conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

Kisha variable ya ku weka data kama tulivyojifunza pia $sql = "INSERT INTO menu (name, description, price) VALUES ('$name', '$description', '$price')

Hakikisha unaziandika vyema. Kama utaangalia kwa makini hapa kuna utofauti kidogo na ambavyo tuliandaa sql variable kwa ajili ya kuongeza data.

 

Badala ya kutaja majina ya column za data zetu ambazo tunakwenda kuweka kwenye VALUE kuli tuliona kuwa tunaweka value ambazo tunataka kuweka. hapa sasa ndipo kwenye utofauti. kumbuka data zetu sisi tumeziingiza kupitia html form na kubebwa. Sasa hapa tutatumia vraiable ambazo tumezitengeneza. kwani variable si kazi yake kuwakilisha thamani. Na thamani yenyewe ni kile ambacho kimeingizwa kwenye html form na kubebwa mna POST method. 

 

Hivyo kwa umakini utaeka variable zako kwa mpangilio na mfuatano ulelule. Id haipo hapo ni kwa sababu yenyewe ni auto increment inajiandika yenyewe hatuhitajiki kuiweka sisi.

 

Baada ya hapo sasa ni kuangalia kama process imefanyika ama laa. kama imefanyika itatiambia data added. Tutatumia mtindo uleule tuliouzoea

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Data added";

} else {

   echo "Error: " . $sql . "<br>" . mysqli_error($conn);

}

 

CODE NZIMA ZA FAILI HILI

<form method="post" action="">

   <input type="hidden" name="add" value="1">

   <label>Name</label><br>

   <input placeholder="Name la menu"  name="name"><br>

   <label>Description</label><br>

   <input placeholder="Inahusu Nini"  name="description"><br>

   <label>Price</label><br>

   <input type="number" placeholder="Weka Price "  name="price"><br>

  <input type="submit" value="save">

</form>

 

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

 

if(isset($_POST["add"])){

   //prepare variable

   $name = ($_POST['name']);

   $description = ($_POST['description']);

   $price = ($_POST['price']);

   //connect database

   $conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

   //insert data in database

   $sql = "INSERT INTO menu (name, description, price) VALUES ('$name', '$description', '$price')";

   if (mysqli_query($conn, $sql)) {

       echo "Data added";

   } else {

       echo "Error: " . $sql . "<br>" . mysqli_error($conn);

   }

   mysqli_close($conn);

}

 

?>

 

 

 

Form itaonekana hivi

Mpaka kufikia hapa utakuwa umeweza kuongeza data kwa kutumia php na html form. Ili kuzisoma data hizo tumia njia ileile kama masomo yaliotangulia yanavyotueleza. Na huu ndio mwisho wa Course tumebakiwa na project moja ya kutengeneza Chat App. Baada ya projecy hiyo tutafunga course ya PHP na kuingia utengenezaji wa blog na website.

 

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT