MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2



Katika somo hili utajifunza namna ya kuunganisha databse na ukurasa wa wavuti kwa kutumia PHP.


Katika somo lililotangulia ulikuwa ni utangulizi wa course. hapa sasa ndipo tunakwenda kuanza somo letu rasmi. katika somo hili utakwenda kujifunza namna ya kuunganisha database kwenye faili la PHP. Hii ni hatuwa ya kwanza na muhimu unatakiwa uijuwe kama unataka kujifunza utengenezaji wa website na blog.

 

Ni kwa nini tunaunganisha PHP na databae?

Hili ni swali muhimu na ni la msingi sana. Jibu fupi ni kuwa ili uweze kuzisoma data zilizopo kwenye database kwenye blog yako ama website unahitaji uconnect na hiyo databse ili upate ruhusa ya kuziona hizo data,

 

Yaani ipo hivi, Fikiria kuwa una database inaitwa blog na  kwenye hiyo database kuna post kwa ajili ya blog yako. Sasa unataka hizo post zionekane kwenye blog yako. Kwanza utahitajika kuunganisha hiyo blog yako na hiyo database yako. kufanya hivi tutatumia php pamoja na ujuzi wa SQL kama tulivyojifunza katika course ya database. baada ya kuunganisha ndipo utaweza kuziweka hizo post kwenye ukurasa wa wavuti (web page)

Njia zinazotumika kuunganisha PHP na MySQL database

kwa maelezo ya w3school kuna njia kuu mbili za kuunganisha PHP na MySQL database. njia hizo ni:-

  1. MySQLi 
  2. PDO

Hiyi ya kwanza herufi i ina maana improved, na hiyo ya pili kirefu chake ni PHP Data Object) unaweza kutumia nji yeyote kati ya hizi. ila hii yenye MySQLi yenyewe inafanyakazi kwenye MySQL tu, lakini hiyo ya PDO inafanyakazi kwenye aina nyinginezo za database pamoja na hii ya MySQL.

 

Mambo muhimu kwenye wakati wa kkonect na database:

 

  1. kjuwa jina la database, passowd, na server
  2. kuanda variable kwa ajili ya kuunganisha na database.
  3. kufunguwa connection (open connection)
  4. kukonect kwenyewe (database connection)
  5. alert message hii ni kwa ajili ya kutoa taarifa kama kuna error ama kama umefanikiwa kukonnect
  6. kufunga connection

 

Kukonekt database kwa kutumia MySQLi:

kuna namna mbili ya kuunga database kwa kutumia MySQLi ambazo ni kama tutakavyoziona hapo chini. Unaweza kuchaguwa yeyote kati ya hizo. Utajifunza zaidi kuhusu njia hizi kwenye masomo yetu ya mbele.

  1. MySQLi object oriented
  2. MySQLi procedural

 

hatuwa kwa hatuwa kukonekt database:

 

  • Maandalizi ya variable: 

 

tulisha jifunza namna ya kuandaa variable kwenye course ya PHP somo la 3. katika kukonekt na databse variable zako ni tatu, kwa ajili ya server, kwa ajili ya database (jina la database) na kwa ajili ya password. Variable zako zinaweza kuwa hizi:

$servername = "localhost";

$username = "username";

$password = "password"

 

localhost ni jina la server ambayo databse yetu ipo. kama unatumia wapserver, ama xamp au aWevServer kwa watumiaji wa simu basi jina la server yako ni localhost. uername ni jina la mtumiaji wa hiyo database. Hii ni akaunt inayomiliki hiyo databse. kama hujabadili jina ama username kwenye database yako basi jina lililopo ni root. na password kama unatumia local host mara nyingi password hakuna unaacha kama ilivyo, hivyo variable hapo zitasomeka  hivi

 

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = ""

 

 

  • kufunguwa database na kuconnect

 

Bada ya kuziweka variable zako sasa ni muda wa kuunganisha PHP na database kwa kutumia hizo variable. Kuna variable nyingine sasa tunatakiwa kuijuwa na hii ni muhimu kwa ajili ya kufanya hiki tunachokitaka. variable hii hutumiaka kuunganisha database. variable hii ni

$conn = new mysqli($servername, $username, $password);

variable $conn inakwenda kuwakilisha function new mysqli()ambapo ndani yake utawka variable zako za database name, server name na username. hivyo kusomeka

$conn = new mysqli($servername, $username, $password);

 

 

  • Kuangalia kama connection imefanikiwa ama imefeli

 

Hapa kuna jambo unatakiwa ulijuwe, ni kuwa unatakiwa uweke meseji ambayo itakueleza kama connection imefanikiwa ikuambie mfani you are connected. na kama connection imefele inatakiwa iseme mfano connection failed. kwa haraka haraka hapa utajuwa kuwa panatakiwa patumike condition sentenses kama tulivyojifunza kwenye php matumizi ya if, else, ifelse n.k.

 

kufanya hivi tutatumia

if (mysqli_connect_error()) {

die("connection failed " . mysqli_connect_error());

}

echo "you are connected";

 

Hapo panajionyesah wazi kuwa mysqli_connect_error() ni kwa ajili ya kuangalia kama connection imefanikiwa ama imefeli. kama imefele itareject (die) hivyo if itatupa matokeo connection failed. Na kama connection imefaniliwa if itatupa matokeo ya else itatupa matokeo ya you are connected.

 

 

  • Kufunga connection

 

Katika hali ya kawaida, connection hijifunga automatik. lakini pia unaweza kuifunga wewe mwenyewe punde tu baada ya kuconnect. kufanya hivyo utatumia $conn->close();kwa Myqli object oriented au mysqli_close($conn);kwa MySQLi procedural au $conn = null; kwa PDO

 

CONNECTION NZIMA IPO HIVI:

Tengeneza faili la php kisha lipejina mfano test.php. hakikisha unaweka faili hilo kwenye localhost server kama ulivyoelekezwa kwenye mafunzo ya php. Kisha pest code hizo hapo chini, load file, itakuletea meseji you are connected kama imesha connect.

 

  • MySQLi object oriented

 

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

 

// Kufanya connection

$conn = new mysqli($servername, $username, $password);

 

// Kuangalia connection

if (mysqli_connect_error()) {

   die("you are not connected: " . mysqli_connect_error());

}

echo "You are connected";

?>

 

hii itakupa matokeo

kama ukijaribu kubadilisha hapo mfano wela username karatasi, itakupa error.

kama unatumia localhost meeji hii ya error itaambatana na maelezo marefu kukuambia error imetokra wapi. kama inavyojionyesha pic hapo chini. Error hii itajitokeza pekeyake kama utahost website yako.

 

 

  • MySQLi procedural

 

Tengeneza faili la php kisha lipejina mfano test.php. hakikisha unaweka faili hilo kwenye localhost server kama ulivyoelekezwa kwenye mafunzo ya php. Kisha pest code hizo hapo chini, load file, itakuletea meseji you are connected kama imesha connect.

 

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password);

 

// Check connection

if (!$conn) {

   die("You are not connected: " . mysqli_connect_error());

}

echo "You are connected";

?>

 

Hapa utaona kuna tofauti kidogo kati ya tulivyoona hapo mwanzo na hapa. Utaona kuna mabadiliko kwenye kukonect na kwenye kutoa error. Utachaguwa mwenyewe ni njia ipi utumia ila zote zinakupa matokeo sawa. Tutajifunza zaidi utofauti wao masomo ya mbeleni.

 

Kukonekt database kwa kutumia PDO:

kama nilivyokueleza hapo mwanzo kuwa hakuna utofauti mkubwa kati ya MySQLi na PDO. ila kama unataka kutumia MySQL tu kwa ajili ya databse yako, ukitumia MySQLi hakuna shida. na kama una matarajio kuwa siku za mbeleni utumie aina ingine ya databse kwenye blog ama website yako basi PDO inakufaa maana yenyewe inaweza kufanya kazi kwenye zaidi ya aina 10 za database.

 

sasa katika PDO tofauti na variable kuu tatu tulizoziona hapo juu hapa utatakiwa utaje na jina la database yako. yaani PDO inahitaji iunganishwe kwenye datanase husika tu na si vinginevyo. na hii ni tofauti yao ingine na MySQLi. katika Somo la PHP tulitengeneza databse yetu utaipata somo la 8,9 na 10. database hiyo iliitwa hotel. hivyo tutaitumia database hii katika siku zijazo. hapa tutaitumia kuconnect na PDO.

 

Code za ku connect PHP kwa kutumia PDO

Tengeneza faili la php kisha lipejina mfano test.php. hakikisha unaweka faili hilo kwenye localhost server kama ulivyoelekezwa kwenye mafunzo ya php. Kisha pest code hizo hapo chini, load file, itakuletea meseji you are connected kama imesha connect.



<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

//kuweka connection

try {

   $conn = new PDO("mysql:host=$servername;dbname=hotel", $username, $password);

   // kuangalia connection

   $conn->setAttribute(PDO::ATTR_ERRMODE, PDO::ERRMODE_EXCEPTION);

   echo "you are connected";

} catch(PDOException $e) {

   echo "you are not connected: " . $e->getMessage();

}

?>



Kufunga connection:

weka hizo code za kufunga connection nimekuonyesha, weka mwisho kabla ya tag ya ?>. Mfano:



<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

 

// Kufanya connection

$conn = new mysqli($servername, $username, $password);

 

// Kuangalia connection

if (mysqli_connect_error()) {

   die("you are not connected: " . mysqli_connect_error());

}

echo "You are connected";

$conn->close();

?>

 

Endelea kufanya mazoezi, tukutane somo la tatu tutakapojifunza jinsi ya kutengeneza databse kwa kutumia PHP. Somo linalofata litategemea na msingi wako kutoka kwenye somo hili la pili.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT