MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4



Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutengeneza table kwenye databse yako kwa kutumia PHP


Katika somo lililotangulia tumejifunza namna ya kutengeneza database kwa kutumia PHP. Hivyo umejifunza pia namna ya kuandaa variable kwa ajili ya kutumia SQL. Hivyo katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza table. Tafadhali rejea mafunzo ya database level 1 kujikumbusha naman ya kutengeneza table.

 

Maandalizi

Maandalizi ni yale yale tuliokwisha kuyaona. kwanza ni kuandaa variable zinazohusu database, server na password, kisha ijuwe SQL ststement za kutengeneza table, kisha ujuwe ku connect database. Hivyo nitakuorodheshea haya yote ili iwe rahisi kwako.

 

  1. Variable zinazohusu database:

Hapa kuna variable nyingine tutaiongeza nayo ni variable ya kuwakilisha jina la database. Yaani kwa kuwa tunataka kutengeneza table, lazima sasa tuseme table hiyo tunakwenda kuitengenezea kwenye database ipi?. Hivy hapa nitatumia $dbname kunaanisha database name, hivyo kuwakilisha jina la database.

 

katika somo lililopita tulitengeneza databse iliyoitwa hoteli. Hivyo katika somo hili tutakwenda kutengeneza table yenye jina menu katika hiyo database yetu ya hotel. kumbuka jina la server ni localhost, na username ni root. password hakuna, hivyo patakuwa kama palivyo.

 

//kuandaa variable

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";



  1. SQL statement za kutengeneza table

CREATE TABLE IF NOT EXISTS `menu` (

  `id` int(100) NOT NULL,

  `name` varchar(255) NOT NULL,

  `description` varchar(255) NOT NULL,

  `price` int(100) NOT NULL

) ENGINE=InnoDB DEFAULT CHARSET=utf8mb4;

Hii ni table tulioitengeneza katika somo la 9 mafunzo ya database bofya hapa kurejea somo

 

  1. variable za ku connect database

/ Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password);

 

  1. function kwa ajili ya kuangalia kama kuna tatizo ama umefanikiwa. apa ndipo tunatumia if else statement, kwa ajili ya kueleza kama table imefanikiwa itatuambia “table menu imetengeneza” Vinginevyo itatuambia “kuna tatizo” Tafadhali rejea mafunzo ya PHP kurejea jinsi condition ststement zinavyofanyakazi.

 

mysqli_query($conn, $sql)

 

Jinsi ya kutegeneza table:

Hapa ni kama ambavyo tumejifunza katika somo lililotangulia. Kitu ambacho kinabadilika ni pale tulipoweka SQL statemet za kutengeneza database hapa tutaweka za kutengeneza table. Hivyo code nzima zitaonekana hivi:-

 

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Kufanya connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// kuangalia connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " . mysqli_connect_error());

}

 

// sql to CREATE TABLE IF NOT EXISTS

$sql = "CREATE TABLE IF NOT EXISTS `menu` (

 

 `id` int(100) NOT NULL,

 

 `name` varchar(255) NOT NULL,

 

 `description` varchar(255) NOT NULL,

 

 `price` int(100) NOT NULL

 

) ENGINE=InnoDB DEFAULT CHARSET=utf8mb4;";

 

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Table menu imetengenezwa";

} else {

   echo "Kuna tatizo " . mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>

 

Tengeneza faili la php kwenye local host kisha pest code hizo. ukimaliza funguwa faili hilo kwa kutumia browser yako, kama umeenda vizuri itakupa ujumbe kuwa tab menu imetengenezwa.

 

Tukutane somola 5 tutakapojifunza namna ya kufuta table na database. hakikisha unaelewa vyema somo lililotangulia kwani masomo haya yote yanategemeana. masomo yatakayofuata yatakuwa ni mazuri zaidi endapo haya yaliopita yameeleweka vyema.



Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT