MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5



Katika somo hili utajifunza namna ya kufuta table na databse kwa kutumia PHP


Tumesha jifunza namna ya kutengenezadatabase na table kwa kutumia PHP. Sasa somo hili tutajifunza namna ya kufuta database na table. Unaweza kufuta vyote kwa pamoja ama kufuta kimoja kimoja. Endapo utachaguwa kufuta table tu, basi database itabakia lakini ukifuta database, na table pia itafutika na data zilizomo.

 

Maandalizi makubwa hapa ni kama yaliotangulia Andaa variable zote zinazohitajika kama vile server name, database name, username, na password. Tutakwenda kufuta table yenye jina menu kwenye databse inayoitwa hotel. Hivyo database name yetu itakuwa hotel

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

Katika mafunzo ya database hakuwahi kusoma namna ya kufuta table kwa kutumia SQL. Sasa hapa nitakwenda kukujuza jinsi ya kufanya hivyo. SQL inayotumiaka ni DROP TABLE kisha unaweka jina la database yenye hiyo table kisha utaweka kidoto kati kisha ndipo utaweka jina la hiyo database. mfano DROP DATABASE hotel . menu. Hivyo variable ya statement hii itakuwa  $sql = "DROP TABLE `hotel`.`menu`";

 

Baada ya hapo utaandaa if else kwa ajili ya kukupa mrejesho kama umefanikiwa ama umefeli. Kama tulivyoona katika masomo yliyopita kufanya hivyo tutatumia function hii mysqli_query($conn, $sql)

 

CODE ZA KUFUTA TABLE ZITAONEKANA HIVI    

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// Check connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " . mysqli_connect_error());

}

 

// delete database

$sql = "DROP TABLE `hotel`.`menu`";

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "table DELETED successfully";

} else {

   echo "Error DELETING table: " . mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>



JINSI YA KUFUTA DATABASE

Hakuna tofauti kubwa sana kati ya kufuta table na kufuta database. Kinachobaldilika hopo ni SQL statement baada ya DROP TABLE hotel.menu itakuwa DROP DATABASE hotel. baada ya hapo utafunguwa faili lako kwenye browser na majibu utayapata. ila hakikisha umebadili alert message za kujulisaha kuwa table imefutwa kuwa zikujulishe kuwa database imefutwa.

 

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// Check connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " . mysqli_connect_error());

}

 

// delete database

$sql = "DROP database `hotel`";

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Database DELETED successfully";

} else {

   echo "Error DELETING database: " . mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>

 

Mwisho

Tukutane somo la 6 tutajifunza jinsi ya kuweka data kwenye databse kwa kutumia PHP. Pia tutajifunza kuedit data hizo. Somo hili litakuwa chachu ya kujifunza matumizi ya html form katika kukusanaya madodoso.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT