MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9



Katika somo la 8 ulijifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa taarifa unazozisoma kutoka kwenye atabase. Katika somo hili utajifunza namna ya ku update na kufuta taarifa zilizopo kwenye database.


Ili ku update data tunatumia UDATE na kufuta tunatumia DELETE. Ni muhimu sana kujuwa kufuta na ku update taarifa kwa sababu mbalimbali. Hatahivyo unatakiwa pia uwe makini wakati wa kufuta taarifa, kwani usipoangalia makini command zako unaweza kujikuta unafuta data zote ama table ama database, ama ukafuta row tofauti na uliokusudia.

 

  1. ku update taarifa kwenye database.

Mfano tunataka kubadili price kwenye ugali kutoka 1500 kuwa 1000. hivyo hapa tutatakiwa ku update taarifa hizi. Kitu cha kwanza unachotakiwa kujuwa ni id ya ugali ni ngapi kwenye table yako. Kulingana na table yetu ya menu ad ya ugali ni 1.

 

Jinsi yakuandaa SQL ya kuweza ku update taarifa

Utaandika UPTADE kisha ikifuatiwa na jina la table mfano UPDATE menu kisha utaandika SET ili kuweza kuset hizo data mpya. mfano UPDATE menu SET itafuatiwa na column unayotaka kui update ikifuatiwa na alama ya =, kwakuwa sisi tunataka ku update column ya price itakuwa hivi UPDATE menu SET price baada ya hapo ni kuweka VALUE au thamani ya hizo data unazotaka ziwe, hakikisha ziwe ndani ya ‘’ kama string (rejea mafunzo ya php kuhusu string). hivyo itakuwa UPDATE menu SET price = ‘1000’ hapa itafuatiwa na WHERE kisha utaweka id ya hiyo row yako. hiyo itakuwa hivi UPDATE menu SET price = ‘1000’ WHERE id = 1

 

kinachofuata ni kuandaa variable zako kwa ajili ya ku connect na database kama tulivyoona katika masomo yaliopita. Variable ya ku update sasa itasomeka hivi 

$sql = "UPDATE menu SET price='1000' WHERE id=1";

 

Sehemu zilizobakia kila kitu hakuna mabadiliko mengi. Hivyo code nzima za ku update ugali zitasomeka kama hivi

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// Check connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " . mysqli_connect_error());

}

 

$sql = "UPDATE menu SET price='1000' WHERE id=1";

 

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Record updated successfully";

} else {

   echo "Error updating record: " . mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>

 

 

  1. Kufuta data kwenye database.

Kama tulivyoona kwenye ku udate kwanza lazima ujuwe id ya hicho unachokwenda kuki update. Basi hata ku delete nako lazima ujuwe id ya hicho unachokwenda kuki delete. sasa chukulia kuwa hatuitaki menu ya ugali hivyo tunataka kuifuta kabisa. Kifanya hivi tutatumia DELETE.

 

Jinsi ya kuandaa SQL kwa ajili ya ku delete.

kwanza utaanza na neno DELETE likifuatiwa na FROM likifuatiwa na jina la table ambalo ni menu likifuatiwa na neno WHERE likifuatiwa na id pamoja na alama ya = kisha utaweka id ya hiyo data unayotaka kufuta. Mfano wa sql hii ni DELETE FROM menu WHERE id = 1. Hivyo variable ya SQL itakuwa hivi 

$sql = "DELETE FROM menu WHERE id=1";

 

Baada ya hapo ni kuandaa variable zote zinazohitajika ku connect database. Rejea masomo yaliopita. Hivyo code nzima za ku delete zitasomeka kama hivi:-

<?php

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// Check connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " . mysqli_connect_error());

}

 

// sql to delete a record

$sql = "DELETE FROM menu WHERE id=1";

 

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Record deleted successfully";

} else {

   echo "Error deleting record: " . mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>

 

Tukutane somo la 10 tutakapojifunza jinsi ya ku search (kutafuta ) taarifa maalumu kwenye database.

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: [email protected]



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 SOMO LA 3


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 4


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 5


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 6


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 7


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 8


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 9


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 10


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 11


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 12


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 13


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 14


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2 SOMO LA 15 PROJECT