MAFUNZO YA PHP LEVEL 3 SOMO LA 1



Katika somo hili utajifunza kuhusu variable kwenye PHP. Utajifunza aina mbalimbali za variable na jinsi zinavyotofautiana.


MAFUNZO YA PHP LEVEL 3 SOMO LA 1

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu variable,na aina zake. Pia tutakwenda kujifunza kuhusu const na define. Naamini kuwa umeshapitia mafunzo yetu level 1 na 2.

 

Kwenye php variable zimegawanyika katika makundi makuu mawili 3. Katika php tunaita variable scope ambazo ni kama:-

  1. Local 

  2. Global

  3. Static

Katika level hii utajifunaza aina zote hizi za variable pamoja na matumizi yakle.

 

Variable ni nini?

Variable ni kitu kinachowakilisha taarifa kwenye program. Ni chombo kinacho beba taarifa fulani. Kwa mfano unaweza kusema X inamaanisha embe, na b inamaanisha dodo. Kisha ukaweka sentensi nipatei embe xb kwa maana embe dodo. Hebu tuone mfano hao chini:

 

Mfano 1

<?php

$x = "embe";

$b = "dodo";

echo "Nipatia $x $b";

?>

 

Hii itakupa matokeo haya

Hapo utakuwa umeona namna ambavyo $x na $b zilivyotumika kuwakilisha taarifa na kutengeneza sentensi nzima. Sasa hebu tuone namna ambavyo variable scope zinafanya kazi ama mgawanyiko wa variable.

 

  1. Globe variable: 

Global variable ni variable iliyotengenezwa nje ya function. Variable hii itatumika nje ya function na si ndani ya function. Tutajifunza zaidi uhusu function. Ila unaweza kurejea level 1 mafunzo haya ya php, utajifunza zaidi kuhusu function.

 

Function yenyewe ni block ya code, sasa endapo variable itapewa thamani  nje ya function hii  kutumika nje ya function tu, variable hii itaitwa global variable. Angalia mifano hapo chini

 

Mfano wa function

<?php

 

function hi(){

   echo "haloo bongoclass";

} //mwisho wa function

 

echo hi();

?>

 

Function hii itakupa matokeo haya:-

Sasa wacha tuone ni kwa namna gani gobal variable inaweza kutumika nje ya function na si ndani.

 

Mfano

<?php

$x = 'embe'; //$x ni imepewa thamani nje ya cuncton

$b = 'dodo'; //$b na $x ni global variable kwa kuwa ipo nje ya function

function hi(){

   echo "nipatie $x $b"; //$x na $b zipo ndani ya function

}//mwisho wa function

 

echo hi();

?>

 

Hii itakupa erro kwa sababu global variable haiwezi kutumiwa ndani ya variable.

 

Sasa ngoja tuiweke variable nje ya function tuione je itafanya kazi?

<?php

$x = 'embe'; //$x ni global variable

$b = 'dodo'; //$b ni global variable

function hi(){

   echo "halooo"; //$x na $b zipo ndani ya function

} //mwisho wa function

echo hi();

 

//variable $x na $b zipo  nje ya function

echo "Nipatie $x $b"

?>

 

Hapa utapata matokeo vyema kwa sababu variable zimetumika nje ya function. Hivyo basi variable $x na $b ni global variable.

 

 

Jinsi ya kuifanya global variable iweze kutumika ndani ya function.

Ili kuweza kuifanya global variable kuweza kutumika ndani ya function tutatukia php keyword “global”. Angalia mfano ufuatao

<?php

//global variable

$b = 'bong';

$c = 'class';

 

//function

function mfano(){

  

   echo $b, $c;

}

mfano()

?>

 

Mfano huu utakupa error kwa sababu variable $b na $c ni global hivyo haziwezi kutumika ndani ya function. Sasa ili tuweze kuitumia varible hizi ndani ya function tutatunia “global” keyword.

 

<?php

//global variable

$b = 'bong';

$c = 'class';

 

//function

function mfano(){

global $b, $c;

   echo $b, $c;

}

mfano()

?>

 

Sasa variable $b na $c zimetumika ndani ya functiona na kutupatia matokeo bongoclass.

 

 

  1. Local variable 

Hii ni variable ambayo imetengenezwa ndani ya function. Variable hii itaendelea kutumika ndani ya function husika. Kwa mfano:

<?php

function mfano(){

   $b = 'bong';

   $c = 'class';

 

   echo $b, $c;

}

mfano()

?>

 

Hii itatupa majibu

Katika mfano huu variable $b na $c ni local variable kwa sababu zimetengenmezwa ndani ya function na zimetumika ndani ya function.

 

  1. Static variable

Wakati mwingine unataka matokeo ya variable yako yawe endelevu. Sasa php hufuta local variable kila inapomaliza kufanya kazi. Hivyo ikimaliza kufanya kazi ya variable itahitajika kuandikwa upya ili iweze kufanyika kwenye matendo yanayofuata. Sasa kwa kutumia keyword static utaweza kuifanya variable hii iendelelee kutumika ndani ya functiion hata baada ya kufanya kazi mara ya kwanza. Angalia mfano hapo chini:

 

<?php

function namba() {

   static $x = 0;

   echo $x;

   $x++;

}

 

namba();

echo "<br>";

namba();

echo "<br>";

namba();

?>

 

Hii itakupa matokeo

Katika mfano huo utaona kila function namba() ilipotumika imechukuwa majibu ya mwanzo na kuyajumlisha na 1 na kuendeleza tendo. Mwanzo $x ambayo ndio static variable iliyopataikana baada ya kuweka keyword static. Kabla ya keyword static $x ilikuwa ni local variable. Hivyo isingeweza kutupa majibu haya, ingetuonyesha 000 kwa kuwa function imeitwa mara 3. Saba baada ya kuibadili local variable $x kuwa static kwa kutumia keyword static tumeweza kuitumia kila tulipoiita function.

 

Turajifunza somo hili kwenye masomo yajayo. Kwa sasa tambuwa uwepo wa aina 3 za variable ambazo ni global, static na local.

 

Tukutane somo la 2 tutajifunza kuhusu php constatnt na jinsi zinavyoweza kufanya kazi.



Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa


Post Nyingine


MAFUNZO YA HTML LEVEL 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 1


MAFUNZO YA HTML LEVEL 1


MAFUNZO YA DATABASE


PROJECT ZA MAFUNZO LEVEL 1


MAFUNZO YA PHP LEVEL 2


MAFUNZO YA PHP LEVEL 3 SOMO LA 1