MAFUNZO YA PYTHON LEVEL 1 SOMO LA 1


picha


Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.


Python ni moja katika lugha za kikompyuta zilizo maarufu. Ilianzishwa mwaka 1991 na Guido van Rossum. Python ni moja katika high level programming language ambayo ni general programming language yaani inatumika kwenye field nyingi.

 

Python imekuwa ikifanyiwa marekebisho mengi toka ilipoanzishwa na sasa tupo katika toleo la 3 yaani python 3. Katika course hii tutakwenda kutumia toleo la 3 la python.

 

Matumizi ya python

  1. Hutumika kwenye kutengeneza website, web app na blog kama sever side langage. Yaani ku wasiliana na server .
  2. Hutumiaka kwenye kutengeneza software mbalimbali kama game
  3. Hutumika kufanya mahesabau kama kwenye takwimu.
  4. Pia huweza kutumika kuwa kama system scripting.

 

Python file extension:

Kama ilivyo kuwa language zote zina extension kama ilivyo hatml ni .html, php ni .php, basi na python ni .py. Mfano main.py

 

Maandalizi kwa ajili ya course hii:

 

Kwa watumiaji wa kompyuta:

Course zinazopatikana bongoclass zinalenga wanafunzi wa aina zote. Kwa wale wanaotumia kompyuta na wale waotumia simu janja. Sasa kwa wale wanaotumia kompyuta fuata maelekezo haya:-

  1. Kwanza install python. Njia rahisi ya kuistall python ni kuwa na python IDE. Ninapendelea utumie pytharm kutoka jetbrain. IDE hii ni rahisi kutumia na haihitaji configuration nyingine. Fuata link hii  https://www.jetbrains.com/pycharm/download/download-thanks.html?platform=windows&code=PCC
  2. Baada ya ku download install hiyo software. Hakikisha una internet ili kwamba kama itahitaji ongezeko la tools iweze ku download. Hata hivyo software hii ni ya offline
  3. Baada ya kumaliza ku install, bofya icon yake ili kuifunguwa. Hapo utakutana na ukurasa huu.

 

Hapo bofya palipoandika New Project.kisha utakuja ukurasa mwingine ambao ni huu

 

Kama ndio mara yako ya kwanza hapo usiset kitu chochote zaidi ya jina la project yako tu. hapo mwanzoni kabisha kuna palipoandikwa pythonProject 

Badili jina la project yako kutoka pythonProject kuwa jina unalotaka wewe. Kwa mfano mimi nitasema pythonMafunzo 

Baada ya hapo bofya create kwa chini upande wa kulia. Itaanza kuload ili kuandaa mazngira ya hiyo project yako. Baada ya kumaliza utakutana na ukurasa mkubwa ambao ndio uwanja wa kuanzika code zako.

 

Kwa upande wa kushoto kuna project root. Ambapo kuna faili linaonekana limefungka kwa upande wa kulia na kuna code utaziona. Faili hilo linaita main.py hilo ndio faili la kwanza la project yako.

 

Sasa fanuya hivi. Kwenye huo ukurasa uliofunguka upande wa kulia futa kila kitu kisha weka code hizi:

print("haloo bongoclass")

 

Baada ya hapo run hizo code kwa kubofya kialama cha ku play kilicho upande wa kulia kwa juu

 

Angalia kwa chini kuna ukurasa umefunguka. Ukurasa huo utaochesha vitu vitatu:-

  1. Location ya hilo faili
  2. Matokeo ya hizo code
  3. Uwepo wa error

 

Hiyo namba 1 inaonyesha hilo faili linapatikana wapi kwenye kompyuta yako. Hiyo namba 2 ndio matokeo ya code zetu. Kwa mfano hapo utaona haloo bongoclass hayo ni matokeo ya code ambayo tumeandika hapo juu. Ha hiyo namba tatu utaona kuwa code 0 kumaanisa kuwa hakuna tatizo. Kama umefiika hapo basi kompyuta yako ipo tayari kuendelea ku code python.

 

Location ya project yako:

Ili kujuwa mahali ilipo  project yako utakwenda kwenye local disc c, kisha user kisha jina la user wa kompyuta yako, kisha shuka mpaka chini utakuta folder limeandika pycharmProject. Hapo ndipo project yako utaikuta.

 

Kwa watumiaji wa kompyuta somo letu limeishia hapa. Tkutane somo la pili ambapo tutakwenda kuzungumzsia sheria za kuandika code ya python.

 

Kwa watumiaji wa simu:

  1. Ingia play store kisha tafuta app inayoitwa Python 3 - IDE for Python 3 kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. App hii ukisha install haihitaji ulazima wa kuwa na internet. Pia ina uwezo wa ku install extensions

 

  1. Baada ya hapo utaifungauwa. Kuna setting utatakiwa kuzifanya. Angalia picha hizo hapo chini.