Siri ya wageni wale

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana.

Siri ya wageni wale

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA
Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Tulikuwa ni marafiki sana tukiwa katika umri wa miaka 7 mapka 18. baba yako alikuwa ni mchamungu toka alipokuwa mdogo. Alipata malezi mema sana. Na mimi nilivutiwa nikawa nirafiki yangu sana. Tulikuwa tukifanya ibada pamoja na karibia mambo yetu yote. Wakati nilipohama Misri kuja Yemeni niliweka ahadi na baba yako kuwa nikipata mtoto wa kike ataolewa na mtoto wake na akiwa wa kiume atauoa wako, na tulimuomba Mungu atutofaitishie watoto wetu, yaani akiwa wangu wakike wake wa kiume ama wake wa kike wangu awe wa kiume.



Miaka mingi ilipita hata tukasahau ahadi zetu. Mimi nilichelewa kupata mtoto na hata yeye. Hata hivi miaka yapata 17 iliyopita nikajiwa na wageni wa ajabu, kisha akataja kisha kama kile kilichomtokea baba. Kisha akaenelea kusema. Wageni wale walikuwa si watu wa kawaida. Ni wajumbe waliotumwa kuja kutukumbusha ahadi zetu na kutupatia habari njema za kaupa watoto. Siku ya mwisho walipoondoka wageni wale walinieleza kuwa mtoto wako atao;ewa na mtoto wa rafiki yako kaam ahadi. Atakuja mwenyewe, na utamjuaje wakaniachia pete hii iliyokufikia. Walinieleza kuwa pete hii ikifika mikononi mwako katu haitaondoka.



Wakanieleza kuwa sifa zako utakuwa ni muuza viatu. Hivyo binti yangu anayemsaidia kazi mke wangu nilimuagiza aje kwako kuuliza viatu kama walivyonieleza wageni wale sifa za viatu. Nikamueleza kama utamuona mtu aliyebadilika utambue huyo ni mtu ninaye mtafuta. Mwambie aje kwangu. Sasa nilikuwa na ugomvi na matajiri wenzangu waliotaka kumuoa binti yangu, niliwakatalia sana, na ndipo wakapanga njama ya mumuua.



Bila ya kutambua wakamuua yule mfanyakazi wangu wakidhani ndiye binti yangu. Baada ya tukio lile kutokea na pete kupotea bikajua kuwa pete imesafika kwa mwenyewe, maana wageni wale walinieleza katu ete isingeweza kuibiwa, ila itamfikia mwenyewe. Baada ya kumaliza kuzungumza akaniambia kuwa nisiendelee tena kuwatafuta wageni wale katu sitawaona. Akamuita binti wake nije nimuone.



Akaja binti mmoja akafunua sura yake. Nilihisi kama nimepigwa shoti kwenye mwili wangu. Ghafla joto likapanda, nilistaajabu kabisha kuona kuwa kumbe duniani kuana mabinti warembo kiasi kile. Nilijisemea kuwa wale waliotaka kumuoa hawakukosea katu. Kwa kweli binti alikuwa ni mzuri sana. Kisha mzee akasema 'mwanangu nitakuozesha binti yangu bure ila kwa sharti kuwa uwe ni kama mwanangu'



Nilikubali na ndipo nikaozeshwa. Nilimuoa mke wangu nikiwa sina mkono mmoja. Bada ya harusi niliishi na mke wangu kwa muda wa miaka 5. kumbe kulikuwa na watu wananifanyia uaduni. Na ndipo wakanifanyia uchawi nikapata jini hili lililokuwa likinisumbua. Tulipata sifa zako ndipo tukaja Baghadad kupata matibabu. Ha hii ndio hadithi ya kukatwa mkono wangu.



Baada ya tabibu kusimulia hadithi hii akamuelekea Sulatani na kumuuliza 'Je! Sultani hadithi hii haiwezi kuwa nzito kama kifo cha mtoa burudani?' mfalme akajibu angalau ila bado. Kama haitahadithiwa hadithi nyingine iatakayoshinda hii, wote mtapoteza vichwa vyenu. Basi hapo Mshona nguo akaja mbele na kusema ' Mtukufu nitasimulia kisa kilichomtokea huyu marehemu jana,kitakuwa ni cha kushangaza zaidi kuliko hadithi za wenzangu waliotangulia kusimulia. Akaanza kusimulia kama ifuatavyo:-





Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 196


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...

MNYAMA ANAYEKIMBIA ZAIDI YA WOTE
4. Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Kwa nini vidole vimekatwa
HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad. Soma Zaidi...

SAFARI SABA 7 ZA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI SABA ZA SINBAD Katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Soma Zaidi...

Kamaralzaman arudi kwao
SAFARI YA KURUDI NYUMBANI Kamaralzamani siku hiyo akamfuata baba mkwe wake na kmueleza ukweli wa mambo na kuwa yeye si mganga. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 03: Nurdini na Mtumwa
Siku ya tano Nurdini alipata taarifa kutoka kwa watu wake yaani wafanyakazi wa chumba chake kuwa kuna binti mgeni ameletwa ila ametengewa sehemu yake maalumu. Soma Zaidi...

SAMAKI WA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)
Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 03
Tatua mzozo wa NI NANI MUUAJI? Soma Zaidi...