MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME


MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME



Binti mfalme aliendelea kukodoa macho yake kwa Aladini, hivyohivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Aladini. Binti mfalme aliapia kwenye moyo wake kuwa hajapatapo kuona kijana aliyemvutia zaidi ya Aladini. Ndiyo yaliyopita kwenye nafsi ya Aladini kuwa naye hajapatapo kuona binti aliyemvutia kama binti Sulatani. Wawili hawa walikuwa kama wakiongea kwa kutumia nafsi. Ndege alipomaliza kazi yake ya kuunganisha nafsi za waungwana hawa wawili alipotelea msituni. Binti sultani hakuendelea kumuangalia Aladini kwa kuhofia kugundulika. Binti akadai anaumwa hivyo apelekwe nyumbani kwa araka. Lengo lake ilikuwa ni kuondoka pale kabla Aladini hajaonekana na Askari.


Binti alipofika nyumbani homa ilimjia kweli na hakuweza kula kitu. Ukweli ni kwamba hakuna na homa ya ugonjwa ila ni msukuno wa moyo wake kwa kijana asiyemjuwa jina wala sauti. Kijana aliyemtovu wa nidhamu aliyediriki kwenda kumchungulia. Kijana aliyediriki kukodolea macho sura ya binti mfalme hata bira ya kupepesa. Tabasamu la Aladini liliendelea kuzunguka kwenye kichwa cha binti huyu. Halima binti sultani hakuweza kulala usiku mzima. Aliweza kuutumia usiku vyema katika kumtafakari kijana aliyemuona, aliendelea kuzungumza na nafsi yake na hatimaye akapata hitimisho kuwa kama kweli aliyemuona ni mtu atakuja kumposa.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Aladini ambaye hakweza kulala hata kidogo usiku. Toka asubuhi ili alipokutanana binti sultani. Mambo mengi aliwaza Aladini, kuhusu ndege aliyewaunganisha, rangi za ndege zilifanana sana na rangi alizoziona kwenye pango lile. Aladini mawazo yalimpeleka mbali sana hata akawaza jinsi watu wenye nyadhifa zao wanavyokuja kwa Sultai kumposa binti yake, watoto wa wafalme na mawziri wanavyokuja kumposa bint Sulatni. Fikra za Aladini zikaenda mbali sana hata ikimjia kuwa posa zte hizo binti Sultani alikuwa akizikataa, eti kwa sababu anampenda Aladni.


Fikra za Aladini hazikuishi hapo akawaza zaidi namna ambavyo amevaa nguo nzuri na za thamani. Manukato ya kuvutia kwenye kuo zake yaliweza kusambaa kila apitapo. Watu wakimkodolea macho na mabinti kumkonyeza. Aladini anaelekea kwa Sulatani kweda kutoa posa. Aladini aliendelea kuwaza eti anafika kwa Sulatani, anamkua Sultani amekaa kwenye kiti kireefu sana, kikubwa kilicho na mapambo ya dhahabu na miguu yenye vishikizo vya Almasi. Fikra za Aladini zilienda mbali zaidi, wakati anakutana na Sultani hata kabla ya kuzungumza binti Sultani akaja na kumkumbatia. Sultani alichukizwa na tabia hiyo na kumuamuru Aladini akatwe kichwa chake. Askaria akanyanyua upanga tayari kuondoa kichwa cha Aladini. 'mamaaa nakufaa' ghafla Aladini akashitka kutoka kwenye mawazo yake.


Hii haikuwa ni ndoto, ila pia haikuwa ni ukweli, ilikwua ni miusanyiko ya fikra zilizopatwa na nguvu ya mapenzi. Mama alitoka mbio kwenda kwa mwanaye kujuwa anasumbuliwa na nini usiku huo. Aladini hakuwacha kuzungumza kila ambacho kimetokea. Mama alisikitika sana kwani aliamini sio kazi ndogo ya kumpata mtoto wa sultani kwa watu walio na hadhi za chini na umasikini kama yeye. Siku ilifata asubuhi binti sultani na Aladini kila mmoja aliamua kuacha kuwaza na kuendelea na shughuli nyingine. Lakini wa Aladini aliamua kufanya kitu. Alikwenda shambani na kuchukuwa maboga makubwa matatu na kumwambia mama aende kwa sultani akamtolee posa, na akubali mahari kiasi chochote atakachotajiwa.


Binti sultani alikuwa na uhakika jambo moja kuhusu kijana aliyemuona kule bwawani, alitambuwa kuwa hakuwa katika familia zenye hadi, wadhifa ama utajiri. Binti akaamuwa kuanza kuangalia watu wote watakaokuja kumtembelea baba yake na kujuwa habari zao. Aliamini kama yule kijana aliweza kuja bwawani kumuona bila shaka ataweza kuja kutoa posa kwani anajiamini kwa kiasi kikubwa. Ukweli ni kkuwa hapo mwanzo posa nyingi zilikuja kwa Sulani kumposa binti yae lakini Sultani alikataa. Na si kama Sultani alikataa katakata ila alikuwa akishinikizwa na waziri mkuu wake. Ni kwamba waziri mkuu alikuwa na kijana wake aliamini kuwa ni mtu pekee ambaye angeweza kumuoa binti sultani. Kwa sababu hii alikuwa akimshinikiza Sultani kukataa posa na kumuandalia kijana wake nafasi.


Mama Aladini alivaa mavazi yake ya kawaida aliyoyaona ni mazuri sana. Akachukuwa maboga yake mawili na kwenda nayo kwa sultani. Alikaa kwenye chumba maalumu cha kuzubiria kuongea na Sulatani. Binti Sultani alimuona huyu mama na kuanza kujawa na furaha. Siku ya kwanza mama hakupaa nafasi ya kuonana na sulatani, hali ilikuwa hivyo hivyo siku ya pili na tatu. Aladini aliendelea kulala na kula kwa uchache muda wote huo wa kusubiria hali haikuwa tofauti wa binti sultani. Ukweli ni kuwa moto wa mapenzi ulikuwa ukiwaka mioyoni mwa watu wawili hawa ijapokuwa hawakuweza kuonyesha hisia zao hadharani. Huwenda ni kwa sababu hawaonani ama hawajuani kwa ndani.


Binti sultani alikuwa alishuhudia nmna ambavyo mama yule alivyokuwa akisubiri kuonana na Sultani. Binti akaamuwa kumsaidia henda ni kwa sababu alitaka kujuwa lengo la mama huwenda ndiye mama mkwe wake mtarajiwa. Basi binti akamfuata baba yeke na kumueleza kuwa kuna mwanamke anakuja kila siku katika chumba cha kusubiria, na ana siku ya nne sasa. Sultani aliagiza yule mama aletwe haraka. Mama akaletwa mbele ya sultani na maboga yake mawili. Maboga yaliyo ya njano kwa kukomaa. Binti sutani aliondoka na kujificha ili ambate kusikia kinachoendelea. Mama akazungumza kuwa amekuja kumposea kijana wake. Waziri mkuu alikuwepo kwenye kikao hiko.


Waziri alikasirika sana, yaani unakuja na maboga kuja kumposa binti Sultani. Waziri aliendelea kutoa maneno ya kashfa na uchafuzi. Lengolake ni kutaka kumtengenezea nafasi mwanae. Mfalme akataka kuyashika maboga hayo. Mfalme aligunduwa kuwa sio maboga ya kawaida. Alipoyakamata vyema akagundua kuwa si maboga bali ni dhahabu. Hapo waziri alitahayari sana. Lakini aliendelea kutoa kashifa. Kashifa za waziri zilimuingia Sultani. Waziri akamueleza Sultani kuwa mama huyu apewe muda wa miezi mitatu ya kusubiria maamuzi ya Sultani. Sulatani alikubaliana na uamuzi huo kama kawaida yake.


Loo! Binti Sultani alichoka sana kwa alilosikia. Miezi mitatu ilitosha kwa waziri kumfanyia mipango mwanae. Mama alirudi akiwa na matumaini kuwa ndani ya miezi mitatu ataweza kupata majibu. Mama alimpatia taarifa Aladini kila kilichotokea. Aladini aliendelea kuwa mvumilivu. Katika kipindi hicho waziri mkuu aliweza kutumia muda vyema na kumposea mwanaye binti Sultani. Kwa ushawishi ali nao aliweza kukubaliwa na harusi ikapangwa. Miezi miwili ikapita na siku hiyo sherehe kubwa aikaanza kufanyika ili siku ya tatu harusi ifanyike. Aladini alipozipata taarifa hizo alikimbia nyumbani kuueleza mama kitu.


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 89

Post zifazofanana:-

MAAJABU YA VIUMBE: TEMBO, NYOKA, MBU, SIMBA, CHUI, TAIGA, FARASI, NGAMIA NA WANYAMA WENGINE
Soma Zaidi...

Mapambano ya waislamu dhidi ya Makabila ya kiarabu wakati wa Mtume
Soma Zaidi...

FIKRA POTOFY KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO
Soma Zaidi...

familia
Soma Zaidi...

Masomo ya Afya kwa kiswahili
Makala za afya zilizopata kusomwa zaidi kutoka bongoclass kitengo cha afya Soma Zaidi...

NAMNA YA KUGUNDUA VIDONDA VYA TUMBO
NAMNA YA KUGUNDUA VIDONDA VYA TUMBO Ili kugundua vidonda, daktari wako anaweza kwanza kuchukua historia ya matibabu na kufanya uchunguzi wa mwili. Soma Zaidi...

Dalili za awali za mimba endapo tu mwanamke ametoka kukutana kimwili na mwanaume
Habari! Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WA KWANZA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA KWANZA MTOTO WA MFALME kwanza utambue mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa. Soma Zaidi...

AFYA NA MAGONJWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

SHARTI ZA KUWAJIBIKA KWA ZAKA
Soma Zaidi...

mwanadamu hawezi kuishi bila ya Dini
Soma Zaidi...

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...