UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO


UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO



Bint mfalme akamwambia mama akae kwenye kiti kilichopo pembeni kidogo na kitanda. Kilikuwa ni kiti kikubwa, kizuri kilichotandikwa magotoro yaliyotengenezwa kwa hariri. Kiti kilikuwa na minguu minne yote imetengenezwa kwa madini ya shaba nyekundu. Viigemeo vya kiti kwa kichwani vilitengenezwa kwa dhahabu na kutengeneza umbo zuri mithili ya uwa liliochanua. Vipande vilaini vya hariri vilifunika viegemeo hivyo. Kwa upande wa pembeni viegemeo vya kiti vilitengenezwa kwa vibao vilivyo kunywa vyema ka kuwekewa virungu vilivyotengenezwa kwa lulu. Kwa uzuri wa kiti hiki mama aladini alijisemea kuwa hata kiti cha mfalme hakifikii uzuri huu. Mama aladini aliendelea kufikiri uzuri wa chumba hiki wapi aladini atamuweka mtoto huwu aendane na hadhi yake.


Mama alikaa kwenye kiti na binti mfalme akakaa wenye kitanda. Ijapokuwa ndani kulikuwa na kajikiti kengine kadogo lakini binti huyu hakutaka kukaa kwenye kiti hiko. Hapo mama akapata muda wa kuanza kumthaminsha vyema mkwe wake mtarajiwa. Hakika binti sultani alikuwa ni mzuri. Hakuwa na kichogo, kichwa kilijawa a nywele zilizo shuka mpaka katikati ya mgongo. Wakiwa kwenye mazungumzo mama Aladini aligunduwa kuwa midomo ya binti mfalme imenona vyema, kama ametoka nywa subu ya kongoro. Mama Aladini aliendelea kumthaminisha zadi na kujiridhisha kuwa anafaha zaidi. Binti mfalme hakuwa na macho makubwa ila yalikuwa ni meupe yaliyoonekana vyema, nyusi zilizojipanga na kuchora umbo la mwezi mwandamo. Weusi wa nyusi ulizidi weusi wa nywele zake.


Zilisimama vyema kope zake, na kutengeneza sura iliyoonekana na umbo la duara kama yai la mbuni. Hakuwa na chunusi wala kipele. Binti sultani aligunduwa kuwa mkwe wake anamthaminisha, hapo akatabasamu kidogo. Binti sultani alikuwa anajikubali kuwa na yeye ni katika warembo, ukweli ni kuwa hakujuwa tu ila yeye ni namba moja. Tabasamu la binti mfalme lilimfanya mama aladini afurahi zaidi. Ukimmya ulitawala kwa kuda kidogo kisha binti mfalme akavuja ukimya na kumwambia mama Aladini 'karibu sana mam, kuwa huru, nimekuwa nikiisubiri sana siku kama hii' mama aladini aliridhishwa zaidi na sauti ya mkwe wake. Hakuwa na mikwaruzo, wala ukakasi, ilitoka vyema na kutengeneza mawimbi mazuuri ya sauti yanayoweza kupennya kwene masikio na kuingia ndani yana ya sikio la ndani na kutengeneza maana ya kilichozungumzwa. 'ahsante sana mwanangu, yaani nimefurahi sana, kukuona ukarimu wako, ila uzuri wa chumba hiki umenistaajabisha sana' ni maneno ya mama Aladini kuonyesha mshangao wake.


'ahasante sana mama, chumba hiki nilikipamba hivi huku nikiwa ninamkumbuka mwanao, kwani tulianza kukutana bwawani akiwa amevaa nguo iliy na rangi ya kijivu. Nilivutiwa na nguo yake lakini ndege wa ajabu alitoea mwenye rangi za kupendeza, ndege huyu alinituwa kichwani na kuelekea juu ya mti alipokuwa mwanao, niliamini kuwa ndege huyu hakuwa ni wa kawaida, ni ndege aliyetumwa kutuunganisha. Toka siku hiyo niliamini kuwa mume wangu si mwingine ila ni kijana yule. Sikuwa nimetambuwa jina lake wala wapi anaishi. Ila kwa uwezo wa mungu nikatambuwa baada ya yale yaliyotokea kati ya mimi na mtoto wa waziri. '


Binti mfalme akaendelea kusema 'toka siku ile niliyokutana na mwanao nilianza kukibadili chumba hiki, na kukiweka katika hadthi inayofanana na thamani ya mwanao kwenye moyo wangu. Hata hivyo nahisi hata robo yake sikiweza kuifikia, ndipo nikaamuwa kutengeneza mdori kwa wenye sura ya mwanao nipate kumuona kila siku, kila saa kila wakati. Nilidiriki kutuma mashishushu waje kumchora mwanao bila yeye kugundua. Kama unavyoona mapazia, kitanda na kila unachokiona ni ishara ya upendo wangu kwa Aladini.' binti mfalme alizungumza maeno haya mpaka machozi yakaanza kumtoka. hakika nguvu ya mapenzi haina mfano, mama aladini alikuwa akizidi kushangaa kwa kila anachokion, sikia na shuhudia hapa ndani.


Bunti mfalme akaendelea kusema 'baadaye nikagunduwa kuwa waziri ana njama ya kuniozesha mtoto wake, nililia sana ila machozi yangu hayakuweza kubadili maamuzi ya baba. Nikaamuwa kukipamba chumba hiki na kuweka picha ya ndege yule aliyetukutanisha ili iwe kumbukumbu ya moyo wangu. Amini ninachokwambia kuwa chumba hiki sikupata kumuingiza mtu yeyote ila ni wewe tu. Na huwa nikilala pindi ninapomkumbuka Aladini. Hata baba yangu hatambui uwepo wa chumba hiki katika ikulu hii' mama Aladini alithibitisha uwepo wa nguzu za giza la mapenzi kwa mtoto huyu. 'sikui Aladini amemroga binti wa watu' ni aneno aliyojisemea mama Aladini huku akimkumbatia mkwewe na kumfuta machozi.


Wawili hawa waliendelea kuzungumza hata ukafika muda wa kuondoka. Mama Aladini aliondoka kwenye chumba na kurudi kwa mfalme ili kupata maelekezo nini kitafuata. Mfalme akamueleza kuwa mwambie mwanao ajinadae ijumaa ya wiki ijayo ndi harusi yao. Mama Aladini aliondoka kwa furaha, lakini kwa upande wa waziri hakukuwa hata na tone la furaha, ila majuto, hasira na ukatili ndio vilitawala zaidi. Mama Aladini lifika kwa mwanaye kipenzi na kumpatia habari za furaha. Aladini alifurahi sana. Pia mama Alimueleza kila alichokiona na kugundua yaliyokuwemo kwenye moyo wa binti mfalme. Aladini laifurahi zaidi. Aladini alimuahidi mama yake nitajenga ikulu nzui kuliko ikulu zote duniani, chumba kizuri kuliko nyumba vyote duniani.
Mama aladini alimuangalia mwanaye kwa macho ya ukali na mshangao. Aladini hujatembea popote, hiko chumba kizuri utakijuaje, ukweli ni kuwa Aladini alikusudia baadhi ya aliyoyaona kule kwenye pango yawepo kwenye ikulu yake na mengineyo. Hivyo mambp yakawa kama hivyo na Aladini akaanza kujenga ikulu lake kwa ajili ya mrembo binti mfalme.


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 105

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII SALIH(A.S
Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Ukwaju
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula papai
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 17
5. Soma Zaidi...

anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu
Abali mkuu Nina mdogo wangu anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu na zenye kutisha uume wake nao umekuwa unakama mabaka umebabuka aisee nime angaika Sana kumtibia mpaka nakata tamaa Soma Zaidi...

Maudhui ya Qur-an na Mvuto wa Ujumbe Wake
Soma Zaidi...

Muhtasari wa sifa za waumini
Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s. Soma Zaidi...

(viii)Wenye khushui katika swala
Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Soma Zaidi...

Ulaji wa protini unasaidia kupunguza unene
Soma Zaidi...

BC
Soma Zaidi...

MAANA NA FADHILA ZA DUA
DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Soma Zaidi...

njia ya maandishi
Soma Zaidi...