SIRI YA KIFO INAFICHUKA

SIRI YA KIFO INAFICHUKA


SIRI YA KIFO YAFICHUKA



Kijana akaanza kueleza kuwa huyu binti ni mkewangukabisa na ni mtoto wa mjpomba wangu, na huyo mjomba ni huyu mzee. Mimi na mkewangu tuliiishi vyema sana. Mkewangu alinipenda sana na miaka yote tulioishi sikuweza kumuona na tabia mbaya hata siku moja. Niliweza kuzaa nay watoto watatu. Siku moja alikuwa anaumwa, maradhi haya yali dumu kwa muda uliokaribia mwezi mmoja kisha akapata nafuu kidogo. Haikuchukuwa muda mrfu akaumwa tena baada ya siku kadhaa akapata nafuu tena.


Siku moja alinipa matumaini kuwa kuwa amepata nafuu sana. Sasa akaniambia kuwa ana hamu na tunda epo na hatokwnda kuoga mpaka ale tunda hilo. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mke wangu. Nilikwenda kumtafutia tunda epo popote pale. Nilihangaika sana kwenye mabostani mengi ya mjini. Lakini bila mafanikio. Siku hiyo nilirudi mtupu kwa mke wangu. Loo siku hiyo mke wangu hakwenda kuoga. Basi siku ilofata nikatoka tena kwenda kutafuta tunda epo. Wakati nilipokuwa nimekata tamaa kabisa ya tunda ndipo nikakutana na mze mmoja akanileza kuwa kuna mji matunda hayo yanapatikana. Basi nikafunga safari kulekea huko.


Safari ilinichukuwa siku tatu hata kufika na kurudi na nilinunua matunda matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabi. Cha ajabu niliporudi mke wangu hakuwa tena na hamu ya tunda epo. Lakini alichukuwa matunda yale na kuyaweka kwenye kabati. Siku tatu zikapita bil mke wangu kugusa yale matunda. Basi siku ya nne nilipokuwa mtaani nilikutana na kijana mmoja mtanashati sana akiwa na tunda la epo. Kijana yule nikamuuliza wapi amepata ili nikanunue mengine. Kijana akanieleza kuwa 'nimepewa na mpenzi wangu kama zawadi, mumewe alikwenda mbali safari ya siku tatu kununua maepo matatu kwa thamani ya vipande 15 vya dhahabu. Na mkewe ambaye nimpenzi wangu wa siri akanipatia kama zawadi.


Niliposikia maneno haya nilistaajabu sana na kuvurugwa moyo wangu. Nilitoka mbio hadi kwa mke wangu. Nilipoangalia kabatini nilikuta tunda moja halipo na yamebakia mawili. Nilistaajabu na kuyasadikisha maneno ya yule kijana. Nilimkamata mkewangu na kmchoma kisu cha tumbo kisha nikamchinja na kumkatakata vipande na kuvifunga kama ulivyoona kwenye boksi. Baadaye nilianza kujuta sana na kulia sana.


Kitu cha ajabu siku ya tatu niimkuta mwanagu analia sana. Nilikuwa na uhakika kuwa hatambui kuwa kama mama yake nimemchinja. Basi nikamuuliza mwanangu kipi kinakuliza?. akanieleza kuwa 'naogopa mama akirudi atanipiga, matunda yake matatu nimechukuwa mmoja, nikaenda nalo kucheza. Mkaka mmoja akaninyang'anya na kunipiga, nikamwambia kuwa ni la mama ameletewa na baba kutoka mbali safari ya siku tatu na amenunua kwa thamani ya vipande vitatu vya dhahabu. Yule mkaka akakimbia nalo' basi hapo hapo nikamwambia mwanangu anyamaze.


Dah nikagundua kuwa yule kijana alikuwa ni muongona ndiye chanzo cha kifo cha mke wangu. Niliia sana sanaaaa. Baba mkwe wangu ambaye ni mjomba wangu huyu hapa akaja. Nikamueleza kila kitu naye alilia sana. Hivyo khalifa mimi ndiye niliyemuuwa huyu binti, tafadhal niadhibu mimi niweze kulipa deni la nafsi ya mke wangu. Baada ya kusikia habari hii khalifa akamueleza waziri Mansur. 'Nenda ukanitafutie huyu kijana, ninakupa siku tatu tu, na endapo hutamleta nitakuchinja kama alivyochinjwa huyu binti'.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 94

Post zifazofanana:-

Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...

DUA YA MUUMINI NA DUA YA KAFIRI
DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI. Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

KIFO CHA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SULTAN. Soma Zaidi...

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)
Soma Zaidi...

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran
Soma Zaidi...

Kiapo ya Mtume Ayub na utekelezwaji wake
Mkewe Ayyuub(a. Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI
Soma Zaidi...

Sababu za mdomo kuwa mchungu
Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu. Soma Zaidi...

Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii
Soma Zaidi...

DUA ZA KUONDOA WASIWASI
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Soma Zaidi...

ZIJUE HUKUMU NA FADHILA ZA KUTOA ZAKA KATIKA UISLAMU
Zaka ni nini? Soma Zaidi...