ASUBUHI YA VARANGATI NA KAMARALZAMAN

VARANGATI ASUBUHI; Baada ya kugunduwa kuwa haikuwa ndoto kamaralzamani aliamini kuwa yule ndio mke ambaye baba yake alimchagulia.

ASUBUHI YA VARANGATI NA KAMARALZAMAN

VARANGATI ASUBUHI;
Baada ya kugunduwa kuwa haikuwa ndoto kamaralzamani aliamini kuwa yule ndio mke ambaye baba yake alimchagulia. Hivyo akaenda kwa baba yake moja kwa moja na kumwambia 'baba kuanzia sasa nimekubali kuoa' mfalme alifurahi sana. Furaha yake haikupimika maana hadi sharubu zilipepea vyema. Taarifa hii ilimchukiza sana waziri mkuu ambaye alitaka amuunganishie mwanaye aolewe na Kamaralzamani. Baada ya kitmya kidogo kamaralzamani akaongeza kusema 'nitaoa tu kama utaniletea yule mwanamke niliyemuona jana usiku'


Hapo mfalme alishikwa na butwaa, jana usiku nini kilitokea kwa kamaralzamani. Mfalme ilibidi aulizie kwa walindani wa mlango wa prince. Nao walisema hawakuona mtu yeyote kuingia wala kutoka. Mfalme akadhani mwanae ana shida ya akili sasa. Kamaralzamani kythibitisha kauli yake akamuonyesha baba yake pete ya huyo mwanamke. Hali hizi zililichanganya sana baraza la mawaziri. Wapo waliokubaliana na kamaralzamani na wapo waliomuona sasa anachanganyikiwa.


Kwa upande wa pili kwa princes hali ilikuwa ni varangati.princes amekuwa kama ng'ombe aliyepandisha joto, hashikiki anamtaka mume aliyeletewa na baba yake jana usiku. Nae kuthibitisha kauli yake ni kukosekaana kwa pete yake moja. Princess alikuwa kila anapokwenda, anapolala huwa pete zake mbili anazo. Pete hizi aliachiwa na marehemu mama yake. Sasa leo pete moja kuwa haipo mikononi mwake halikuwa jambo la kawaida. Mfalme akaagiza princess awekwe chini ya ulinzi mkali huwenda akacanganyikiwa.


Kamaralzamani, naye ilibidi aongezewe ulizi. Ila alipewa ruhusa ya kutembea mjini kumtafuta huyo mwanamke kama atamuona. Hapo watu wa mjini nao wakapata kuona sura ya Kamaralzamani kwa mara ya kwanza. Wat walisifia sana uumbaji wa mwenyezi mungu rura ya kamaralzamani. Uzuri wa kamaralzamani ukaanza kuenea sasa nchini kutoka mijini kwenda vijijini. Hali hii pia ilifanywa kwa princess, kwa ulinzi kali aliruhusiwa kutembea mjini kumtafuta huyo mwanaume aliyemuona.


Hapo watu wakaanza kujuwa sura nzuri ya binti mfalme. Sifa na uzuri wa binti mfalme nazo zikazagaa nchini na maeneo ya jirani. Mwezi mmoja sasa umepita bila mafanikio. Mmoja katika mabinamu wa binti mfalme alimfuata binti mfalme na kutaka kujuwa jinsi huyo mwanaume alivyo.binamu huyu aliahidi kuwa atamtafuta hata ikiwezekana atembee dunia nzima hadi ampate. Princess akaanza kueleza sifa za mtu huyo katika sifa nyingi mwisho akaasema amafanana naye. Baada ya mazungumzo haya binamu wa bint mfamle akaahidi kuwa atatimiza ndoto ya binamu wake.


Binamu akaanza kutembea na baada ya kuda wa mwezi na nusu akafika nchini kwa wakina kmaralzamani. Mjini akakuta stori kumuhusu mtoto wa mfalme. Ila stori ile ikawa inafanana na ile ya binamu wake binti mfalme. Kijana ikabidi atafute njia ya kuonana na na mtoto wa mfalme bila mafanikio. Miezi miwili imefika sasa. Kule nyuma mtoto wa mfalme bint nurat akawa kama amechanganyikiwa mpaka mfalme akaagiza waganga waje kumuaguwa. Basi waganga wakawa wanashindana kuja kumuaguwa bila mafanikio. Ikafikia wakati mfalme akatangaza atakayemtibu na kupona binti yake ataozeshwa.


Kwa upande wa binamu wa binti mfalme aliendelea kutafuta juhudi zakuonana na kamaralzamani bila mafanikio. Sik moja akagundua kuwa alipo kamaralzamani kuna mto amabo mto huo unakwenda mnje ya ikulu. Hivyo aka kutumia njia hiyo. Siku hiyo akaogelea kisirisiri hadi akatokea kwenye bostani kubwa. Akajibanza kwenye kisima hadi uingia ndani bila hata ya kuonekana. Alipomuona tu akajuuwa ndie mwenyewe maana sifa zote alizotajiwa na binti mfalme zinafanana.

Kamaralzaman akamuashiria kamaralzamani asipige kelele. Kisha wakaingia ndani zaidi na kuanza kuzungumza. Binamu wa binti mfalme akazungumza kila anachokijuwa kuhusu hali ya dada yke. Kila anapozungumza kamaralzammani alikuwa akitokwa na chozi kwa furaha. Mwisho Kamaralzamani akamkumbatia binamu wa binti Mfalme na kuanza kulia kwa furaha. Kwa uthibitisho akamuonyesha ile pete. Hapo kaka binamu ndipo akaamini kabisa kuwa stori za watu hawa wawili ni za kweli. Lakini nini kilitokea bado ni hadithi nzito.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 86

Post zifazofanana:-

Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake
34. Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu
HADITHI ILIYOSIMULIWA NA TABIBU: Tambua ewe Sultani mwadilifu kuwa mimi nimezaliwa katika familia ya wachamungu waabuduji wanaofata mila za kiyahudi. Soma Zaidi...

Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...

SIMPLE BIOLOGY EXPERIMENT
SIMPLE BIOLOGICAL EXPERIMENTS Experiment One: Measure pulse rate Aim: To measure average pulse rate by using simple method. Soma Zaidi...

SWALA YA MTUME (s.a.w)
SWALA YA MTUME Kumswalia Mtume (s. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 35: Msioneane Choyo, Msizidishiane Bei, Msichukiane
Soma Zaidi...

KATU USITAMANI MAUTI (KIFO) YAANI KUFA, HATA UKIWA NA MARADHI AMA UKIWA MCHAMUNGU UKIWA NI MUOVU MTENDA MADHAMBI MAKUBWA NA MADOGO
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUTI
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME AL-YASA'A(A.S)
Mtume Alyasa'a(a. Soma Zaidi...

PARTS OF MICROSCOPE
MICROSCOPE Microscope this is an instrument used for viewing objects which are too small to be seen by our naked eyes. Soma Zaidi...

ZOEZI
Zoezi la'1 (a) Ainisha maana ya sunnah kilugha na kisheria. Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...