HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli

Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito.

HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli

RAFIKI WA KWELI




Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito. Mfalme aliendelea kumkumbusha waziri Faridi hatimaye akasahau kabisa lile swala. Miezi saba ikapita. Maradhi ya ajabu yakampata waziri faridi na akafariki dunia. Baada ya taratibu za mazishi kukamilika haikupita hata miezi mitatu mama Nurdini akafariki dunia. Loo !!!!! yalikuwa ni maonzi juu ya majonzi kwa Nurdini ambaye siku zote alitegemea baba na mama. Kwa kweli kizuri hata hakidumu kwa muda mrefu. Ukweli ni kuwa mzee Faridi aliishi mika mingi na kula chumvi nyingi. Alifariki akiwa na miaka 81. je kizuri hakidumu kweli?



Nurdini sasa akiwa yaima, akawa ndiye mrithi wa pekee wa mali za baba. Hakuweza kuwafahamu ndugu za baba yake hatammoja. Maisha yaliendelea, aliendelea kula mali za baba bila kuzalisha. Aliendelea kufurahi na mkewe kipenzi. Marafiki zake waliendelea kula na kusaza. Waliendelea kutanua na mengineyo kibao. Kama ilivyo mali bila daftari huisha bila habari, hatimaye mali ya Nurdini ikaendelea kupungua kwa kasi sana. Kweli bandubandu hualiza gogo. Baada ya miezi kadhaa pesa zilimuishia. Nurdini akaanza kuuza Watumwa wote apate pesa ya kutumi,.



Mambo hayakumnyookea, marafiki wakakata mguu kabisa kuonana naye. Akaanza kuuza vitu vya ndani hata vikamwishia na kubakiwa na kitanda na vitu vichavche kwa ajili ya kupikia. Mwishowe akaamuwa kwenda kumuuza mewe ambaye alikuwaga ni mtumwa hapo mwanzo. Hii ni kutokana na ushauri wa mkewe kumuonea huruma mumewe hivyo akamwambia amuuze apate pesa, huwenda akazalisha pesa ya kumkomboa na wakakutana mbele ya safari. Nurdini alimpenda sana mkewe lakin aliamini kuwa ushauri huu ni mzuri.



Alimchukuwa mkewe na kwenda kumuuza kwa pesa ile ambayo baba yake alimnunulia. Waziri Masoud alimuona Nurdini akimuuza mtumwa ambaye anafanana sifa na yule aliyekuwa akitafutwa na baba ake. Hapo aliamini kuwa baba yake alimpatia mwanaye mtumwa wa mfalme. Masoud aliweka oda ya kumnunua yule mtumwa, lakini Nurdini alipotambuwa hili akagoma kumuuza maana aliamini kwa ukorofi wa Masoud asingeweza kumpatia pesa. Ikabakia ugomvi kati ya Masoud na Nurdini. Nurdini wakati huo akamchukuwa mkewe na kumtia kwenye farasi tayari kuondoka mbio.



Masoud alitaka kutumia uwaziri wake lakini alishindwa, kwani Nurdini alikuwa ni mjeuri. Masoud akamvuta shati Nurdini na akaanguka chini yeye na mkewe, tena kwenye matope. Nurdini alimpiga ngumi waziri, ngumi iliyomtoa damu. Kisha akatimua mbio. Waziri bila ya kujifuta damu akaenda kwa mfalme kushitaki. Hiko akaeleza wazi kila ambacho kilitokea kwa yule mtumwa aliyemtaka kuwa bwana faridi alimuozesha mwanaye na sasa mtoto anataka kumuuza.



Mfalme alikasirika sana, na akatangaza aletewe Nurdini popote alipo. Jeshi kubwa liliamuriwa likamchukuwe Nurdini. Katika jeshi lile alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa na ukaribu sana na baba Nurdini, hivyo akaenda mbio kwa Nurdini na kumtaarifu akimbie haraka sana. Nurdini hakuamini anachoambiwa ila akakubali kuamini, hivyo akajiandaa kuondoka yeye na mkewe. Yule askari akampatia nurdini kiasi cha pesa alicho nacho na kuwafanyia mipango ya kupata jahazi dogo la kuondokea kwasiri. Mambo haya yalifanyika kwa siri sana na haikuchukuwa muda Nurdini akaondoka, na mkewe kuelekea Baghadad.





Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 202


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo namba 21
15. Soma Zaidi...

HADITHI YA MKE NA KASUKU
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MKE NA KASUKU. Soma Zaidi...

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s. Soma Zaidi...

ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRI
Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI
Soma Zaidi...

SAFARI SABA 7 ZA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI SABA ZA SINBAD Katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Soma Zaidi...

KISIWA CHA UOKOZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli. Soma Zaidi...

Alif lela u lela: utangulizi
Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Soma Zaidi...

JINI NA MFANYABIASHARA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA. Soma Zaidi...

Utajiri wa Baba na kifo chake
UTAJIRI WA BABA NA KIFO CHAKE. Soma Zaidi...

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...

SAFARI YA TATU YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TATU YA SINBAD Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao. Soma Zaidi...