TAHARUKI YA MFALME WA BAGHADANI

TAHARUKI YA MFALME WA BAGHADANI

TAHARUKI YA MFALME


Basi mfalme na waziri wake wakaenda mpaka kwenye bostani. Loo walikuta na geti lipo wazi. Waakingia bila hata ya tatizo. Walishangaa sana kukuta kuna watu watatu wakiwa katika furaha kubwa sana wakiimba na kunywa. Mfalme na waziri wake wakanyata ili wasionekane na mtu wasijewakavuruga burudani ya watu hawa. Basi wakanyata kwa kufuata miti ya matunda. Mfalme akapanda juu ya mti kuchunguli kupitia kwenye dirisha.



Loo alishangaa sana kumuona mzee ibrahimu akiwa amelewa. Hakika hajapatapo kumuona mzee Ibrahimu akiwa katika hali hii kwa miaka 13 sasa. Basi baada ya kushangaa kwa uda akashuka ili apate kutafakari. Akamwambia waziri wake Jafari panda na wewe ujionee maajabu ya watu hawa. Jaafari alipopanda alishangaa zaidi. Wakaanza kushauriana nini wafanye, ili wapate kujuwa hasa ni kitu gani kimewatokea watu hawa na mzee Ibrahim. Wakaamuwa wakabadili mavazi yao waingie kama watu wasiojulikana ili wapate kufahamu ukweli wamambo.



Wakati wanatafuta cha kufanya, mfalme akamuona kijana mmoja mvuvi aliyejulikana kwa jina la Karim. Mfalme akamwambia waziri amsubiri palepale asiondoke mpaka arudi. Waziri hakufahamu wapi mfalme anakwenda hata hivyo pia hakumuoona yile mvuvi. Karim hana ajualo alipofika karibu na geti akalikuta lipo wazi. Akaingia mule ndani kwa siri ili kavue samaki kwenye kajibwawa ka mfalme kwa siri wakati ule wa usiku.



Alipofika kwenye kibwawa akatupa nyavu yake kisha akaanza kusubiri inase samaki wengi. Kumbe mfalme alikuwa nyuma yake. Alipohakikisha samaki ni wengi akatoa nyavu yake. Loo kugeuka nyuma anamuona mfalme. Alijitupa chini ya muguu kuomba msamaha. Mfalme akamsamehe kisha wakabadilishana mavazi. Mfalme akachukuwa samaki wawili na kumuachia akarimu aondoke na samaki wake. Mflme akiwa katika mavazi ya Karim alirudi akiwa na samaki wake mpaka alipo Waziri wake. Akamsalimia, kwa hakika waziri alijuwa anaongea na Karimu. Loo kumbe alikuwa ni mfalme. Hapo mfalme akasema 'kama wewe ambaye hujalewa umeshindwa kunijuwa vipi Ibrahim ambaye amelewa atanijuwa.



Basi mfalme akamwambia tena waziri wake amsubiri palepale asiondoke. Sasa mfalme akijifanya ni mvuvi akagonga hodo kwenye lile geti kwa sauti ya juu akijifananisha na Karim. Mzee Ibrahim akauliza nani wewe. Akajibu mfalme ni mimi karim, nimekuletea samaki. Sasa mzee ibrahi anafahamiana na Karim na huwa wanauziana samaki. Kijana Nurdin aliposikia samaki uchu ukamtoka. Akamlazimisha mzee aagize samaki aletewe. Wakaltwa samaki ila yule mrembo alipowaona ni wazima kwenye ndoo ya maji akaomba akaangiwe kwanza.



Mzee Ibrahimu bila ya kuelewa akamuagiza mvuvi akawakaange kisha aje nao. Mfalme akatoka hadi alipo waziri wake. Kisha akamueleza kuwa ameambiwa awakaange. Waziri akataka kulifanya yeye jukumu lake, ila mfalme akakataa alitaka kutimiza amri kama mvuri. Hivyo akaagiza aletewe kila kitu kinachohusika katika kukaanga mpaka chumvi. Alipoletewa aliwakaanga vyema sana kwa umakini mkubwa kisha akawapelekea kwa Mzee Ibrahim. Nurdini alifurahi sana na akampatia mvuvi kiasi kikubwa cha dhahabu ambapo ni mara 100 ya malipo halisi ya samaki wale.



Mfalme akiwa katika umbo la mvuvi alishukuru sana. Yule mtumwa (mke wa Nurdini) alifurahi zaidi na akaanza kuimba tena na kupiga gitaa. Mfalme alifurahi sana na kuonyesha furaha yake dhahiri. Bila ya kujuwa hili wala lile Nurdini akamwambia 'mvuvi wewe ni mkarimu sana, umeleta samaki na ukawakaanga, ilaonyesha umependezwa sana na mtumwa wangu huyu. Kuanzia sasa nakupatia iwe kama zawadi yako. An-neese aliposikia maneno hayo alilalamika sana kwa kutumia mashairi, alionyesha dhahiri kuwa hakupenda uamuzi ule, hakupenda kutengena na Nurdini wake. Mfalme ilibidi aulize hasa nini kimetokea kati yao ama ana deni?

Kufikia hapo Nurdini akaanza kuhadithi kila ambacho kilichotokea. Kutoka baba yake akiwa karibu na Mfalme mpaka kununuliwa mtuwa. Kifo cha baba yake hata kukimbiwa na marafiki. Mwisho mpaka anakuja Baghadad na kukutana na mzee Ibrahimu. Mfalme akiwa anasikiliza maneno haya alikuwa akivijwa na machozi. Hakika yalukuwa ni maeneno yenye kutia huruma na simanzi.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 175


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo
learn English Vocabulary Soma Zaidi...

NDOTO YA MGONJWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 12
8. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...

BINTI WA NDOTONI
Download kitabu Hiki Bofya hapa BINTI WA NDOTONI. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Kiapo Cha Mfalme
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran
Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 03: Mtumwa wa Gharama
Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi. Soma Zaidi...

Kuangamizwa Firauni na Majeshi Yake
Soma Zaidi...

kamaralzamani
HADITHI YA CAMARALZAMANI PRINCE PEKEE Inapata mwendo wa safari ya siku 4 kwa farasi kutokea nchi ya Peshia alikuwepo mfalme maarufu sana aliyefahamika kwa jina la Shahzaman. Soma Zaidi...

KWENYE BOSTANI LA MFALME WA
KATIKA BOSTANI LA KIFALME BAGHADADBasi Nurdini na mke wake bila hata ya kujuwa wapi watafikia waliingia kwenye mashua na kuwasili Baghada wakati wa jioni. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MFANYABIASHARA NA JINI
Soma Zaidi...