NURDINI ANARUDI KWAO NA BARUA YA MFALME WA BAGHADAD

Hadithi za Alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya nane

NURDINI ANARUDI KWAO NA BARUA YA MFALME WA BAGHADAD

NURDINI ANARUDI KWAO NA BARUA YA MFALME WA BAGHADAD
Baada ya mfalme kusikiliza hadithi ile akiwa katika mavzi ya mvuvi. Aliwaaga vyema bila hata ya wao kujuwa kuwa huyu ndie mfalme wa hap ana mmilikiwa hili bustani. Baada ya mfalme kuondoka haukupita muda watatu hawa wakalala fofofo. Mfalme kwa upande wake hakupata usingizi kabisa kutokana na yale aliyoyasikia kutoka kwa kijana Nurdini. Ilipofika asubuhi Mfalme akaagiza aletwe mzee Ibrahim una wageni wake mapema kabisa kabla hata hawajaamka.



Basi askari wakatoka muda uleule, walipofika kule loo bado watatu wale wamelala fofofo. Askari wakawaamsha na kuwachukuwa hadi kwa mfalme. Mzee Ibrahim una vijana wake walishikwa na taharuki kubwa sana. Walijuwa kuwa siri yao leo imefichuka. Kijana Nurdini alianza kujuta na kuanza kutubia madhambi yake kwa mungu, maana alijuwa kuwa itakuwa ile sehemu waliolala sio ya kawaida. Mzee Ibrahimu alianza kuwahadithia vijana wake huku wakiwa wanaburuzwa na askari.



Vija wangu tambueni kuwa hii bostani sio mali yangu ni ya mfalme wa Baghadad. Na bila shaka alipata habari ya jambo lililotokea jana. Nisameheni sana vijana wangu kwa kutokuwaambia na kuwasababishia matatizo haya. Nurdini hakujali alijuwa kuwa kila kwenye uzito kutakuwa na wepesi tu. Mrembo mtumwa yeye aliendelea kubalia kimya bila hata ya kutia neno huku akiendelea kufuta machozi yake na ya mume wake Nurdini.



Mbele ya mfalme wakawekwa wakisubiria kitakachojiri. "mzee Ibrahimu na vijana wake wamesha wasili Mfalme" ilikuwa ni kauli ya Jafari akimpa ishara mfalme kuwa wageni wake wameshafika tayari. Mfamel kwa bashasha na tabasamu aliwakaribishwa vyema sana. Hali hii iliwashangaza watu wote pale ndani, inakuweje wafanyaji makosa wanakaribishwa hivi?. Ukweli ni kuwa hata mfalme alifurahia sana siku ya jana. Mfalme akaanza kuelezea yeye kila ambacho kilitokea siku ya jana na namna ambvyo aliazima mavari kwakarimu na kuyavaa. Pia alielezea namna ambavyo aliguswa na tukio la Nurdin.



Mwisho mzee Ibrahimu akaomba msamaha kwa tabia ambayo aliionyesha jana. Nurdini na mkewa wakafuata kuomba radhi. Mfalme alizidi kufurahi zaidi. Kisha aka uuliza Nurdini "je ungependa kuishi hapa ama kurudi kwwenu?" Nurdini baada ya kusita kidogo akauliza "kwani ipo nji aya mimi kurudi bila ya matatizo?" ndio ipo wala hakuna shida, ila itabidi umuache mkeo hapa kwanza. Nurdini alikubaliana na wazo hili. Kwa upande wa binti yeye hata hakupenda kuachwa na Nurdini hata kwa muda mchache.



Kisha mfalme akamkabidhi barua Nurdini na kumwambia "chukuwa barua hii kampe mfalme wa nchini kwako kisha usubirie majibu ila uusiisome barua hii hadi unamkabidhi". Nurdini alimtegemea Mungu maana hakuwa na uhakika kama barua ile ni ya kumuokoa ama ya kumuuza. Siku ya pili aliangana na mke wake na kuanza safari ya klurejea nchini kwao.



Akiwa yeye na farasi yake, huku amechomeka kabendera kadogo ka nchi ya Baghadad. Bendera hii ilikuwa ikimtambulisha kuwa yeye ni mjumbe kutoka mchi husika. Kiendera hiki kingeweza kumlinda asikamatwe mpaka kufika mbele ya mfalme. Na hii ndio maana ya kusema kuwa mjumbe hauwawi. Basi Nurdini hatimaye akawa mbele ya mfalme na kumpatia barua mabyo hata yeye hakujuwa ni nini kimeandikwa humo ndani.



Mfalme alipoisoma tu barua mdomo ukaanza kumtetemeka, hatimaye sura akaikunja kama aliyekula ndimu iliyowekwa kwenye kifuu cha mbata ya mnazi kitamli. Macho yalimtoka hata waziri wake wakaanza kumshangaa. Mfalme alionekana kuishiwa nguvu kabisha na akaondoka ghafla na barua yake mkononi. Alimuangalia sana Nurdini wakati anaondoka. Mawazir wasijuwe ni nini kimetokea pale.



Punde tu baada ya mfalme kutoka waziri Masoud alimng'olea macho Nurdini, kisha akakumbuka kilichotokea na jinsi alivyomdhalilisha mbele za watu. Kisha akaunganisha na barua aliyokuja nayo aliyompataharuki mfalme. Basi waziri Masoudi akaamrisha Nurdini afungwe gerezani. Bila ya kujuwa kinachoendelea ama nininkimo kwenye barua masoud alifanya maamuzi ya kukurupuka sana. Ni siku tatu zimepita toka Nurdini aondoke Baghadad.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 138


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

Utajiri wa Baba na kifo chake
UTAJIRI WA BABA NA KIFO CHAKE. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 18
21. Soma Zaidi...

SABABU YA NENO LAKO
Sababu ya neno lako, nasema nimesikia,Sababu ya neno lako, nasema hongera pia,Sababu ya neno lako, nishajua yakonia,Wasema afukuzwae, sihadi pasemwe toka,Sababu ya neno lako, maumivu yanijia,Sababu ya neno lako, nami leo nakwambia,Sababu ya neno lako, sit Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 24
13. Soma Zaidi...

JIFUNZE DINI YA KIISLAMU, quran, hadithi, tawhid, tajwid, sira na fiqh
Jifunze mengi kuhusu dini hapa Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU(A.S.): Ndoto ya nabii Yusufu
Mtume Yusufu(a. Soma Zaidi...

Siku ya sita ya wageni
SIKU YA SITA YA WAGENI Siku ya sita walianza mapema kama siku ya nne kisha wakamueleza baba awapeleke msituni. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 03
Tatua mzozo wa NI NANI MUUAJI? Soma Zaidi...

Kitabu Cha mashairi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Ndoa ya siri
NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Soma Zaidi...