picha

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah.

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

SURAT AL-FIIL
Sura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Sura hii imeshuka ili kueleza kuhusu tukio la kuangamizwa kwa jeshi la tembo. Na hii ni katika sura ambazo zinataja neema ambazo wamepewa Maquraysh, nao ni ule ushindi dhidi ya Makafiri walotaka kuvunja Al-Kaโ€™abah. Tukio hili limeelezwa kwa kirefu kwenye vitabu vya Sirah na hapa nitaleta kwa ufupi zaidi



Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-kaโ€™aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)



Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.



Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo Sanโ€™a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.



Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.



Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-kaโ€™aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 1626

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    ๐Ÿ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰3 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰4 web hosting    ๐Ÿ‘‰5 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN

ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.

Soma Zaidi...
Adabu za kusikiliza quran

ADABU ZA KUSIKILIZA QURANI 1.

Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al adiyat

Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah.

Soma Zaidi...
Viraa saba na herufi saba katika usomaji wa quran

Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa surat Dhuha

Sura hii imetermka Makkah na ina aya 11. Sura hii ni moja ya sura ambazo zimeshuka mwanzoni wakati ambapo Mtume ameanza kazi ya utume.

Soma Zaidi...
Saratul-asr 103

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...