picha

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)

SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)

Sababu za kushuka surat an-Nasr (idhaa jaa)

SURATUN-NASR
Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.a.w) hupo maka wakati wa hija ya mwisho, hija ya kuaga. Sura hii matika mashafu imewekwa katika sura za Madina kwa sababu imeshuka wakati mtume ameshafanya hijira kwenda madina.



Sura hii inaitwa ya Madina kwa kuwa ilishuka baada ya Mtume kuhama ingawa iliposhuka ilikuwa ni katika Makka wakati Mtume alipokwenda kufanya Haji ya mwisho. Sura hii imekuja kutabiri kifo cha Mtume (s.a.w).



Kutokana na mapokezi ya hadithi sura hii ndiyo sura ya mwisho kushuka katika quran ila sio aya ya mwisho kushuka. Sura hii ilishuka kwenye masiku ya tashriq katika mwezi wa dhul-hija. Baada ya kushuka sura hii Mtume (s.a.w) ndipo akahutubia waumini.


Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu.



Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.

Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu



Na Ushindi mkubwa uliotajwa hapa ni ushindi wa Makka ilipoingia katika mamlaka ya Waislamu, mwaka wa 8 wa Hijra, na mwaka uliofuata ikawa makundi-makundi ya makabila ya Waarabu yanakuja ingia Uislamu. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotimiza bishara Zake za ajabu; na Mtume s.a.w. anaambiwa aombe ghofira kwa ajili ya makundi hayo yatakayoingia Uislamu maana kazi ya kusimamisha sheria ilikuwa kubwa. Seyidna Abu Bakar iliposhuka sura hii alilia. Watu wakamwuliza mbona unalia? Akajibu, Kazi ya Mtume s.a.w. sasa imekwisha na Atatutoka.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views 3417

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 ai web app     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)

(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.

Soma Zaidi...
Nini maana ya Quran

Post hii inakwenda kukuambia maana ya Quran

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
quran tahadhari

TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.

Soma Zaidi...