Fadhila za surat al-fatiha na sababu za kushuka kwake

1.

Fadhila za surat al-fatiha na sababu za kushuka kwake

Fadhila za surat al-Fatiha

1.SURAT AL-FATIHA.
Muhadithina wengi wanaeleza ya kuwa sura hii nzima ilishuka Makka, na toka mwanzo ilikuwa ni sehemu ya maombi ya Waislamu. Hii ndiyo sura iliyotajwa katika aya ya Qur'an, Na kwa yakini Tumekwisha kupa (Aya) saba zisomwazo mara kwa mara na Qur'an kubwa (sura 15:88), ambayo ilishuka Makka. Habari zingine zinaeleza ya kuwa sura hii iliteremshwa tena mara ya pili, Madina. Sura hii ilishuka mapema tu Mtume s.a.w. alipoanza kazi.



MAJINA YA SURA HII NA MAANA YAO.
Jina maarufu la sura hii ni Faatihat-ul-Kitaab (Inayofungua Kitabu) (Tirmidhi na Muslim). Baadaye jina hilo lilifupishwa kuwa Surat-ul-Faatihah, au Al-Faatiha. Sura hii imepewa majina mengi, na haya kumi ndiyo yaliyo sahihi zaidi: Al-Faatiha, As-Salaat (Sala), Al-Hamdu (Sifa njema), Ummul-Qur'aan (Mama ya Qur'an), Al-Qur'aan-ul-Adhiim (Qur'an Kubwa) As-Sab'ul-Mathaani (Aya saba zinazosomwa mara kwa mara), Ummul-Kitaab (Mama ya Kitabu), Ash-Shifaa (Ponyo), Ar-Ruqya (Kago), Al-Kanz (Hazina).

Maulamaa wa elimu za Qurani hawakutoa zaidi ufafanuzi wa sababu ya kushuka kwa sura hii. Au jambo hili halikuwashughulisha kabisa.



FADHILA ZA SURA HII

Amesimulia Ibn 'Abas kuwa 'wakati ambao jibril alikuwa amekaa na Mtume akasikia sauti ya mlango uliofunguliwa juu yake akanyanyu kichwa chake kisha akasema 'hiyo ni nsauti ya mlango uliopo mbinguni umefunguliwa siku ya leo, na katu haujawahi kufunguliwa ila ni leo tu (ndio mara ya kwanza kufunguliwa). Basi akashuka Malaika kutoka kwenye mlango huu akasema (Jibril) huyu ni malaika ameshuka duniani na hajawahi kushuka kamwe ila ni leo tu akatoa salamu (malaika huyo) kisha akasema (kumwambia mtume) tuo habari za furaha kwa nuru mbili ulizopewa na hakuwahi kupewa mtume yeyote kabla yako kamwe (ambazo ni) surat al-fatiha na aya za mwisho za surat al-baqarah hatusoma herufi yeyote isipokuwa utapewa' (amepokea Muslim). Amesema Mtume 'surat al-fatiha ni dawa ya kila gonjwa' amepokea Bayhaqiy)



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 255

Post zifazofanana:-

Kitabu cha Afya 02
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Soma Zaidi...

Fahamu vitamini A na kazi zake, vyakula vya vitamini A na athari za upungufu wake
Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Soma Zaidi...

nikiasi gani chaprotini kinachohitajika mwilini kwa siku kwa mtumzima
Soma Zaidi...

Zoezi 2:2
Soma Zaidi...

WAQFU WAL-IBTIDAAI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

jamii
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

VYANZO VYA VYAKULA VYA VITAMINI NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

kitabu cha afya
'J'5'M' C'~'q'Q' ('xb'[['n'('&B'? Soma Zaidi...

NINI VIDONDA VYA TUMBO?
Ni vidonda vinavyotokea katika ukuta wa tumbo. Vidonda hivi tumezoea kuviita vidonda vya tumbo ila hapa nitataja kitaalamu kuwa vidonda hivi hufahamika kama peptic ulcers. Soma Zaidi...

Ijuwe Dua ya Ayyuub(a.s)
Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Je! inajuzu wanawake kuzuru makaburi?
As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, nauliza inajuzu wanawake kuzuru makaburi? Soma Zaidi...