Post hii inahusu zaidi dalili za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ingawa sio watu wote wenye dalili kama hizi Wana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo Ila zikitokea mtu anapaswa
1. Maumivu makali wakati wa kujamiiana.
Kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo bakteria tayari wameshambulia sehemu mbalimbali kwenye kibofu Cha mkojo na sehemu zinazozunguka kama vile via vya uzazi kwa hiyo wakati wa kujamiiana mtu anapata maumivu hali hii uwatokea hasa watu wale ambao maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo yanapokuwa yamesambaa sana na yamekaa mda mrefu.kwa hiyo tunapaswa kuhakikisha kuwa tunaangalia afya zetu mara kwa mara Ili kuepusha matatizo makubwa yanayoweza kujitokeza.
2.Mtu mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo anasikia maumivu wakati wa kukojoa.
Hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa bakteria ambao uingia kwenye kibofu Cha mkojo na kusababisha maambukizi na pengine kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe na uharibifu wowote ambao umeshafanyika kwenye kibofu Cha mkojo kwa hiyo wakati wa kukojoa mkojo ugusa sehemu ya majeraha na kusababisha maumivu wakati wa kukojoa kwa hiyo basi baada ya kujua hayo yote tunapaswa kutumia madawa ambayo yanatibu ugonjwa huu kwa sababu yapo na wengi wamepona na tusiyameze bila ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.
3. Kuwepo kwa damu kwenye mkojo.
Hali hii utokea kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na Maambukizi hayo yamekuwa makubwa zaidi na kusababisha kuvuja damu kwenye sehemu mbalimbali za kibofu Cha mkojo ndio maana mkojo utoka n damu au uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo inakuwa unavuja damu ndo maana mkojo utoka pamoja na damu, hali hii sio nzuri inaweza kuleta madhara makubwa zaidi kwa hiyo mgonjwa anapaswa kuwaona wataalamu wa afya kwa msaada zaidi kwa sababu magonjwa haya yanatibika na dawa zipo hospitalini.
4. Maumivu makali kwenye Tumbo la chini.
Kwa wakati mwingine Kunakuwepo na maumivu kwenye sehemu ya tumbo la chini , hali hii usababishwa na Maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo ambapo kibofu Cha mkojo kinakuwa kimeshambuliwa na bakteria ambapo maumivu huwa mengi kwenye tumbo la chini.
5. Mkojo kutoa harufu mbaya.
Watu wenye matatizo ya uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, mkojo wao utoa harufu mbaya hali hii ni kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo ambayo usababisha harufu ya mkojo kubadilika na kuwa mbaya kwa hiyo pengine mkojo unaweza kuwa na usaha ambao usababisha mkojo kutoa harufu mbaya. Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi mgonjwa inabidi kwenda hospitalini kwa matibabu zaidi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2420
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Aina za minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya aina za minyoo Soma Zaidi...
Dalili za Kuvimbiwa kwa watoto
Posti hii inazungumzia kuhusiana Kuvimbiwa kwa watoto ni tatizo la kawaida.Kuvimbiwa kwa watoto mara nyingi kuna sifa ya kupata haja kubwa mara kwa mara au kinyesi kigumu, kikavu. Sababu mbalimbali zinaweza kusababisha kuvimbiwa kwa watoto.Sababu za kawa Soma Zaidi...
MALARIA INATOKEAJE? (Namna ambavyo malaria inatokea, inaanza na inavyoathiri afya)
Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi. Soma Zaidi...
Ugonjwa wa kuchelewa kuganda kwa Damu unaojulikana Kama hemophilia.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na tatizo la Kurithi ambapo Damu inatoka kwa muda mrefu wakati au baada ya jeraha bila kuganda. Soma Zaidi...
Dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanawake
Somo hili linakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanawake Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...
NINI SABABU YA VIDONDA VYA TUMBO
NENO LA AWALI Hapa utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu vidonda vyatumbo. Soma Zaidi...
Fahamu Ugonjwa unaosababisha madhara kwenye mapafu
Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa yanayosababisha madhara kwenye mapafu na kitaalamu hujulikana Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu Soma Zaidi...
Dalili za macho makavu.
Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo. Soma Zaidi...
Je dalili za kisonono au gonoria kwa mwanamke huonekana baada ya mda gani
Soma Zaidi...
Vyakula hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo Soma Zaidi...
Dalilili za kukosa oksijeni
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalilili za kukosa oksijeni ambalo kitaalamu hujulikana Kama apnea.kukosa oksijeni ni tatizo ambapo kupumua kwako hukoma na kuanza unapolala. Soma Zaidi...