Dalili za uvimbe kwenye kizazi

Posti hii inahusu zaidi Dalili za uvimbe kwenye kizazi,hizi ni Dalili ambazo ujitokeza kwa akina mama ambao wana uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo endapo mama ameona Dalili kama hizi anapaswa kuwahi hospitali mara moja kwa uangalizi zaidi.

Dalili za uvimbe kwenye kizazi.

1. Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.

Hii ni Dalili mojawapo ambayo inaweza kujitokeza kwa Mama au msichana ambaye hajaolewa, ikitokea damu ikaongezeka kupita kiasi kusiko kwa kawaida wakati wa hedhi ni Dalili mojawapo ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.

 

2. Maumivu makali wakati wa hedhi.

Kwa wakati mwingine maumivu yanaweza kuwa makali kuliko kawaida au mtu mwingine anakuwa hana maumivu wakati wa hedhi ila ikitokea shida hizi ya kuwepo kwa uvimbe maumivu yanaanza kuwepo.

 

3. Kuvimba miguu.

Nayo ni Dalili ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi utaona mama au mdada yeyote amevimba miguu kwa hiyo anapaswa kwenda hospitalini kupima.

 

4. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Kwa wenye matatizo ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi wanapatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa na kwa hiyo huwa hawana furaha wakati wa tendo ila ni maumivu tu.

 

5. Kuwepo kwa gesi tumboni .

Au kwa wakati mwingine mtu ujisikia kama amevimbiwa na tumbo linakaa limevimba kama vile linakuwa na gesi.

 

6. Kupata choo kigumu au kufunga choo kabisa .

Kwa kawaida mtu mwenye matatizo ya kuwepo kwa uvimbe huwa na matatizo ya kukosa choo na huko anakuwa anakula chakula kawaida na kwa wakati mwingine anahisi kwenda haja kubwa ila choo kigumu nakuwa kama kigumu sana.

 

7. Maumivu n kwenye mgongo.

Hili tatizo uwapata wanawake walio wengi na udhani ni mgongo inauma lakini baada ya kufanyiwa upasuaji na kutoa uvimbe kwenye kizazi maumivu haya hayatokeagi tena.

 

8. Maumivu kwenye miguu na miguu kuvimba.

Kwa wakati mwingine Maumivu yanakiwepo kwenye miguu na miguu uanza kuvimba .

 

9. Kuwepo kwa ugumba au uzazi wa shida.

Kwa wakati mwingine wa mama wengi wanaangalia kutafuta watoto na hawapati shida kubwa inakuwa kwenye kizazi na wakifanyiwa upasuaji wanaweza kupata watoto.

 

10. Maumivu kwenye nyonga.

Kwa wakati mwingine mama huwa anapata maumivu makali kwenye nyonga ambayo umfanya mama kulalamika kila wakati.

 

11.mimba kutoka mara kwa mara.

Ikitokea mama kabeba mimba, hizo mimba utoka mara kwa mara na wakati mwingine mama anaweza kuangaika mpaka pale atakappgundua tatizo.

 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/07/Monday - 12:34:51 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1288

Post zifazofanana:-

Tofauti kati ya Quran na vitabu vingine vya mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Dalilili za kidole tumbo (appendicitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa Kidole ambao kitaalamu hujulikana Kama Appendicitis. Kidole tumbo husababisha maumivu kwenye tumbo la chini la kulia. Hata hivyo, kwa watu wengi, maumivu huanza karibu na kitovu na kisha kusonga. Kadiri uvi Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyeng'atwa na nyuki
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko Soma Zaidi...

Assalam Baada yakufariki wazazi wake mtume alilelewa nanani???
Mtume Muhammad s.a.w amezaliwa yatima asiyena baba. Lakini hii haikumfanya asipate maelezo bora yaliyo mazuri. Je unajuwa aliyemlea baada ya kufariki kwa mama yake?. Soma Zaidi...

Dawa ya Rifampicin na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi Dawa ya Rifampicin na kazi zake, hii ni dawa mojawapo inayotibu kifua kikuu kati ya Dawa zilizoteuliwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu. Soma Zaidi...

Namna ya kujikinga na VVU/UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza namna mbalimbali za kujikinga na VVU/UKIMWI Soma Zaidi...

Sababu za Kutokwa Damu moja kwa moja bila kuganda (hemophilia).
Posti hii inaelezea kuhusiana na Damu kutokuganda ambalo hujulikana Kama Hemophilia, ni ugonjwa nadra ambapo damu yako haigandi kawaida kwa sababu haina protini za kutosha za kuganda. Ikiwa una tatizo la Damu kutokuganda, unaweza kuvuja damu kwa muda mre Soma Zaidi...

Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

Faida za minyoo
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za minyoo Soma Zaidi...

Umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu.pua ni mlango wa fahamu ambao uhusika na kupumua. Soma Zaidi...

Kukosa choo
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kukosa choo Soma Zaidi...

Dalili za Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu cha mtoto mdogo, kwa kawaida kitovu cha mtoto kama kiko vizuri kinapona kwa mda mchache na kinakauka mapema iwezekanavyo bila kuwa na tatizo lolote ila kama kuna Dal Soma Zaidi...