Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi
Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi.
UTARATIBU NA DUA YA KUZURU MAKABURI
Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi. Ni katika matendo yanayotukumbusha kifo. Hata mtume allikuwa akienda kuzuru makaburi mara kadhaa. Hata mwishoni mwa siku za mwisho za uhai wake alikwenda kuzuru makaburi na kuwaaga waliokufa na kuwaombea dua.
Hapo mwanzo wanawake walikatazwa kuzuru makaburi kwa maneno ya Mtume aliposema “wamelaaniwa wanawake wenye kuzuru makaburi”. lakini baadaye mtume akawaruhusu wanawake kuzuru makaburi. Kwa ufupi ibada hii ni kwa waislamu wote na haina siku maalumu ama wakati maalumu. Kwani Mtume alikuwa anakwenda kuzuru makaburi hadi wakati wa usiku.
Kuzuru makaburi sio lakima uwe na udhu. Unaweza kuzuru hata ukiwa hupo twahara. Ukifika kwanza unaanza kusalimia (kutoa salamu) kisha unaomba dua pia ukiwa makaburini unaweza kulimia ama kusafishai kaburi ama makaburi. Ama kujazia udongo haya yote sio ya lazima. Kisha utaomba dua
Dua ya kuzuru kaburi
لسَّلامُ عَلَـيْكُمْ أَهْلَ الدِّيارِ مِنَ المؤْمِنيـنَ وَالْمُسْلِمينَ، وَإِنّا إِنْ شاءَ اللهُ بِكُـمْ لاحِقُـونَ، (وَيَرْحَمُ اللَّهُ الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّا وَالْمُسْتَأْخِرِينَ) أَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمْ العَـافِيَةَ.
Assalaamu ’alaykum ahlad-diyaar minal Mu-uminiyna wal Muslimiyn, wainnaa In Shaa Allaahu bikum laahiquwn. (Wa yarhamu-Allaahu al-mustaqdimiyna minnaa wal musta-akhiriyna). As-alu-Allaaha lanaa walakumul-’aafiyah
Amani ishuke juu yenu watu wa nyumba za Waumini na Waislamu, nasi apendapo Allaah tutakutana nanyi (Na Allaah Awarehemu wa mwanzo na wa mwisho). Namuomba Allaah Atupe sisi nanyi Al-’Aafiyah
al-hidaayah.com
Mwenye kuzuru makaburi anaruhusiwa kwenda akiwa peke yake ama akiwa na wenzie. Halikadhalika hakuna mavazi ya rangi maalumu wakati wa kuzuru ama kuzika. Hakuna haja ya kunyoa nywele wana kuandaa vyakula. Hairuusiwi kuyataja mabaya ya aliuyefariki ama kukaa juu ya kaburi. Pia hairuhusiwi kuzungumza mabo maovu maeneo ya makaburi.
Kwa hakika kuzuru makaburi ni ibada inayotaka utulivu wa nafsi. Kwani inatakikana moyo upate mawaidha kutokana na kutembelea kaburi. Mwenye kuzuru kaburi apate athari ya kuyaogopa mauti ili apate kufanya maandalizi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu.
Soma Zaidi...Ndoa ya mke zaidi ya mmoja katika uislamu na taratibu zake, faida zake na namna ya kuitekeleza
- Je, Ukeweza, (ndoa ya mke zaidi ya mmoja) humdhalilisha mwanamke?
Soma Zaidi...Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Swala ya ijumaa, nguzo zake, sharti zake na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...