Madai ya Makafiri Dhidi ya Qur’an na Udhaifu Wake

i.

Madai ya Makafiri Dhidi ya Qur'an na Udhaifu Wake

Madai ya Makafiri Dhidi ya Qur'an na Udhaifu Wake

i. Dai kuwa Qur'an ni mashairi aliyotunga Muhammad (s.a.w)

- Maquraishi wa Makka walidai kuwa Qur'an ni mashairi aliyotunga

Muhammad kwa ujuzi na ueledi mkubwa wa historia ya Waarabu.



Udhaifu wa dai hili:

- Ujumbe wa Qur'an unatofautiana sana na ule wa mashairi kimvuto na taathira kama mshairi mashuhuri Labiib Ibn Rabiah alikiri hilo.




ii. Dai kuwa Qur'an ni zao la njozi za Mtume (s.a.w) zilizovurugika

- Waandishi kama akina Anderson na Watt walidai kuwa Qur'an ni zao la

mawazo na dhana tu za Muhammad zilizovurugika.



Udhaifu wa dai hili:

- Dhana hizi hazina ukweli wowote kwa sababu haijawahi kutokea katika historia ya mwanaadamu kuuunda kitabu kwa ndoto mithili ya Qur'an. Rejea Qur'an (21:5)


iii. Dai kuwa Qur'an ni zao la mwenye kifafa na aliyepagawa na shetani

- Baadhi ya waandishi wa kikafiri wamedai bila ushahidi wowote kuwa

Mtume Muhammad (s.a.w) alitunga Qur'an akiwa katika hali ya kifafa.



Udhaifu wa dai hili:

- Dai hili halina ukweli wowote kwani haijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu mtu mwenye kifafa kuunda Kitabu chenye wafuasi wengi. Rejea Qur'an (10:38)



iv. Dai kuwa Qur'an ni aya za shetani

- Salman Rushdie alidai kuwa Muhammad hakushukiwa na wahyi wowote

isipokuwa ni mawazo yake akiongozwa na shetani katika kuandika Qur'an.



Udhaifu wa dai hili:

- Qur'an yenyewe inadhihirisha kuwa si aya za shetani, na kama ingelikuwa

ni aya za shetani kwa nini adhhirishe uadui wake kwa wanaadamu?

Rejea Qur'an (81:25), (6:112), (35:6), (17:88), (4:82)



v. Dai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliandika Qur'an kwa msaada wa Mayahudi na Wakristo

- Makafiri wanadai kuwa Mtume (s.a.w) aliandika Qur'an kwa kunakili

mafundisho ya Biblia kutokana na baadhi ya aya kufanana.



- Pia wanadai kuwa alifundishwa na Ujumbe wa Qur'an alipokutana na Padri

Bahirah katika safari yake ya Shamu akiwa na miaka 12.



Udhaifu wa madai haya:

- Mtume Muhammad (s.a.w) hakujua kusoma wala kuandika na alisema

Qur'an inatoka kwa Allah (s.w) vinginevyo ingelikuwa na hitilafu nyingi.



- Nakala ya kwanza ya Agano la Kale iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiarabu ilipatikana miaka 200 baada ya kutawafu (kufa) Mtume (s.a.w).


- Mtume (s.a.w) alikutana na Padri Bahirah akiwa na miaka 12, sio jambo rahisi kufundishwa ujumbe muda huo na aje kuufundisha baada ya miaka
28.

Rejea Qur'an (16:103)



vi. Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur'an ili kuleta umoja na ukombozi wa

Waarabu

- Wako baadhi ya Makafiri wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga

Qur'an ili awaunganishe na kuwakomboa Waarabu.



Udhai wa dai hili:

- Dai hilo sio la kweli kwa sababu hakuna msisitizo wowote ndani ya Qur'an juu ya ukombozi na umoja wa Waarabu na Qur'an inapingana na ukabila.


- Pia Mtume (s.a.w) angelikubali pendekezo la Maquraishi kuwa kiongozi wa

Waarabu ili atumie fursa hiyo kujenga umoja wa Waarabu.

Rejea Qur'an (3:42)



vii. Dai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur'an ili kurekebisha tabia za

Waarabu.

- Wapo Makafiri wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur'an ili

kujenga mwenendo na tabia nzuri za ndugu zake Waarabu.



Udhaifu wa dai hili:

- Kujenga tabia na mwenendo mzuri wa watu ni jambo zuri ambalo halihiajii kutumia udanganyifu au uongo wa aina yeyote.
Rejea Qur'an (6:93), (5:101)



viii. Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur'an ili ajinufaishe kiuchumi.

- Baadhi ya watu wanadai kuwa Muhammad (s.a.w) kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi.


Udhaifu wa dai hili:

- Kama Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur'an kujinufaisha kiuchumi mbona

hali yake kiuchumi ilizidi kuwa duni hata baada ya Utume.

Rejea Qur'an (33:28-29)



ix. Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur'an ili kuwania madaraka na ukubwa

- Makafiri wamedai pia kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur'an ili kujipatia

madaraka na ukubwa kwa Waarabu.



Udhaifu wa dai hili:

- Mtume Muhammad (s.a.w) ni mtu aliyejulikana sana ulimwenguni, hivyo

hakuwa na haja ya kutumia Qur'an kuomba madaraka.



- Mtume (s.a.w) mwenyewe alikataa ofa ya kuwa kiongozi wa Waarabu walipomtaka ili aache kazi ya kulingania Uislamu.
Rejea Qur'an (9:61), (45:9), (28:86), (18:110), (6:50)



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 380

Post zifazofanana:-

tamaa
33. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA IDGHAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Kitabu Cha Dua 120
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu maumivu ya jino
Utaijuwa Dawa ya maumivu ya jino, sababu za maumivu ya jino na njia za kujikinga na maumivu ya jino Soma Zaidi...

Dua Sehemu ya 02
Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA
SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina i'rab ( '). Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani
(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu. Soma Zaidi...

Uanzishwaji wa Makundi mbalimbali ya Harakati za Kuhuisha Uislamu Ulimwenguni
8. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Nazi
Soma Zaidi...

QURAN: TAJWID, FADHIKA ZA KUSOMA QURAN, FADHILA ZA KUSIKILIZA QURAN, FAIDA ZA SURAT FATIHA, YASIN, BAQARA, TABARAK
Soma Zaidi...

Vinywaji salama kwa mwenye kisukari
Vijuwe vinywaji salama kwa mgonjwa wa kisukari Soma Zaidi...

Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri
18. Soma Zaidi...