Namna ya kuswali swala ya maiti: nguzo zake, sunnah zake na maandalizi juu ya maiti

3.

Namna ya kuswali swala ya maiti: nguzo zake, sunnah zake na maandalizi juu ya maiti

Namna ya kuiswali sala ya maiti

3. Kumswalia Maiti.

Masharti ya Swala ya Maiti.
- Kwa wenye kumswalia maiti, watekeleze masharti ya kawaida ya swala.
- Masharti ya maiti anayeswaliwa:
1. Maiti awe muislamu
2. Maiti iwe imeoshwa na kukafiniwa
3. Maiti iwekwe mbele ya wanaoisalia.


- Inajuzu kusalia maiti iliyo masafa ya mbali (swala ya ghaibu).
- Maiti zikiwa nyingi zipangwe mbele, za kiume zikiwa karibu na imamu kisha kusaliwa zote kwa pamoja.
oMaiti isiwe ya shihidi.
- Kwa mujibu ya Hadith ya Mtume (s.a.w), mashahidi hawaoshwi wala kusaliwa.



Nguzo za Swala ya maiti.
- Swala ya maiti inaswaliwa wima; haina rukuu, sijda wala kikao.
- Nguzo za swala ya maiti ni;
i.Nia
ii.Takbira ya kuhirimia
iii.Kusoma Suratul-Faatiha.
iv.Takbira ya Pili.
v.Kumswalia Mtume (s.a.w) kama tufanyavyo kwenye Tahiyyatu.
vi.Takbira ya Tatu.
vii.Kumuombea dua maiti.
viii.Takbira ya Nne.
ix.Kuombea dua waislamu wote, kisha kutoa Salaam.



Namna ya kutekeleza swala ya Maiti hatua kwa hatua.
Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo;
a)Maiti iwekwe mbele.
b)Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti ikiwa maiti ni ya kike, na usawa wa mabega kama maiti ni ya kiume.
c)Maamuma watasimama kwenye mistari (safu) kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, n.k.
d)Baada ya hapo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
i.Nia - ambayo ni kukusudia moyoni.
ii.Kuleta takbira ya kwanza; kwa kusema, 'Allaah Akbar'
iii.Imamu na maamuma watasoma suratul-Faatiha ' kimya kimya.
iv.Imamu ataleta Takbira ya Pili kisha maamuma ' kimya kimya kwa maamuma na si lazima kuinua mikono wao.
v.Kumswalia Mtume (s.a.w) kama ilivyo katika Tahiyyatu, wote ' kimya kimya.
vi.Imamu ataleta takbira ya Tatu kisha maamuma- kama walivyofanya awali.
vii.Wote kumuombea maiti dua kimya kimya, ikiwemo:


'Allaahumma ghfir lihayyinaa wamaayyitinaa washaahidinaa waghaaibinaa waswaaghirinaa wakaabirinaa wadhakirnaa waunthaanaa. Allaahumma man ahyaytahuu minnaa faahyi 'alal Islaam. Waman tawaffaytahuu minnaa tawaffahuu 'alal Imaani. Allaahumma laa tahirimnaa ajirahuu walaa taftinaa ba'adahuu'


Tafsiri:
'Ewe Allah tusamehe sisi, na maiti wetu, na mashahidi, na wasiokuwepo miongoni wetu, vijana wadogo miongoni mwetu na wakubwa miongoni mwetu, wanamume wetu, na wanawake wetu. Ewe Allah, yeyote yule miongoni mwetu utakayemewezesha kuishi, mjaalie aishi katika Kiislamu na yeyote miongoni mwetu utakayemfisha, mfishe katika Imani (ya Kiislamu). Ewe Allah, usitukatishe ujira kutoka kwake na wala usitufitinishe baada yake.'



- Au kwa kifupi tuweza kumuombea maiti kama ifuatavyo;
'Allaahumma ghfir lahuu warhamhuu wa-afihii wa-afu-anhu'
Tafsiri:
'Ewe Allah, Mghufirilie na Umrehemu'.



viii.Imamu ataleta Takbira ya nne na maamuma kufuatihia kama awali.
ix.Wote watawaombea waislamu dua ' (pia si lazima kuleta dua hii).
Rejea Qur'an (59:10).



x.Imamu kutoa salaam na maamuma kufuatishia bila kutoa sauti kama ilivyo kwenye swala ya kawaida kwa kusema;
'Assalaamu 'alaykum Warahmatullaah (Wabarakaatuh)'
Tafsiri:
'Amani iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake'.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 722

Post zifazofanana:-

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
2. Soma Zaidi...

English tenses test 001
Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Faida za kula Nanasi
Nanasi ni katika matunda matamu lakini mazuri pia kiafya, je unazijuwa faida zake kiafya Soma Zaidi...

Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces
Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis. Soma Zaidi...

DARSA: FIQH, SUNNAH, HADITHI, QURAN, SIRA, TAFSIRI YA QURAN, VISA VYA MITUME NA MASAHABA
1. Soma Zaidi...

Uanzishwaji wa Makundi mbalimbali ya Harakati za Kuhuisha Uislamu Ulimwenguni
8. Soma Zaidi...

Hija ya kuaga kwa mtume, na hutuba ya mwisho aliyotowa mtume katika hija
Mwaka mmoja baada ya msafara wa Tabuuk Bara Arab zima ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Soma Zaidi...

Maana ya talaka na kuacha ama kuachwa
Maana ya TalakaTalaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili. Soma Zaidi...

Ndoa ya mke zaidi ya mmoja na taratibu zake
Soma Zaidi...

HUU NDIO USIA WA MTUME KWA WAISLAMU
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '. Soma Zaidi...

Sifa na vigezo vya dini sahihi
1. Soma Zaidi...