picha

Dawa ya fangasi uumeni

kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka

Dawa ya fangasi uumeni

Dawa ya fangasi uumeni
Fangasi wanaweza kuathiri watu wa marika yeto, pia kuathiri maeneo mengi ya mwili. Lakini hapa nitakuletea fangasi wanaoathiri uume, sababu zao, dalili zao na dawa inayotumika kutibu fangasi hawa wa kwenye uume.



Dalili za fangasi wa kwenye uume
1.Upele na ukurutu kwenye uume
2.Vidoadoa vyeupe kwenye uume
3.Uume kuwa na umajimaji kwenye ngozi yake
4.Kwa ambao hawajatahiriwa kutakuwa na uchafu mweume kwenye ngozi ya govi
5.Miwasho kwenye uume na kuhisi kuunguwa



Nini sababu ya fangasi hawa wa kwenye uume?
Fangasi wa kwenye uume husababishwa na aina ya fangasi inayojulikana kama candida. fangasi hawa wanapenda sana maeneo yenye majimaji. Hususan sehemu za siri ambapo ndipo panakuwa na majimaji mengi. Fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kupitia ngono. Usafi wa sehemu za siri ukawa ni mbovu hali inaweza kuwa mbaya zaidi.



Watu walio hatarini kupata fangasi wa uumeni
1.Watu walio na Uchafu wa mwili hasa sehemu za siri
2.Watu walio na kisukari
3.Watu wenye viribatumbo (kitambi)
4.Watu wenye kinga dhaifu kama waathirika wa VVU ama walioanza matibabu ya saratani
5.Watu ambao hawajatahiriwa



Dawa zinazotumika kutibu fangasi wa uumeni
Fangasi hawa wanaweza tu kutibiwa kwa dawa za fangasi za kupaka yaani za losheni kama:-
1.Miconazole (lotrimin AF, Ceruex, Desenex, Ting Antifungal)
2.Imidazole (canesten, Selezen)
3.Clotrimazole (Lotrimin AF, Anti-Fungal, Cruex, Desenex, Lotrimin AF Ringworm)



Pia endapo hali itaendelea, mgonjwa anaweza kutumia dawa za kumeza, baada ya kupata ushauri kwa daktari. Dawa hizi ni kama:-
1.Fluconazole (Diflucan) hii ni ya kumeza pia hutumika pamoja na ya kupaka inayoitwa hydrocortisone cream. Tiba hii hasa ni kwa wale ambao hali imekuwa mbaya sana (balanitis).



TIBA MBADALA ZA KUTIBU FANGASI WA UUMENI
1.Mafuta ya majani ya chai
2.Kitunguu thaumu
3.Siki ya epo
4.Mafuta ya nazi
5.Mafuta ya karafuu



Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi, ama tuachie maoni yako hapo chini.





                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views 16871

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 web hosting     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Fahamu dawa za kutibu mafua

Post hii inahusu dawa za kutibu mafua ambazo ni cough seppessants na nasal congestion ni dawa ambazo zimependekezwa kwa ajili ya kutibu mafua.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya ALU au kwa lugha nyingine ni dawa ya mseto

Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida.

Soma Zaidi...
IJUE DAWA YA AMOXLINE (antibiotic) NA MATUMIZI YAKE

Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya kutuliza mishutuko.

Post hii inahusu zaidi dawa ya phenytoin,ni dawa inayotuliza mishutuko mbalimbali inayoweza kutokea kwenye mwili na kutokana na mishutuko hiyo tunaweza kupata kifafa.

Soma Zaidi...
Fahamu Dawa inayotumika kupunguza maumivu (ibuprofen)

Ibuprofen ni mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana duniani kote! Ili kupunguza maumivu na kuvimba, agiza Ibuprofen leo na upate afya bora! Ni kiungo amilifu katika dawa za jina kama vile Motrin na zaidi. Ibuprofen pia inaweza kuuzwa kama: Advil Motrin,

Soma Zaidi...
Ijue Dawa ya lignocaine

Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.

Soma Zaidi...