image

Fahamu kuhusu vitamini D na kazi zake mwilini

Hapa utajifunza kuusu vitamini D, kazi zake, upungufu wake na chanzo cha kupata vitamini D.

 

VITAMINI D NA FAIDA ZAKE MWILINI

Vitamini D ni vitamini inayosaidia miili yetu iweze kuvyonza madini ya calcium, magnesium na phosphate. Vitamini D hutengenezwa chini ya ngozi kwa kutumia mwanga wa jua. Vitamini D ipo katika makundi makuu mawili nayo ni vitamini D2 na vitamini D3. Vitamini vipo katiaka makundi mengi kuna vitamini A, BC, D, E na K . katika makala hii tutakwenda kuona zaidi kuhusu vitamini D, namna ambavyo vitamini D hutengenezwa mwilini, Je ni zipi kazi za vitamini D, na upungufu wake unasababisha athari gani mwilini?.


 

YALIYOMO:
1.Maana ya vitamini D
2.Makundi ya vitamini D
3.Kazi za vitamini D
4.Chanzo cha votamini D
5.Upungufu wa vitamini D


 

Maana ya Vitamini D
Vitamini D ni matika fat soluble vitamin ambayo imetokana compound za cholesterol. Vitamini D vimegunduliwa mwaka 1922 na Mwanasayansi anayefahamika kwa jina Elmer McCollum. Historia ya uchunguzi huu wa vitamini D ulianzia toka mwaka 1914 wakati Elmer McCollum na Marguerite Davis walipogundua vitamini A


 

Vitamini hivi vimeitwa D kwa sababu ndio vitamini vya nne kugundulika toka A, B, C na sasa ni vitamini D. ugunduzi wa vitamini D ulianzia kwenye mbwa mgonjwa ambaye alikuwa ana matege. Baadaye ikajulikana kuwa mbwa aliweza kupona matege kwa sababu ya chembechembe amazo baadaye ndiyo zikaitwa vitamini D.


 

Makundi ya vitamini D
Kama ilivyokuwa vitamini K na vitamini B zina makundi mengi. Basi hata hivyo vitamini D vimegawanyika katika makundi kadhaa, makuu katika kundi hilo ni vitamini D2 na bitamini D3. makundi haya mawili kwa pamoja ndiyo hufahamka kama vitamini D.


 

Vitamini D1 na vitamini D2 kwa pamoja pia huitwa calciferol. Vitamini D2 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwa ka 1931 na vitamini D3 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwaka 1935.


 

Kazi za vitamini D
Katika miili yetu vitamini D ina kazi kuu ya kufanya metabolism ya madini ya calcium. Kwa lugha nyepesi ni kuhakikisha kuwa unyonzwaji wa madini ya chumvi ambayo ni calcium, magnesium na phosphate unafanyika vyema ndani ya utumbo mdogo.


 

Faida za vitamini D:
1.Husaidia kufyonza mwili kufuonza madini ya calcium
2.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
3.Husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani
4.Husaidia kuboresha mfumo wa faya
5.Kupunguza uzito na kitambi


 

Chanzo cha vitamini D
Chanzo kikuu cha vitamini D ni mwanga wa jua ambao husaidia katika utengenezwaji wa vitamini D chini ya ngozi. Kama mtu hataweza kupata mwangaza wa jua vyema kuna uwezekano wa kupata upungufu wa vitamini D.


 

Pia tunaweza kupata vitamini D kutoka katika vyakula na mboga, kama vile:-
1.Uyoga
2.Yai lililopikwa
3.Maini
4.Samaki


 

Upungufu wa vitamini D
Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha athari kubwa kwenye afya. Miongoni mwa athari hizo ni:-
1.Matege
2.Udhaifu wa mifupa
3.Mifupa kuvunjika kwa urahisi

 

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1474


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Fahamu kuhusu vitamini K na kazi zake mwilini
vitamini k ni moja katika vitamini vinavyoitajika sana mwilini. Je unazijuwa athari za upungufu wa vitamini k mwilini? Soma Zaidi...

Hatari ya uzito mkubwa
Posti hii inahusu zaidi hatari zilizopo kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa sababu ya kuwepo kwa uzito mkubwa na pia unene usio wa kawaida usababisha mtu kuwa na matatizo mbalimbali hasa saratani za kila sehemu kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Kazi za vitamin B na makundi yake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take Soma Zaidi...

Vifaa vya kutumia wakati wa kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi vifaa vya kutumia wakati wa kusafisha vidonda, ni vifaa muhimu ambavyo mara nyingi kutwa hospitalini. Soma Zaidi...

Umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu.pua ni mlango wa fahamu ambao uhusika na kupumua. Soma Zaidi...

Kazi ya madini mwilini
Posti hii inakwenda kukueleza kuhusu kazi za madini mwilini Soma Zaidi...

Njia za kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya njia za kuongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...

Utaratibu wa lishe kwa vijana
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa vijana Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEANGUKA KIFAFA
Kifafa kinaweza kumpata mtu muda wowte. Soma Zaidi...

Kumsaidia mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote machoni
Posti hii inahusu hasa jinsi uchafu, wadudu na vitu vingine vinavyoweza kuingia machoni.macho ni mojawapo ya milango mitano ya fahamu ambapo kazi yake ni kuona. Soma Zaidi...

Nini husababisha kizunguzungu?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu vitamini C na kazi zake
Makala hii itakujulisha kazi kuu za vitamini C mwilini. Hapa pia utatambuwa ni kwa nini tunahitaji vitamini C na wapi tutavipata Soma Zaidi...