picha

Kupanga uzazi na uzazi wa mpango katika uislamu

Kupanga uzazi na uzazi wa mpango katika uislamu

Kupanga Uzazi katika Uislamu



Kama ilivyo haramishwa kwa jamii, Uislamu umeharamisha pia kudhibiti uzazi kwa mtu binafsi kwa khofu ya kushindwa kuwalisha au visingizio vingine. Hata hivyo Uislamu haujawataka watu wazae kiholela. Kwanza umekataza watu kuzaana nje ya ndoa. Pili, walioona wanatakiwa wazingatie umri baina ya mtoto na mtoto mwingine. Kwa anayetaka kukamilisha muda wa kunyonyesha, basi amnyonyeshe mtoto wake kwa miaka mwili:


Na wanawake waliozaa wawanyonye.she watoto wao miaka miwili kainilz kwa anayetaka lwkamilisha lwnyonyesha..." (2:233)



Kunyonyesha humsababisha mama mzazi kuchukua muda mkubwa kabla ya kuingia tena katika siku zake. Iwapo mwanamke atapata siku zake wakati mtoto yungali mchanga (hajafikia umri wa miaka miwili), anatakiwa ajizuie asipate mimba; kwani katika Hadith iliyosimuliwa na Imamu Muslim, Mtume (s.a.w) amesema kuwa mwanamke akipata mimba wakati yungali na mtoto mchanga, afya ya mtoto hudhurika. Njia za kuzuia mimba katika kipindi hiki cha kunyonyesha ni zile ambazo hazina madhara ya kiafya kwa baba wala mama. Katika Hadith iliyopokelewa na Bukhari na Muslim, Jabir (r.a) amesema kuwa wakati wa Mtume (s.a.w) wao walikuwa wanatumia njia ya kuzuia mimba inayoitwa 'azal" (with drawal au coitus interuptus), yaani njia ya kumwaga mbegu za uzazi nje lakini Mtume (s.a.w) hakuikataza.



Hapa ifahamike kwamba suala Ia kupanga juu ya muda wa kunyonya mtoto linamhusu baba na mama na si suala Ia kuwekewa sera na taifa; kwani hali za watu zinatafautiana.



Ama kwa mama atakayekuwa na matatizo ya kiafya, ikathibiti kuwa akibeba mimba atadhurika au kuhatarisha maisha yake, anaruhusiwa kufunga kizazi hata kutoa mimba ambayo imeshatunga.



Hitimisho juu ya Kudhibiti uzazi
Tumeona kuwa kuongezeka kwa watu si tatizo kwani hakuna tatizo Ia riziki kama wale wasiomtegemea Allah (s.w) wanavyodai. Hivyo, kuwapangia watu wazae watoto idadi Fulani ni kinyume kabisa na mafundisho ya Uislamu. Wajibu wa mwanadamu ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, na pia kuweka utaratibu mzuri wa mgao wa rasilimali katika jamii.



Uislamu umekemea vikali zinaa na kuweka adhabu kali kwa wazinifu. Sera ya kudhibiti uzazi na Elimu ya ngono (sex education) ni nyenzo "nzuri sana na madhubuti" za kupalilia zinaa katika jamii. Katu waislamu hawatazikaribisha. Huu ndio msimamo wa Uislamu juu ya suala Ia kudhibiti uzazi na waislamu wa kweli daima watakuwa katika msimamo huu kwani:


Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume, hakika amepotea upotofu ulio wazi kabisa. (33:36)





                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2123

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Wanaowajibika kuhijji

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada

Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudiย kumfanya Mtume (s.

Soma Zaidi...
Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu

Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa

Kutawadha ni katika ibada muhimu za mwanzo kutakiwa kuzijuwa na ni lazima. Swala yako haitaweza kutimia bila ya kujuwa udhu. Inakupasa kujuwa nguzo za udhu, yanayoharibu udhu na namna ya kutawadha kifasaha. Hapa utajifunza hatuwa za kutawadha

Soma Zaidi...
Taratibu za kumuona mchumba katika uislamu

Hspa utajifunza taratibu za kuonana na mchumba katika uislamu.

Soma Zaidi...
Mafungu ya urithi katika uislamu

Hspa utajifunza viwango maalumu vya kutithi mirathi ys kiislamu.

Soma Zaidi...