Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii

Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii

Wajibu wa Watoto kwa Wazazi



Wajibu wa watoto kwa wazazi wao ni kuwatii katika kiwango cha hali ya juu, kuwaheshimu na kuwahurumia hasa wanapokuwa wazee. Kuwatii wazazi ni kitendo kinachochukua nafasi ya juu sana katika Uislamu. Utii kwa wazazi huchukuwa nafasi baada tu ya Kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Msisitizo wa kuwatii wazazi, kuwaonea huruma na kuwafanyia ihsani uko wazi katika Qur-an:


Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee pamoja nawe, au wote wawili, usiwaambie hata A/i! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa heshima kabisa. Na uwainamishie bawa ?a unyenyekevu kwa (kuwaonea) huruma na useme: 'Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto ". (17:23-24).



Wazazi, hasa mama, wamestahiki kutiiwa kwa kiwango cha hali ya juu, kuwafanyia ihsani na kuhurumiwa na watoto wao hasa wanapokuwa wazee, iii iwe kama malipo ya kazi ngumu ya kuwalea watoto wao. Mtoto hana malipo ya kumlipa mzazi wake kwa kumzaa na kumlea mpaka kufikia utu uzima wake. Malipo anayotakiwa na Mwenyezi Mungu (s.w)


awalipe wazazi wake kwa taabu zote walizochukua katika kumlea ni kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w) na wazazi wake kwa kumtii Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume na kisha kuwatii wazazi wake, kuwafanyia ihsani na kuwahurumia kama tunavyojifunza katika Qur-an:


Na tumemuusia mwanaadamu (kuwafanyia ihsani) wazazi wake - mama yake amechukua mimba yake kwa udhafujuu ya udhafu na kumnyonyesha katika kipindi cha miaka miwili - (tumemuusia) ya kwamba unishukuru Mimi na wazazi wako, marejeo yenu ni kwangu. (31:14)


Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake,.Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu. Na ku be ha mimba yake hata kumwachisha ziwa, (uchache wake) ni miezi thelathini (46:15). Pia mtoto mwema, pamoja na kuwatii na kuwahurumia wazazi wake kwa kuwapa kila msaada wanaohitajia, huwaombea dua wakiwa hai au wakiwa wametangulia kufa kwa kusema:


Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili na wanaoamini Siku ya Hisabu. (14:41). Utii kwa wazazi unatakiwa uendelezwe hata baada ya kufa kwao kama tunavyojifunza katika hadithi: Abu Usaydi as-Said (r.a) amesimulia: Tulikuwa karibu na Mtume (s.a.w) wakati alpomjia mtu wa ukoo wa Salimah na kumuuliza: Ee Mtume wa mwenyezi Mungu! Kuna utii


mwingine uliobakia kwa wazazi baada ya kutawafu kwao? "Ndio" alUibu Mtume. "Kuwaombea dua, kuwaombea msamaha na maghfira kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kutekeleza wasia wao, kuwa na uhusiano mwema na wale mliofahamiana kutokana na wao na kuwaheshimu rafiki zao ". (Abu Daud, Ibn Majah)



Pia katika hadithi iliyosimuliwa na Ibn Umar mtume (s.a.w) amesema:
Utii wa hali ya juu kwa wazazi ni mtu kufanya urafiki na marafiki wa baba yake baada ya kufa kwake. (Muslim).
Hata hivyo, kiwango cha utii na huruma ya mtoto kwa wazazi wawili kinatofautiana. Mama anastahiki kupata nafasi ya kwanza ndio baba afuatie kama tunavyojifunza katika hadithi:



Abu Hurairah amesimulia kuwa mtu mmoja aliuliza: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni nani hasa anayestahiki upendo wangu wa hali ya juu? 'Mama yako ", alijibu Mtume. Kisha akauliza tena: Nani anayefuatia? "Mama yako ", alijibu Mtume. Akauliza tena: Nani anayefuatia? 'Mama yako ' alj/ibu Mtume. Katika maelezo mengine al/ibu Mtume: Mama yako, kisha mama yako, kisha mama yako, kisha baba yako, kisha jamaa zako wa karibu, (Bukhari na Muslim).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 286

Post zifazofanana:-

surat al mauun
SURATUL-MAM'UUN Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yat.. Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

Faida za kula Faida za kula buluu beri
4. Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Uislamu unakataza mtu kulaani hovyo
20. Soma Zaidi...

Kukaa itiqaf na sheria zake hasa katika mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

NECTA FORM YWO GEOGRAPHY PAST PAPERS
Soma Zaidi...

Utekwaji wa Misri na Gavana Muawiya
Soma Zaidi...

mfano mtu ametoka kusex, jana alafu Leo akikojoa mkojo una muhuma na Wa mwisho unatoka damu, itakuwa ugonjwa gani eti,
Soma Zaidi...

Kitabu cha Afya 04
Afya inaweza kuathiriwa na vitu vingi sana. Hapa tutaendelea kuona mabo zaidi yanayoathiri afya yako. Soma Zaidi...

Mapambano ya waislamu dhidi ya Makabila ya kiarabu wakati wa Mtume
Soma Zaidi...

FAIDA ZA MATUNDA NA MBOGA MBALIMBALI KWA AFYA
FAIDA ZA MATUNDA Makala hii inakwenda kukuletea faida za matunda mbalimbali na mboga upatikanaji wake na faida zake kiafya. Soma Zaidi...