Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh.
Kuingizwa au Kutolewa Eda
Katika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh. Kizuka huanza eda baada tu ya kufariki mumewe na eda yake huisha mara tu baada ya muda wa miezi mine na siku kumi kuisha. Wala hapana vazi maalum Ia kukalia eda. Si nguo nyeupe, wala nyeusi, wala kuvaa matambara kama baadhi ya watu wanavyoitakidi. Mwanamke mfiwa atabakia nyumbani kwa mumewe au kwa warithi wa mumewe katika sitara kama kawaida anavyotakiwa awe mwanamke yeyote wa Kiislamu na ataendelea kufanya shughuli zake za nyumbani na nje ya nyumbani zilizo katika mipaka ya sheria ya Kiislamu. Wala hapana sheria yoyote ya kukaa nyumbani kivivu-vivu kama wanavyoitakidi watu wengine.
Hekima kubwa ya kuamrishwa kizuka kukaa eda, pamoja na haja ya kuangaliwa uwezekano wa kuachwa na mimba, kunampa kizuka nafasi ya kutulizana na kuliwazika baada ya kupatwa na msiba mkubwa kiasi hicho. Pamoja na kuwa mwanamke baada ya kipindi cha eda huwa huru kutoka nyumbani kwa mumewe marehemu na kuolewa na mume mwingine, akitaka kubakia katika nyumba ya mumewe pamoja na watoto wake, ana haki kisheria kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
Na wale waliofishwa miongoni mwenu na wakawacha wake, wawausie (warithi wao) kwa ajili ya wake zao kupata matumizi ya mwaka mmoja bila ya kutolewa (katika nyumba za waume zao). Na kama wanawake wenyewe wakiondoka, basi si kosa juu yenu kwa yale waliyoyafanya kwa nafsi zao
wenyewe yanayofuata sharia. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye hi/dma. (2:240).
Katika baadhi ya jamii za kijahili pamekuwa na mtindo wa kuwarithi wanawake waliofiwa na waume zao kama mali inavyorithiwa na jamaa wa marehemu. labia hii ya kumdhalilisha mwanamke na kumnyima uhuru wake wa kuolewa na mwanamume ampendaye imepigwa marufuku katika sheria ya Kiislamu kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
Enyi mlioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa jeuri. Wala msiwazulie (kuolewa na waume wengine) iii mpate kuwanyang 'anya baadhi ya vile mlivyowapa (katika urithi wa waume zao...) (4:19)
Ama mwanamke mjane mwenyewe akiridhika kuolewa na ndugu au jamaa wa marehemu mumewe, ili aweze kubakia pale na watoto wake hapana ubaya ili mradi tu wafunge ndoa kama ilivyo katika sheria.
Umeionaje Makala hii.. ?
Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako.
Soma Zaidi...Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo?
Soma Zaidi...Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu, kusimamisha swala za Sunnah (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...