Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai
Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa.
Talaka Kabla ya Jimai:
Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa. Mwanamume atatoa talaka na mkewe ataachika hapo hapo bila ya kukaa eda. Kama mwanamume ameshatoa mahari hatadai chochote kama yeye ndiye aliyeamua kumuacha mkewe bali atalazimika kumpa kiliwazo (kitoka nyumba). Ikiwa hajatoa mahari atalazimika kutoa nusu ya mahari. Kama mke ndiye aliyedai talaka atalazimika kumrudishia mumewe mahari aliyompa. Hukumu ya talaka ya ama hii inabainika katika aya zifuatazo:
Si dhambi kwenu kama mkiwapa wanawake talaka ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari (yao). Lakini wapeni cha kuwaliwaza (kitoka nyumba); mwenye wasaa kadiri awezavyo, na mwenye dhiki kadiri awezavyo. Matumizi hayo (wanayopewa) yawe kama inavyosema Sharia. Ndio wajibu kwa wafanyao mema. (2:236)
Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa na mmekwisha wawekea hayo mahari (basi (wapeni) nusu ya hayo mahari mliyoagana, isipokuwa wanawake wenyewe waache (wasitake kitu), au yule (mume) ambaye kifungo cha ndoa ki mikononi mwake aache (haki yake kwa kumpa mahari kamili). Na kuachiana ndiyo kunakomkurubisha mtu sana na kumcha Mungu. Wala msisahau kufanyiana ihsani baina yenu; hakika Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyafanya. (2:237)
Talaka ya Aliyerukwa na akili na aliyetenzwa nguvu
Talaka si jambo Ia kulifanyia maskhara Muislamu anatakiwa awe hadhiri wakati wa kutoa talaka. Ahakikishe kuwa wakati anaamua kutoa talaka akili yake iko katika hali ya utulivu. Talaka ya aliyerukwa na akili haiswihi kama tunavyojifunza katika Hadith:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kila talaka ni halali isipokuwa talaka ya punguani na mwenye kurukwa na akili". (Tirmidh).
Pia mtu akilazimishwa kutoa talaka pasina sababu za kisheria au mume na mke wakitalakishwa kwa nguvu huku bado wanapendana katika mipaka ya Allah (s.w), talaka hiyo haitaswihi kama tunavyojifunza katika Hadithi:
Aysha (r.a) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allah akisema: "Hakuna talaka wala hakuna kumwacha huru mtumwa kwa nguvu ". (Tirmidh).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 ai web app 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Funga za Sunnah na namna ya kuzitekeleza
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Taratibu za mirathi katika zama za ujahilia
Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi.
Soma Zaidi...Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya Jamii
(c) Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya JamiiKimaumbile wanaadam kama walivyo wanyama, wamejaaliwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kati ya mume na mke ili kuwawezesha kutekeleza wajibu mkubwa wa kuzaana na kuendeleza kizazi.
Soma Zaidi...Je ni zipi nguzo za uislamu, na ni ngapi nguzo za uislamu?
Post hii itakujuza maana ya uislamu na nguzo zake.
Soma Zaidi...