Eda ya kufiwa na hukumu zake
Eda ya Kufiwa
Eda ni kipindi cha kungojelea mwanamke baada ya kupewa talaka au baada ya kufiwa na mumewe. Katika kipindi cha eda ni haramu mwanamke kuolewa na mume mwingine. Ambapo tumejifunza kuwa eda ya kuachwa inaisha baada ya twahara tatu au miezi mitatu (kwa wale wasiopata hedhi) au baada ya kujifungua (kwa mke aliyeachwa), eda ya kuachwa inachukua miezi minne na siku kumi au siku mia moja thelathini (130).
Hukumu ya Eda ya kufiwa inabainishwa katika Qur-an:
Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na kuacha wake; hawa (wake) wangoje (wasiolewe) miezi mine na siku kumi. Na wanapofikia muda wao (wa kumaliza eda yao hiyo), basi si dhambi juu yenu kwa yale wanayoyafanyia nafsi zao (hao wanawake) kwa yanayowafiki (kufuata) Sharia. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. Wala Si dhambi kwenu katika kupeleka habari ya posa kwa ishara tu (Si kwa maneno) kuwaoa wake (walio edani), wala (hapana dhambi pia) katika kutia katika nyoyo zenu azma (za kuwaoa) Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka.
Lakini msifunge nao ahadi kwa Sifl (ya kuwaoa maadam eda haijesha) isipokuwa mseme maneno yaliyo mazuri. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda uliyoandikwa (katika eda) ufike mwisho wake. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo katika nafsi zenu, basi mwogopeni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, (na) Mpole sana. (2:234-235)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa kizuka (mwanamke aliyefiwa na mumewe) anapokuwa katika eda harusiwi kuolewa wala hata kuposwa wala hata kudhihirishiwa nia ya kuolewa baada ya eda. Bali ni ruhusa kuweka azma moyoni na kuongea naye kwa wema bila kuidhihirisha azma hiyo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Mambo anayofanyiwa mtu anayekaribia kufa
Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut
Soma Zaidi...Hili ndio lengo la kufunga.
Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.
Soma Zaidi...Nguzo za swala ya maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...