Usawa katika uchumi wa kiislamu

5.

Usawa katika uchumi wa kiislamu

5. Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu



Kwa kuwa kuchuma kwa njia za halali ni wajibu kwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, hapana budi kila mtu kupewa uhuru kamili wa kutumia juhudi yake na vipawa vyake katika kuchuma kwa njia za halali. Katika Uislamu ni kosa kubwa kwa serikali au Dola kuweka vikwazo vya kuwazuia watu wasitumie vipaji vyao na uwezo wao wote katika kuchuma kwa njia za halali. Kinyume chake, serikali au dola ya Kiislamu ina wajibu wa kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia watu kutumia vipawa vyao vyote katika kuchuma na inawajibu pia wa kutoa motisha na vishawishi vya kuwavutia watu binafsi au watu waliojiunga katika vikundi wajiingize katika sekta mbali mbali za uchumi kwa juhudi kubwa na maarifa.


Pamoja na uhuru kamili uliotolewa na Uislamu wa kuchuma kwa njia za halali kwa kadri ya uwezo wa kila mtu, pia unampa kila mtu haki ya kumiliki kila alichokichuma kwa njia za halali kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:



β€œWala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma, na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma. Na mwombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mjuzi w a kila kitu. (4:32)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 641

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Mafungu ya mirathi katika uislamu

Mafungu ya urithi yaliyotajwa katika haya sita yafutayo:1.

Soma Zaidi...
Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)

- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.

Soma Zaidi...
Maana ya kusimamisha swala

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu

Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume.

Soma Zaidi...
Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Hii ndio hutuba ya ndoa ya kiislamu

Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha

Soma Zaidi...