Mifumo ya benk na uchumi wa kiislamu

Mifumo ya benk na uchumi wa kiislamu

7.

Mifumo ya benk na uchumi wa kiislamu

7. Mfumo wa benki
Mabenki ni taasisi za fedha ambazo ni muhimu sana katika uchumi. Benki husaidia uchumi kwa kutoa huduma kuu zifuatazo:



Kwanza, Benki hutoa huduma ya kuhifadhi akiba za watu na kuhifadhi mali zenye thamani kubwa kama vile dhahabu, na mfano wake.



Pili, kutokana na akiba inazozikusanya, benki hujikuta kila wakati ina fedha nyingi zisizo na shughuli yoyote. Benki hukopesha fedha hizi kwa watu wanaozihitajia ili ziwe mtaji wa kuendeleza biashara, viwanda, kilimo na sekta nyingine mbali mbali za uchumi na utoaji huduma.



Tatu, benki hutoa huduma ya kurahisisha malipo kwa njia ya hundi (cheque) kuwalipa Wafanyakazi kupitia benki zao au kwa hundi, huwaepusha walipaji na hatari ya ku ib iwa.



Nne, pia benki hutoa huduma ya kutoa malipo ya mbali popote pale penye matawi yake nchini au ulimwenguni. Huduma hii ni muhimu sana kwani huwapunguzia watu mzigo wa kusafiri na fedha nyingi mkononi.



Badala yake benki huidhinisha malipo kwa simu au kwa njia yoyote ya mawasiliano ya haraka katika tawi la Benki hiyo popote lilipo nchini au ulimwenguni kupitia kwenye Account ya huyo anayestahiki kulipwa.



Huduma hizi muhimu na nyinginezo nyingi ambazo hatukuzitaja hapa zinatudhihirishia umuhimu wa kuwepo taasisi hii ya fedha katika jamii. Hivyo ni dhahiri kwamba Uislamu ukiwa ni mfumo kamili wa maisha unaojitegemea kwa kila kitu, hautarajiwi ukapinga au ukaharamisha kuwepo kwa mabenki katika jam ii.Bali Uislamu u n ah aram is ha m ab en ki yanayoendeshwa kwa kipato cha riba.


Mabenki ya Riba
Mabenki ya kitwaghuti (yasiyokuwa ya Kiislamu) sehemu kubwa ya kipato chake hutokana na riba.
Mabenki ya Riba hukopesha watu wenye miradi mbali mbali ya uchumi na kuwatoza riba kubwa katika mfumo wa malimbikizo (compound interest). Sehemu ndogo ya riba inayokusanywa na Benki za Riba, hutumiwa katika kuwalipa wateja walioweka akiba zao ambao ndio hasa matajiri walioifanya Benki iwepo.



Ni kutokana na unyonyaji wa namna hii utakuta, wakati wakulima na Wafanyakazi wa ngazi za chini ambao ndio wanaovuja jasho ili kuchangia riba, hawajimudu katika kujipatia chakula, mavazi, na makazi bora, wenye mabenki wanagawa β€œbonus ” kwa wafanya kazi wao na wao wenyewe wanaponda starehe na anasa zilizopindukia kutokana na riba ambayo hawakuitoleo jasho lolote.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF
Views: 1630

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 web hosting     πŸ‘‰2 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)

Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi

Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna hizo hufanana. Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutwaharisha najisi mbalimbali.

Soma Zaidi...
Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali

Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali.

Soma Zaidi...