kwa nini riba ni haramu?
Uharamu wa Riba katika Uislamu
Kwanza, Uislamu umeharamisha riba kwa sababu ni dhulma (unyonyaji).Ukichukua mkopo wa riba uliochukuliwa kwa madhumuni ya kukidhi haja ya matumizi ya lazima ya nyumbani, utozaji wa riba unakiuka lengo la Allah la kuumba (kuleta) mali kwa wanadamu. Utaratibu aliouweka Allah ni kwamba kwa kuwa mali ameileta kwa wanaadamu wote:
“Yeye (Allah) Ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi...” (2:29).
Ni lazima matajiri (wenye mali) wawapatie wanyonge na wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha.
Pili, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu inahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge na kuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katika mgawanyo wa mali. Hii ni kinyume na mahitaji ya jamii. Uislamu unataka kila mtu apate mahitaji muhimu ya maisha. Hivyo wale walio na ziada ya mahitaji muhimu ya maisha wanatakiwa wawape wasionacho kabisa au wale waliopungukiwa kwa upendo na udugu. Riba inakanusha kabisa msimamo huu.
Tatu, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu hufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila ya kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishi kwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katika mabenki, bima, na vyombo vingine vya riba. Jamii inakosa mchango wa watu hawa katika uzalishaji na si hivyo tu, bali watu hawa wanakuwa mzigo na bughudha katika jamii. Ufasiki (uharibifu) wa aina zote katika ardhi hufanywa na kundi hili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Mambo yaliyo haramu kwa mwenye hedhi na nifasi
Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi
Soma Zaidi...Hii ndio hutuba ya ndoa ya kiislamu
Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha
Soma Zaidi...Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu
Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...