1.
1.Nadharia ya uchumi wa Kiislamu
Mfumo wa uchumi katika Uislamu ni utaratibu utokanao na Qur-an na Sunnah juu ya uzalishaji, umilikaji, usambazaji, na utumiaji wa mali na huduma pamoja na miiko yake. Kwa msingi huo, uchumi huo umejengwa juu ya fikra ya ukati na kati (Iqtisaad), hivyo umetofautiana na mifumo mingine iliyobuniwa na watu.
Dhana (concept) ya ukati (Iqtisaad) katika shughuli za kiuchumi ni kule kutoa uhuru kwa mtu binafsi (sekta binafsi) kuchuma na kumiliki mali ili iwe motisha kwake ya kuchapa kazi wakati huo huo serikali ikisimamia na kutoa miongozo katika uzalishaji na ugawaji, na vile vile kuwa na sekta zake (sekta za umma) ili kila mwana jamii apate haki za kimsingi. Mifumo iliyobuniwa na watu imeathiriwa na udhaifu wa kibinaadamu wa kuelemea upande huu au ule.
Ipo mifumo ya kiuchumi kama vile ubepari ambao umeelemea mno katika ubinafsi kiasi ambacho umepuuza kabisa haki za kijamii. Katika mfumo huu (ubepari) umma hauna chake; mali, huduma na shughuli mbali mbali hubinafsishwa. Wachache chini ya mfumo huu ndio hunufaika na rasilimali za Taifa. Hujilimbikizia mali, na motisha yao ya uzalishaji ni ile faida waipatayo. Serikali kuu ya mfumo huu wa kibepari hushirikiana na wachache hao waliohodhi mali, kuwanyonya walio wengi.
Pia, kuna mfumo wa uchumi wa Kikomunist au Kijamaa ambao nadharia yake imeelemea mno katika βusawaβ wa sare kiasi cha kudhoofisha mno motisha ya watu binafsi na hivyo kupelekea kukosekana kwa ufanisi katika uzalishaji. Katika mfumo huu mali na shughuli mbali mbali hutaifishwa (toka milki ya watu binafsi kuwa milki ya taifa).
Ukweli ni kwamba huwa si mali ya taifa kama inavyotangazwa bali mbiu ya βusawaβ, na βmali ya ummaβ, chini ya mfumo huu, ni mwavuli tu uliokinga kikundi cha watu kilichojipa mamlaka ya uendeshaji wa nchi kwa sura ya chama au serikali kwa maslahi ya kikundi hicho. Kikundi hicho ndicho humiliki na kutafuna mali huku wananchi wengi wakiendelea kudhulumiwa kwa sababu mbali mbali. Hivyo hakuna usawa ulio chini ya mfumo huu bali ni ubinafsi ule ule ambao huhamishwa toka kwa mtu binafsi kwenda kwenye kikundi fulani.
Umeionaje Makala hii.. ?
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala.
Soma Zaidi...Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu, masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...