3.
3.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu Kanuni kuu za uchumi katika Uislamu ni:
(i)Kumwamini Allah kuwa ndiye Muumba na mfalme wa ulimwengu huu yaani kumtii Allah katika mambo yote.
(ii)Binaadamu ni Khalifa wa Allah hapa duniani, hivyo wajibu wake ni kusimamisha amri ya Allah.
(iii)Ili kumsaidia mwanaadamu kutimiza wajibu wake kama Khalifa, Allah amemdhalilishia kila kitu katika ulimwengu huu:
βMw enyezi Mungu ndiye aliyekutiishieni bahari ili humo zipite merikebu kwa amri yake ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru β. (45:12).
βJe, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amevitiisha kwa ajili yenu vilivyomo ardhiniβ¦β (22:65)
βJe, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini na anakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? β¦β (31:20).
βYeye ndiye aliyefanya ardhi iweze kutumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika rizki zake na kwake ndiyo marejeo.β (67:15).
Hivyo kuzitumia neema hizo za Allah si dhambi bali ni katika kushukuru.
(iv)Kutokana na wajibu wa Ukhalifa wa Allah, mwanaadamu ataulizwa kwa neema alizompatia na atahesabiwa kwazo, ikiwa ni pamoja na namna alivyochuma na kutumia mali.
(v) Kuwa na mali au kutokuwa na mali nyingi au kidogo si dalili ya ubora au udhalili wa mtu. Hali zote mbili ni mtihani. Anachotazama Allah ni nyoyo za watu. Misingi au kanuni hizo zikithibiti katika moyo wa mtu zinakuwa na athari kubwa sana katika shughuli za kiuchumi za Muislamu.
Kanuni ya kwanza kwa mfano humfanya mtu afuate maamrisho ya Allah na hivyo atafanya kila njia ajiepushe na makatazo yake.
Pili, kwa kujua kuwa yeye ni Khalifa tu atajua yeye si mmilikaji wa hakika, hivyo atafuata maagizo ya huyo aliyempa ukhalifa yaani Allah.
Tatu, atajua kuwa utajiri si kitu cha kukipigania, bali mtu apiganie maisha bora na afya katika kutafuta radhi za Allah (s.w).
Nne, kwa kujua kuwa atahesabiwa na Allah anayeshuhudia kila kitu ataendesha shughuli zake za kiuchumi kwa kumcha Allah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Assalaam alykum warahmatullah wabarakatuh.
Soma Zaidi...Haki za UchumiKuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii.
Soma Zaidi...Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo.
Soma Zaidi...