Hadithi Ya 40: Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia
Hadithi Ya 40: Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia
الحديث الأربعون
"كن في الدنيا كأنك غريب أو عابر سبيل"
عن ابنِ عُمَرَ رضي اللهُ عنهما قال: أَخَذَ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبيَّ فقال : ((كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ، أو عابرُ سبِيلٍ)).
وكانَ ابنُ عُمَرَ رَضي اللهُ عنهما يقولُ: إذا أمْسَيْتَ فلا تَنْتظِرِ الصبَّاحَ، وإذا أصْبَحْتَ فلا تَنْتَظِرِ الَمسَاءَ، وخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرضِكَ، ومِنْ حَياتِكَ لِمَوْتِكَ.
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 40 KUWA DUNIANI KAMA VILE MGENI AU MPITA NJIA
Kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنهما ambaye alisema:
Mtume صلى الله عليه وسلم alinishika bega na akasema: Kuwa (ishi) duniani kama vile mgeni au mpita njia.
Naye Ibn 'Umar رضي الله عنه alikuwa akisema : Ukishinda hadi jioni usitaraji kuishi mpaka asubuhi, na ukiamka asubuhi usitaraji kuishi mpaka jioni, chukua uzima wako kwa ugonjwa wako (yaani fanya yale yote mema uwezayo wakati bado una afya nzuri kwani siku ukiumwa hutoweza kuyafanya), na uhai wako kwa kifo chako (tumia maisha yako vizuri kwa kufanya amali njema maana ukishafariki hakuna tena uwezalo kulifanya).
Imesimuliwa na Al-Bukhari
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Darsa 5: Kujiepusha na tabia za unafiki na kutimiza ahadi
Katika Darsa hii tutajifnza kuhusu kujiepusha na tabia za unafiki na kitimiza ahadi.
Soma Zaidi...MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.
Soma Zaidi...