NIZIPI FADHILA ZA KUSOMA QURAN?

NIZIPI FADHILA ZA KUSOMA QURAN?

Quran ni maneno ya Allah yaliyofunuliwa kwa mtume Muhammad (s.a.w) kwa kupitia Malaika jibril. Quran imetufikia sisi kwa hatua. Na duniani imeshuka kwa muda wa miaka 23 vipande vipande, sura kwa sura hata ikatimia yote yenye sura 114, aya 6236, yenye herufi 330,709 maneno 77,449. quran ni kitabu pekee ambacho usahihi wake unaweza kuthibitika kwa kutumia sayansi na teknolojia, ushahidi wa kihistoria juu ya mambo yaliyozungumzwa kuhusu kutokea kwake. Usahihi katika utoaji taarifa wake, muundo wa maneno yake na mengineyo mengi.

 

Wasomaji wa qurqn wanapata hali flani ya utulivu wa nafsi pindi wanapoisoma kisahihi kwa kuzingatia. Na hili si kwa wasomaji tuu bali hata kwa wasikilizaji wa quran. Kwa hakika kuna gfaida kubwa sana katika kusikiliza na kusoma qurana. Lakini je ni Zipi faida hizo?. makala hii itakwenda kukuletea faida ama fadhila za kusoma quran sambamba na hilo pia tutakwenda kuziona faida za kusikiliza quran inaposomwa.

 

Makala hii imeandaliwa na Al-Ustadh Rajabu Athuma na kusambazwa katika tovuti hii. Unaweza kutuunga mkono kwa kazi hii kwa kushea na wengine ama kuhariri makala hizi, ama kukosoa makosa ama kuongezea maarifa katika pale palipo pungua. Hatulipwi kwa kazi hii, tunatarajia malipo kwa Allah.

 

NI ZIPI FADHILA ZA QURAN?

 

 

Kama nilivyotangulia kukwambia kuwa kuna ubora mkubwa katika kuzoma quran. Sasa hebu tuzione fadhila hizo bila ya kupoteza muda.

 

 1. Katika hadithi iliyopokewa na Abuu Umamah ni kuwa :Mtume Muhammad (s.a.w) amesema kuwa “somenu quran kwani hakika ya hiyo quran italetwa siku ya qiyama kuja kumuombea mtu aliyekuwa akiisoma” (Muslim)

عن أَبي أُمامَةَ رضي اللَّه عنهُ قال : سمِعتُ رسولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : » اقْرَؤُا القُرْآنَ فإِنَّهُ يَأْتي يَوْم القيامةِ شَفِيعاً لأصْحابِهِ « رواه مسلم

Hadithi hii inatueleza mambo yatakayotokea siku ya qiyama. Kwanza tutambuwe kuwa siku ya qiyama hakuna yeyote yule atakayezungumza ila yule atakayepewa idhini na Allah na atazungumza ukweli tupu (quran-surat An-Nabai). na katika aya zingine Allah anatuambia kuwa siku hiyo hatutaweza kuzungumza kwa midomo kwa midomo itakuwa imefungwa, na hivyo viungo kama miguu na mikono ndio vitazungumza uyataja yale tuliokuwa tukiyafanya (quran-sural Yasin). na katika aya nyingine Allah anatueleza kuwa mpaka ngozi zitatowa ushahidi kwa yale tuliokuwa tukiyafanya.

 

Hivyo katika hali kama hii kuna wengine watakuwa karibu kuingia motoni, wengine watakuwa tayari wamehukumiwa moto, na wengine katika hali tofautitofauti.basi hapo na quran itapewa ruhusa ya kumtetea mtu ambaye alikuwa akiisoma. Hivyo ndo maana Mtume wa Allah ametutaka sana tusome quran (rejea hadithi hapo juu).

 

 1. Kwa hakika hali ya siku ya qiyama ni hali ngumu na nzito sana. Siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli cha Arsh ya Allah. Jua litavutwa karibu sana na vichwa vya watu, majasho yatakaribua kufunika watu, katika hali hiyo watu wakiwa wanahukumiwa kwa wema wao, siku hiyo baba hatamsaidia mama, hakutakuwa na wakili wa kukutetea mbele ya hakimu Allah hakimu wa mahakimu (quran-sural At-tiin). basi Allah ataleta baadhi ya sura za quran zije kukutetea mtu aliyekuwa akiisoma quran huku duniani sra hizo ni surat al-Baqarah ikifuatiwa na surat al-’Imran.

 

عَن النَّوَّاسِ بنِ سَمعانَ رضيَ اللَّه عنهُ قال : سمِعتُ رسول اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : »يُؤْتى يوْمَ القِيامةِ بالْقُرْآنِ وَأَهْلِهِ الذِين آانُوا يعْمَلُونَ بِهِ في الدُّنيَا تَقدُمهُ سورة البقَرَةِ وَآل عِمرَانَ ، تحَاجَّانِ عَنْ صاحِبِهِمَا « رواه مسلم

Imepokewa hadithi kutoka kwa An-Nawwas bin Sam`an (r.a) kuwa amesema nimemsikia Mtume wa Allah akisema: “Italetwa siku ya qiyama quran na mtu wake aliyekuwa akiisoma na kuifanyia kazi (italetwa) surat al-baqarah na surat Al-’Imran (zitakuwa) zikitoa hoja kumtetea mtu wao. (Muslim).

 

 1. Katika mapokezi mengine Mtume (s.a.w) kuwa mtu aliye bora ni yule anayejifunza quran kisha akaifanyia kazi.

عن عثمانَ بن عفانَ رضيَ اللَّه عنهُ قال : قالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : » خَيرآُم مَنْ تَعَلَّمَ القُرْآنَ وَعلَّمهُ رواه البخاري

 

Imepokewa hadithi kutoka kwa ‘Uthman Ibn ‘Afan kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mbora wenu ni yule mweye kujifunza quran kisha akaifanyia kazi” (Bukhari). Hadithi hii inatupa mafunzo kuwa mbora katika watu si tajiri, ama mtoaji sadaka sana ila mbora ni yule aliyejufunza quran na kuifanyia kazi kwa kuisoma na kufuata maamrisho yake na makatazo yake. Na hii ndio uchamungu wenyewe.

 

 1. Katika Hadithi nyingine tunajifunza kuwa Allah hupandisha watu darja kwa hii quran. Imepokewa hadith kutoka kwa ‘Umar Ibn Al-Khataab kuwa Mtume (s.a.w) amesema “hakika Allah hupandihs (darja) watu kwa hii quran na kushusha (darja) watu kwa hii quran” (Muslim)  

 

عن عمرَ بن الخطابِ رضي اللَّه عنهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » إِنَّ اللَّه يرفَعُ بِهذَا الكتاب أَقواماً ويضَعُ بِهِ آخَرين « رواه مسلم

 

 1. Kwa hakika inafaa kabisa kumuonea wivu yule ambaye anaisoma quran na kuifanyia kazi. Katika hadithi mtume (s.a.w) anazungumza kuhusu husda na kuwa kuna watu aina mbili inafaha kuwaonea husda kwa ajili ya Allah na si kwa ubaya wowote. Miongoni mwa watu hao ni yule aliyeisoma quran na kuifanyia kazi.

 

عنِ ابن عمر رضي اللَّه عنهما عن النَّبِيِّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » لا حَسَدَ إلاُّ في اثنَتَيْن : رجُلٌ آتَاهُ اللَّه القُرآنَ ، فهوَ يقومُ بِهِ آناءَ اللَّيلِ وآنَاءَ النَّهَارِ ، وَرجُلٌ آتَاهُ اللَّه مالا ، فهُو يُنْفِقهُ آنَاءَ اللَّيْلِ وَآنَاءَ النهارِ « متفقٌ عليه .

«والآناءُ « : السَّاعات

Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) ambaye anesema: “Hukuna hasadi ila kwa watu aina mbili. Mtu wa kwanza ni yule a,baye Allah amempa quran naye akawa anasimama kuifanyia kazi (kwa kuisoma na kuifata) wakati wa mchana na usiku, na mtu wa pili ni yule ambaye Allah amempa mali naye akawa anasimama kwa kuitoa (kuifanyia kazi kwa ajili ya Allah) mchana na usiku (Bukhari na Muslim).

 

Husda hii si kwa ajili ya mabaya bali ni kwa ajili ya Allah, yaani ni hali ya kutamani kile ambacho mwenzio anacho. Haya yote yafanyike kwa lengo la kutaka radhi za Allah na si vinginevyo, bila ya kusababisha madhara kwa yeyote.

 

 1. Msomaji wa qurqn anapata sakina yaani utulivu. Huu ni utulivu, yaani mtulizano wa nafsi, fikra (akili) na mwili. Utulivu huu humpata pindi anaposoma quran.

عنِ البُراء بنِ عَازِبٍ رضيَ اللَّه عَنهما قال : آَانَ رَجلٌ يَقْرَأُ سورةَ الكَهْفِ ، وَعِنْدَه فَرسٌ مَربوطٌ  بِشَطَنَيْنِ فَتَغَشَّته سَحَابَةٌ فَجَعَلَت تَدنو ، وجعلَ فَرسُه ينْفِر مِنها . فَلَمَّا أَصبح أَتَى النَّبِيَّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم .فَذَآَرَ له ذلكَ فقال : » تِلكَ السَّكِينَةُ تَنَزَّلتْ للقُرآنِ « متفقٌ عليه .

«الشَّطَنُ « بفتحِ الشينِ المعجمةِ والطاء المهملة : الْحَبْلُ

Imepokewa hadith kutoka kwa A-bara Ibn ‘Azib (r.a) kuwa alikuwa mtu mmoja (katika masahaba) akisoma quran surat al-kahaf na pembeni yake kulikuwa na farasi akiwa amefungwa kamba. Basi wakati alipokuwa akisoma quran kulikuwa na kiwingu kikishuka karibu yake, kikawa kinaendelea kushuka, na huku farasi akiwa akihangaika huku na huko. Basi mtu yule alipoamka asubuhi akamueleza mtume kuhusu mambo yaliyotokea. Mtume (s.a.w) akamwambia: “hicho (kiwingu) ilikuwa ni sakina (utulivu) hushuka kwa kusoma quran. (Bukhari na Muslim)

 

 1. Kwa hakika kuna ubora na fadhila nyingi sana katika kusoma quran. Kwani kila herufi moja ya quran utakayoisoma utapata mema (thawabu) kumi. Kama tulivyoona hapo juu kuwa quran ina herufi 330,709 hivyo atakayesoma quran yote ataweza kupa thawabu 3,307,090 hiki ni kiwango cha chini, lakini Allah analipa zaidi ya hapo mpka kila jambo jema mmara 700.

 

عن ابن مسعودٍ رضيَ اللَّه عنهُ قالَ : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : منْ قرأَ حرْفاً مِنْ آتاب اللَّهِ فلَهُ حسنَةٌ ، والحسنَةُ بِعشرِ أَمثَالِهَا لا أَقول : الم حَرفٌ ، وَلكِن : أَلِفٌ حرْف،ٌ ولامٌ حرْفٌ ، ومِيَمٌ حرْفٌ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح

Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn Mas’ud kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mwenye kusoma herufi moja (katika quran) Allah atampa jema. Na jema mojqa hulipwa mara 10….

 

 1. Waislamu wanatakiwa waisome quran na kuihifadhi katika vifua vyao. Kwa hakika kuna faida kubwa katika kuhifadhi quran. Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya muislamu anayesoma quran na yule asiyesoma quran. Muislamu asiyesoma quran ni sawa na jumba bovu.

 

عنِ ابنِ عباسٍ رضيَ اللَّه عنهما قال : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : »إنَّ الَّذي لَيس في جَوْفِهِ شَيْءٌ مِنَ القُرآنِ آالبيتِ الخَرِبِ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح

Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn ‘Abas (r.a) kuwa amesema: Amesema Mtume (s.a.w) kuwa: “hakika yule ambaye hakuna katika kifua chake  (yaani hakuhifadhi) chochote katika quran ni sawa na jumba bovu”. (Tirmidh)

 

 1. Kutakuwa na kuachana kukubwa sana kwa darja peponi kati ya waliohifadhi quran na wale ambao hawakuihifadhi. Watakaoingia peponi wataambiwa soma quran, hapo kila atakayesoma aya atakuwa akipanda daraja, atapanda kadiri ya aya atakazozisoma.

 

عن عبدِ اللَّهِ بنِ عَمْرو بن العاصِ رضي اللَّه عَنهما عنِ النبيِّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » يُقَالُ لِصاحبِ الْقُرَآنِ : اقْرأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ آَما آُنْتَ تُرَتِّلُ في الدُّنْيَا ، فَإنَّ منْزِلَتَكَ عِنْد آخِرِ آيةٍ تَقْرَؤُهَا « رواه أبو داود ، والترْمذي وقال : حديث حسن صحيح

Imepokewa hadithi kutoka kwa ‘Abdallah Ibn ‘Umar Ibn Al-’Aas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa amesema: “Itaambiwa kwa mtu (msomaji wa quran siku ya qiyama) “soma na na upande (daraja) na uisome (tartila) kama ulivyokuwa ukiisoma duniani. Kwani kwa  hakika mafikio (daraja) yako yatakuwa ni mwisho wa aya yako (utakayoisoma mwisho)” (Abuu Daud)

 

MWISHO

Kwa hakika tunatakiwa kusoma sana qurani na kuihifadhi, na katu kusiiwache ikatitoka. Mtume (s.a.w) amekataza sana vikali kuisahau quran. Darsa lijalo tutakwenda kuangalia makatazo juu ya kuisahau quran baada ya kuihifadhi. Msomaji wa quran anakuwa tofauti na asiyeisoma kwani msomaji anapata faida nyingi kama tulivyoziona.

 

Ndugu yangu Muislamu, tunakuomba utuunge mkono kwa kazi hii. Kwani ni sadaka yenye kuendelea. Hatufanyi hii kazi kwa kulipwa ni radhi za Allah ndio tunatarajia. Unaweza kutuunga mkono kwa kuongeza maaraifa katika darsa zeu, kurekebisha makosa ya kiuandishi, kushea darsa hizi kwa wengine.

MAKALA NYINGINE ZAIDI

 1. DARSA ZA FUNGA
 2. DARSA ZA DUA
 3. DARASA LA AFYA
 4. AFYA YA UZAZ
 5. DARSA ZA SIRA