MAKATAZO DHIDI YA KUISAHAU QURAN BAADA YA KUIHIFADHI

MAKATAZO DHIDI YA KUISAHAU QURAN BAADA YA KUIHIFADHI

MAKATAZO JUU YA KUISAHAU QURAN BAADA YA KUIHIFADHI

 

Kuifadhi quran ni jambo linalotakiwa sana kwa Muislamu kulifanya. Kwani tusipofanya hivyo tunaweza kukosa faida nyingi. Maulamaa wameweka njia mbalimbali katika kusaidia kuihifadhi quran. Na Mtume pia ametueleza baadhi ya njia hizo ikiwemo kuisoma quran mara kwa mara. Laini leo watu wengi waliohifadhi quran wamesha sahau. Wapo waliohifadhi msahafu mzima na kusahau, na wapo waliohifadhi baadhi tu ya sehemu na kuzisahau.

 

Mtume (s.a.w) amekataza vikali kuiwachia quran kuisahau baada ya kuihifadhi. Katika makala hii tutakwenda kuona baadhi ya makatazo juu ya kuisahau Quran. Ndugu yangu muislama, kabla ya kuianza Darsa yetu ningependa kukwambia kuwa elimu hii unaipata bure, tunafanya kazi hii kwa ajili ya Allah na hakuna anayetulipa. Tunakuomba utuunge mkono kwa kuongeza maarifa katika makala za dini kama hizi, ama kuharir i(edit)  makata zetu ama kushea makala hizi.

 

Kwa hakika makataz juu ya kuisahau quran baada ya kuihifadhi yanawahusu waislamu wote. Katika Hadithi mbalimbali Mtume (s.a.w) anahimiza waislamu waisome quran mara kwa mara na katu tusiiwache ikapoteka au kuisahau. Hadithi zifuatazo zinaonesha mahimizo juu ya kutoisahamu quran

 

' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' : » ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' « ' '

Imepokewa Hadith kutoka kwa Abuu Musa kuwa Mtyme (s.a.w) amesema: “isomeni quran mara kwa mara kwani kwa hakika naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo Mikononi mwake, (hiyo quran) inakimbia haraka (kutoka kwenye moyo bada ya kuhifadhiwa) kuliko ngamia (anavyokimbia) kwenye kamba aliyofungiwa” (Bukhari na Muslim)

 

Hadithi hii inatupa mafunzo kadhaa kama:

 

Miongoni mwa njia za kuwezesha kusoma quran mara kwa mara ni katika swala za usiku. Mtume (s.a.w) alikuwa swala za usiku akisoma sura ndefu sana. Wakati mmoja aliswali na sahaba mmoja basi katika rakaa ya kwanza alisoma surat al-Baqarah yote na Sura inayofata yote.

 

' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' : » ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' « ' '

Imepokewa Hadith kutoka kwa Ibn ‘Umar kuwa Mtume (s.a.w) amesema “Mfano wa mtu aliyehifadhi quran ni sawa na mfano wa mtu mwenye ngamia, akimfunga vyema ataweza kuwa naye lakini akimuachia atakwenda (mbali). (Bukhari na Muslim)

 

Hadithi hii pia inatupa funzo kuwa endapo tusipo ikamata quran vyema kwa kuisoma mara kwa mara basi ni rahisi kukumbia na hivyo tukapata taabu wakati wa kuirudisha tena kama atakavyopata taabu mmiliki wa ngamia pindi alipomwachia ngamia wake na kupotea hivyo akataka kumrudisha.

 

JE KUISAHAU QURAN NI MADHAMBI?

Maulamaa kwama Imam Suyut na Imam Nawaw wao wanaona kuwa kusahau quran ni katika madhambi makubwa. Kuna hadithi wanaitegemea juu ya msimamo wao huu. Wapo baadhi ya watu waliwacha kabisa kuhifadhi quran wakihofia adhabu pindi watakapoisahau. Tafadhali soma makala hii mpaka mwisho.

 

Kusahau ni jambo la kawaida kwa mwanadamu, na ndio maana mwanadamu ameitwa insan yaani mwenye kusahau. Kusahau ni sifa katika sifa za mwanadamu. Kwama ilivyo unaweza kusahau chochote hata hivyo unaweza pia kusahau quran. Hivyo Allah hawezi kukuadhibu kwa sifa hii ya kusahau. Na ndio maana hata swala unaweza kusahau na ukajakuiswali muda utakapokumbukwa. Lakini ni kwa nini maulamaa wamesema ni madhambi makubwa?

 

Maulamaa wanaosimama na msimamo wa kuwa mwenye kusahau quran yupo kwenye madhambi wanafuata hadithi ya Mtume (s.a.w). lakini uchambuzi wa hadith hii unaonyesha kuwa hadithi hii ni dhaifu (yaani sio sahihi) haina nguvu katika kutoa hukumu kama hii. Kwa ufupi hadithi hiyo ni:-

 

Imepokewa hadithi kutoka kwa Anas Ibn Maalik (r.a) ambaye amesema: ‘nilionyeshwa madhambi ya ummati wangu, na sikuona dhambi kubwa zaidi ya dhambi la mtu ambaye mepewa (amesaidiwa kuhifadhi) sura ama aya katika quran kisha akaisahau”  hadithi hii imetajwa kuwa ni Dhaifu na Imam Bukhar na Imam Tirmidh na ameitaja pia imam Al-Alban kuwa ni dhaifu. Allh ndiye anajuwa zaidi.

 

 

MWISHO:

Napenda kuhitimisha darsa hii kwa kuwakumbusha ndugu zangu waislamu kuhusu kutilia mkazo jambo hili la kuhifadhi quran na kuisoma mara kwa mara. Kuwa pamoja nasi kwenye darsa zijazo za quran, kama fadhila za baadhi ya sura kwenye quran, quran na sayansi, darsa za dua na darsa za ndoa na talaka.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 172

Post zifazofanana:-

Hadithi Ya 41: Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Mapenzi Yake Yatakapomili (yatakapoendana) Na Yale Niliyokuja Nayo
Soma Zaidi...

Muhtasari wa madili malezi ya jamii kama ilivyobainishwa katika Qur-an
(v)Kuwaombea dua wazazi. Soma Zaidi...

DARASA LLA AFYA na afya ya uzazi na malezi bora kwa jamii
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kisa cha Malkia wa Sabaa.
Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ISHAQA NA YAQUB
Soma Zaidi...

Kupanga uzazi na uzazi wa mpango katika uislamu
Soma Zaidi...

Mafunzo ya swala
Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike? Soma Zaidi...

KITABU CHA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

MAZINGIRA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu
VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza 'wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi' alibakia kimya ... Soma Zaidi...

DUA ZA WAKATI WA SHIDA
DUA ZA WAKATI WA SHIDA 1. Soma Zaidi...

NJIA ZA KUJIKINGA NA MALARIA (zijue njia za kupambana na mbu wa malaria)
Soma Zaidi...